Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-15 18:02:52    
Mapishi Yanayochapukia

cri
    Watibet ni wakarimu na wanyofu. Wamezoea kuwaalika wageni watembelee nyumbani mwao. Baada ya kuingia chumbani na kukaa, mwenyeji humkaribisha mgeni kwa chai ya samli ya moto huku muziki nyororo ukipigwa. Wakati wa chakula, mezani huandaliwa samli, zanba (kama ugali, lakini ilitengenezwa kwa unga wa shayiri na samli), pombe ya qingke na nyama. Wenyei hawaachi ukarimu wao mpaka wageni wameshiba sana au karibu kulewa.

    Samli, zanba na chai ni "hazina tatu" za chakula cha Watibet.

    Samli ni mafuta yaliyotenganishwa kutoka kwenye maziwa ya ng'ombe na mbuzi (au kondoo). Watibet wanapenda zaidi samli iliyotenganishwa kutokana na yak, ambao ni aina mojawapo ya ng'ombe wa Nyanda za Juu za Tibet. Kwa kulinganisha samli ya ng'ombe na kondoo, ile ya ng'ombe inaishinda ile ya kondoo kwa ladha na lishe.

    Katika maisha ya Watibet, samli ina matumizi mengi sana. Moja kati yao ni kupikia chai ya samli. Njia ya upikiaji ni kama ifuatayo: kwanza hupika "tofali" la chai mpaka kuwa rojo, baadaye hutia samli na chumvi kidogo na kutia ndani ya ndoo, hukoroga kwa muda mrefu mpaka mafuta na maji vichanganyike vizuri. Baada y ahapo humiminwa ndani ya birika la towe au madini, baada ya kupasha moto kidogo, chai namna hii inaweza kunywewa. Chai ya samli ina vijenga mwili vingi, kwa kuwa ina wingi wa vitamini za aina mbalimbali, mafuta na protini ya juu. Kunywa chai ya samli kunaweza kukata kiu, njaa na kuzuia midomo isipasuke. Watibet wanatia maanani sana unywaji wa chai ya samli. Wanakubali kuviacha vyakula vingine, lakini hawawezi kuiacha chai ya samli hata siku moja.

    Chakula kikuu cha Watibet ni zanba, ambayo hupikwa kwa unga wa kukaangwa washayiri. Upikaji wake ni tofauti na unga wa kukaangwa wa kawaida. Shayiri hukaangwa kwanza, kisha kusagwa. Shayiri iliyokaangwa ni kama maua meupe madogo, inanukia vizuri na ina ladha tamu. Wasichana na wavulana wanapenda kuila kama vitafunio.

    Wakati wa kula zanba, kwanza mlaji anaitia ndani ya bakuli, baadaye anamiminia chai ya samli, kisha anakoroga kwa mikono na kuitumia kama ugali. Kwa watu wa kawaida, chakula chao cha mara moja ni zanba na chai ya samli tu. Kwa ajili ya sherehe, wanaongeza pombe ya qingke na nyama. Pombe hiyo ina harufi nzuri, ladha lamu na kali kidogo. Ndiyo maana, inapendwa kunywewa na watu wote, wanaume na wanawake, wazee na vijana. Wakati wa kunywa pombe, Watibet huipika samli kwenye midomo ya birika au kingo za mabakuli ya pombe, kusudi kutoa heshima kwa Mwenyezi Mungu, kufuatilia mbali ubovu na kuomba dua ya baraka. Nyama ya ng'ombe na mbuzi, hukatwa vipande vikubwa na kupikwa pamoja na mifupa. Wakati wa kula, mlaji anashika nyama kwa mkono huku akikata kwa kisu kidogo.

    Watibet pia wanakaanga kwa mafuta ya samli aina nyingi za chakula cah unga wa ngano, kutengeneza soseji za damu ya ng'ombe na kondoo.

    Hapo zamani, Watibet hawakulima mboga, kwa hivyo vyakula vyao vilikuwa vyepesi. Sasa, licha ya kulima mboga katika mashamba, wanailima ndani ya mabanda makubwa ya joto wakati wa majira y abaridi. Vyakula vya Watibet vitazidi kuwa bora siku baada ya siku.

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-15