Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-19 17:51:36    
Barua za wasikilizaji 1019 (b)

cri

    Wasikilizaji wapendwa, ni watangazaji wenu Chen na Fadhili Mpunji tunawakaribisha katika kipindi hiki cha sanduku la barua. Leo kwanza tunawasomea barua tulizopokea kutoka kwa wasikilizaji wetu, na baadaye tutawaletea makala ya tatu ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa Miaka 55 ya China mpya.

   Msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa shule ya msingi kiliwi, mwamashimba division, sanduku la posta 1421, Mwanza Tanzania, ametuletea barua akisema ana tumaini kuwa wafanyakazi na watangazaji wote wa Redio China Kimataifa hatujambo na tunaendelea kuchapa kazi kuwatangazia habari motomoto wasikilizaji wetu kutoka Radio China Kimataifa.

    Anasema anapenda kutumia fursa hii na kwa dhati kabisa kuishukuru Redio China Kimataifa kwa kuwatangazia wasikilizaji wake habari zinazohusu China, Asia na ulimwengu kwa jumla. Vilevile anapenda kuishukuru Redio China Kimataifa kwa kuwapa wasikilizaji kumbukumbu ya lugha ya kichina ambayo mpaka sasa ni miaka mingi iliyopita tangu lugha hiyo ivumbuliwe.

    Pia anapenda kutoa shukrani zake nyingi na za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuwakaribisha viongozi wa mataifa mbalimbali ya ulimwengu kuhudhuria mkutano wa kupunguza umaskini duniani. Akiwemo rais wao mpendwa wa Tanzania mheshimiwa Benjamin William Mkapa ambaye ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Mkutano huo ulifanyika huko Shanghai ambao ulihusu upunguzaji wa umaskini duniani. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na marais wa nchi mbalimbali, akiwemo rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, rais Da Silva wa Brazil na wengine mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.

    Anasema anaishukuru Jamhuri hii ya watu wa China kwa kuwakaribisha viongozi hao wote katika mkutano huo wa kupunguza umaskini duniani. Vilevile anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa viongozi wote wa Jamhuri ya Watu wa China. Wakiwemo rais wa China, waziri mkuu wa China pamoja na viongozi wengine wote anasema asante sana kwa kuwakaribisha viongozi wa mataifa mbalimbali duniani katika mkutano wa huko Shanghai China. Mkutano huo umezisaidia nchi mbalimbali zinazoendelea zenye tatizo la umaskini.

    Pamoja na hayo pia anapenda kuipongeza serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuipatia misaada mbalimbali serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupeleka wataalamu wa nyanja mbalimbali wakiwemo madaktari pamoja na wakandarasi kuwasaidia watu wa nchi mbalimbali.

    Mwisho kabisa anapenda tumjulishe shirika lililokuwa likitengeneza au kuchapisha magazeti lililokuwa likiitwa Guoji Shudian la China kwa sasa linahusika na nini. ?

    Kuhusu suala hilo, tunaweza kumwambia kuwa, Guoji Shudian yaani Duka la vitabu vya kimataifa la China bado lipo na linaendelea na shughuli zake za uchapishaji wa vitabu.

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-19

.