Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-15 18:19:06    
Mpunga uliobadilishwa "gene" kupata msingi wa kuoteshwa kwa kiwango kikubwa nchini China

cri

    Teknolojia ya kupata mbegu za mpunga uliobadilishwa "gene" (transgenic) wenye uwezo wa kujikinga dhidi ya wadudu waharibifu iko tayari nchini China na wakati wowote inaweza kukaguliwa na kutambulika rasmi.Tarehe 6 wataalamu wa Idara ya Sayansi na Teknolojia ya Mkoa wa Fujian walikagua teknolojia ya kupata mbegu za mpunga uliobadilishwa "gene" wenye uwezo wa kujikinga na wadudu waharibifu, na walithibitisha kuwa teknolojia hiyo tayari imekwisha pevuka na imekuwa na msingi imara wa kuzalisha mbegu za mpunga huo kwa kiwango kikubwa.

    China ni nchi yenye ufanisi mkubwa wa kukchanganya sifa bora za aina tofauti za mpunga, kwa makadirio nchi ya China itakuwa na hakimiliki ya teknolojia ya kisasa kabisa duniani katika uzalishaji mbegu za mpunga uliobadilishwa "gene". "Mradi wa uzalishaji mbegu za mpunga wenye "gene" ya kukinga wadudu waharibifu" na "Utafiti wa mfumo wa uzalishaji mbegu za mpunga uliobadilishwa "gene" wenye uwezo wa kijikinga na wadudu waharibifu" ni miradi miwili mikubwa ya sayansi na teknolojia mkoani Fujian. Miradi hiyo ilishughulikiwa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Kilimo cha Mkoa wa Fujian na kusaidiwa na Taasisi Kuu ya Sayansi ya China. Wataalamu kutoka ndani na nje ya mkoa huo wanaona kuwa miradi hiyo imepata mafanikio makubwa, na mafanikio yenyewe ni kama yafuatayo:

    Mfumo wa kuzalisha mbegu za mpunga wenye "gene" ya kujikinga na wadudu waharibifu umekamilika. Umewekwa utaratibu wa kuchagua mpunga wenye uwezo mkubwa zaidi wa kujikinga na wadudu waharibifu na wenye urithi bora tulivu, na mpunga wenye sifa hizo umepatikana kwa wingi ambao ni akiba kubwa ya mpunga wenye mabadiliko ya "gene".

    Kuchanganya aina kadhaa za mpunga wenye uwezo wa kujikinga na wadudu waharibifu na mwishowe kuchagua mpunga wenye aina tatu za "gene" kushiriki katika majaribio ya kisehemu na mpunga wenye aina nne za "gene" kushiriki katika majaribio ya mkoa na imepata akiba kubwa ya mbegu za mpunga wenye uwezo mkubwa wa kujikinga na wadudu waharibifu.

    Aina 45 za mpunga zimepata alama ya kutokuwa na madhara kwa binadamu baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kisayansi.

    Umewekwa mfumo wa kubadilisha "gene" ya mpunga, na kiasi cha mabadiliko ya "gene" ni zaidi ya 5%, muda wa mabadiliko ni ndani ya wiki 12, na mimea ya mpunga huo zaidi ya 2000 inaweza kupatikana kwa mwaka.

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-15