Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-14 18:36:57    
Opera ya Dixi ya Guizhou

cri

        

    Katika vijiji vyenye majina ya "tun, bu, qi, ying, guan, shao na chang", vilivyoko ndani ya eneo la mamia ya kilomita za mraba linalozunguka Mji wa Anshun, jimboni Guizhou, kunaishi aina pekee zote za matamshi ya lugha, mila na desturi, mavazi na ufuataji wa dini, watu hawa wanatofautiana na Wahan na watu wa makabila mengine madogo wa huko. Watu hao ndio Watunbu waliotokea mara kwa mara katika vitabu vya historia ya China.

    Mwaka wa 14 wa utawala wa Hongwu wa Enzi ya Ming (1368-1644), ili kuimarisha utawala wake, Mfalme Zhu Yuanzhang aliongoza jeshi lake kuingia Jmbo la Guizhou. Kwa ajili ya kuzoea mazingira ya vita na kulinda usalama wa maisha yao, vikosi vya jeshi hili vilivyokaa sehemu ya Anshun vilijenga ukuta kwenye kambi zao na vituo vya ulinzi. Askari hawa wa Kihan na Wahan waliofika baadaye katika kipindi cha mwisho wa Enzi ya Ming na Enzi ya Qing kufuatana na mpango wa mfalme wa "kupeleka askari Guizhou", walikuwa sehemu kuu ya wenyeji wa Anshun. Malaki ya Watunbu wanaoishi huko leo ndio wajukuu wa vizazi vya askari wa vikosi vile vya zamani.

    "Tun" vilikuwa ni vjijiji vya kijeshi na "bu" vilikuwa ni vijji vya raia. Wakati ule wakulima wa Kihan waliohamia huko kutoka majimbo mengine walifyeka ardhi bikira na kulima kwa ajili ya kutoa mahitaji kwa jeshi na pia walifnaya kazi za kupeleka barua na nyaraka na kuwakaribisha na kuwasindikiza maofisa wa serikali. Kwa sababu, "tun" na "bu" vilijengwa kwenye maeneo ya tambarare, yenye ardhi ya rutuba, karibu namaji na kando ya njia ya usafiri, kwa hivyo maisha na hali ya uchumi ya Watunbu ilikuwa ni nzuri kuliko wenyeji wa huko. Hali hiyo imedumisha utamaduni wa kieneo, inatupiwa macho na watu wengi.

    Opera ya Dixi ilitokana na michezo ya kuingiza mungu wa kufukuza maradhi ya mashetani. Wengi wa askari wa jeshi la Zhu Yuanzhang walitoka majimbo ya kusini ya Mto Changjiang, sehemu zilizovuma kwa michezo hiyo. Mfalme Zhu Yuanzhang alitia motisha michezo hiyo yenye kazi za kutambika, kufanya mazoezi ya mwili na kustarehesha katika jeshi lake, ili kuinua moyo wa askari wake wa kupigana na kuimarisha utawala wake. Miaka nenda miaka rudi, kusudi la mwanzo la kijeshi lamichezo lilitoweka, bali opera ya Dixi ikiwa ni hali ya utamaduni iliyopokezana kizazi kwa kizazi imeota mizizi katika maisha ya Watunbu.

    Katika miaka 600 iliyopita, opera ya Dixi ilitajirisha utamaduni wa Watunbu na watu wa makabila mengine madogo ya huko, vilevile ilishikilia moyo wa Watunbu wa kujikumbusha mambo ya zamani. Opera ya Dixi inachezwa kwenye uwanja wa ardhi tambarare usio najukwaa, michezo yenyewe huonyesha hadhithi za vita vilivyotokea katika historia. Kwa hivyo, opera hiyo husifiwa ni "kisukusuku hai cha opera".

    Opera ya Dixi ni harakati ya michezo ya Watunbu ya kukumbuka maisha ya vita, kuwakumbuka mababu na kuomba baraka. Maisha ya jeshini y awatangulizi wa Watunbu yaliwafanya waheshimu moyo wa ushujaa wa askari na walipenda sana mashujaa wenye utiifu kama Xue Rengui, Di Qing na Yue Fei, ambao walikuwa majenerali wakuu wa jeshi kutoka askari wa kawaida na baada ya mapigano ya kishujaa katika historia ya China. Hii ndio nguzo ya moyo wa ndani wa michezo ya opera ya Dixi. Hii ilitilia mkazo nguvu ya kukusanyika kwa Watunbu wa kale waliohamia Guizhou wakati walipopambana na mabadiliko ya mazingira, vita vikali na upinzani wa wenyeji; kwa Watunbu wa leo, kucheza michezo hiyo ni kuwakumbuka mababu zao, kuonyesha heshima kwa mashujaa. Kwa hivyo, Watunbu wanaipenda opera ya Dixi na kurithi kizazi baada ya kizazi. Kwa sababu ya upendo huo mkubwa, wakati wa maonyesho wachezaji na watazamaji wote wanasisimka kwa hisia tele, wachezaji huingia katika hali ya hadithi kiasi cha kujisahau na watazamaji huzama katika hali ya vita vikali vya michezo.

    Kutoka tarehe 1 hadi 18 mwezi wa kwanza katika kalenda ya China, kila mwaka, Watunbu wanacheza michezo ya hadithi hizohizo na kuonyesha historia sawasawa lakini wachezaji na watazamaji, wazee kwa watoto, wanaume kwa wanawake, wote wanafurahi sana katika harakati hiyo bila ya kujali upepo na baridi kali. Wataalamu, wasomi na watalii kutoka nchini na nchi za nje kwa safari maalumu ya kutazama michezo ya opera ya Dixi, wote walivutwa na utamaduni huo pekee wa kale na pia kuzama ndani yake.

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-14