Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-19 18:38:55    
Sera za kustawisha sehemu ya kaskazini mashariki ya China zahamasisha maendeleo ya viwanda vya serikali vya mkoa wa Liaoning

cri

       

    Wilaya ya Tiexi iliyoko kwenye mji wa Shenyang mkoani Liaoningmu ya kaskazini mashariki ya China ina viwanda vikubwa na wastani karibu 100 vya serikali na ni kituo muhimu cha uzalishaji wa mitambo nchini China. Watu wakitembea kwenye barabara za wilaya hiyo, wataona miti na maua yaliyopandwa kwenye kando mbili za barabara, anga ya buluu na karakana safi za kisasa, lakini hapo zamani palikuwa na mabomba mengi ya moshi. Hayo ni matokeo ya mageuzi yaliyofanywa dhidi ya viwanda vya serikali. Baada ya serikali ya China kuanza kutekeleza sera za kustawisha sehemu ya kaskazini mashariki, viwanda vya serikali vimekuwa na nguvu zaidi.

    Kampuni ya Dawa ya Kaskazini Mashariki ni kampuni kubwa ya serikali iliyoko katika wilaya ya Tiexi. Katika miaka ya karibuni nguvu ya ushindani ya kampuni hiyo imeimarika kwa mfululizo kutokana na mageuzi dhidi ya utaratibu wa kampuni. Hivi sasa Kampuni ya Dawa ya Kaskazini Mashariki imekuwa moja ya kampuni muhimu za uzalishaji wa Vitamini C duniani. Msimamizi mmoja wa kampuni hiyo bibi Feng Yan alisema,

    "Vitamini C ya Kampuni ya Dawa ya Kaskazini Mashariki inachukua 20% ya jumla ya dawa hiyo inayouzwa duniani, lengo letu zaidi ni soko la kimataifa, kufanya uchambuzi, kukadiria mwelekeo wa mahitaji ya soko la kimataifa, kufanya mageuzi ya teknolojia. Hivi sasa, mstari wa mitambo inayozalisha Vitamini C wa kampuni yetu ni wa kwanza kwa ukubwa duniani, ambayo viwango vingi ni vya kisasa duniani. Baada ya kufanya mageuzi ya teknolojia kwa miaka kadhaa, ufanisi wa kampuni umeongezeka kwa kiwango kikubwa".

    Katika mkoa wa Liaoling, kuna viwanda vikubwa vya serikali makumi kadhaa kama Kampuni ya Dawa ya Kaskazini Mashariki. Mwaka jana, serikali ya China ilianza kutekeleza sera za kustawisha kituo cha viwanda cha sehemu ya kaskazini mashariki ya China ikitaka kutatua suala la upungufu wa nguvu ya ushindani ya viwanda vya serikali, na kuleta maendeleo ya uwiano ya uchumi.

    Viwanda vikubwa 100 vya serikali vimehusishwa na sera za kustawisha kituo cha viwanda cha sehemu ya kaskazini mashariki ya China, na viwanda 50 kati ya viwanda hivyo viko katika mkoa wa Liaoning, hii inaonesha msingi na nguvu kubwa ya viwanda vya serikali vilivyoko katika mkoa wa Liaoning.

    Serikali ya mkoa wa Liaoning katika miaka ya karibuni imejitahidi sana kuvifanyia mageuzi viwanda vya serikali, kupunguza mizigo yake, kuviondoa kutoka kwenye hali yenye matatizo na kuviwezesha kupiga hatua kubwa ya maendeleo. Katika wakati huu, serikali kuu ilibuni sera za kustawisha kituo cha viwanda cha sehemu ya kaskazini mashariki, naibu katibu wa chama cha kikomunisti cha mkoa wa Liaoning Bw. Wang Wanbin anaona kuwa sera hizo zitaanzisha mazingira bora kwa viwanda vya serikali mkoani Liaoning. Alisema,

    "Sera hizo zitaharakisha hatua za kurekebisha mfumo wa uchumi na viwanda vya mkoa wa Liaoning, kuhimiza mkoa wa Liaoning kuwa kituo cha uzalishaji wa mitambo na mali ghafi inayotumiwa na viwanda, kuwa na viwanda vya uzalishaji vyenye umuhimu wa kama nguzo kwa uchumi wa taifa na kwa usafirishaji bidhaa nchi za nje."

    Mnamo zaidi ya mwaka mmoja tangu kutekeleza sera za kustawisha sehemu ya kaskazini mashariki ya China, viwanda vya serikali mkoani Liaoning vimekuwa na mabadiliko makubwa ya mazingira ya viwanda na juhudi ya wafanyakazi. Katika siku za baadaye, viwanda hivyo vitaagiza zana za kisasa za kazi, kuimarisha uvumbuzi wa teknolojia mpya na nguvu za ushindani.

    Meneja mkuu wa Kampuni ya Winchi ya Dalian, ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa nchini China, Bw. Qi Yumin anaona kuwa viwanda vinapaswa kupiga hatua, kuharakisha hatua za mageuzi, ufunguaji mlango na mageuzi ya teknolojia. Alisema,

    "Tumeingiza teknolojia ya kisasa duniani ili kuinua kiwango cha teknolojia ya kiwanda chetu, na tumenuia kufikisha kiwango cha teknolojia yetu kuwa cha miaka kumi hivi nyuma ya kiwango cha kisasa kabisa duniani ifikapo mwaka 2010."

    Ili kuharakisha mageuzi ya teknolojia ya viwanda, Kampuni ya Winchi ya Dalian imeajiri wataalamu duniani na kuajiri wahandisi na wasimamizi wa kiwango cha juu kwa mishahara mikubwa. Meneja Qi Yumin anaona kuwa wataalamu ni mali kubwa ya viwanda, wataalamu wa kiwango cha juu wanaweza kuleta mafanikio makubwa kwa viwanda.

    Ni kama meneja Qi Yumin anavyofanya, mameneja wakuu wa viwanda vikubwa vingine vya serikali nao pia wanazingatia sana umuhimu wa wataalamu, wanawapa mazingira bora na mshahara mkubwa, hali ambayo imefanya viwanda vya sehemu ya kaskazini mashariki ya China kuwa sehemu inayovutia zaidi wataalamu.

    Licha ya wataalamu wenye elimu kubwa wanaoshughulikia utafiti wa teknolojia mpya, mafundi pia wanahitajika sana katika maendeleo ya viwanda. Mafundi wengi walioandaliwa zamani katika viwanda vya serikali vya sehemu ya kaskazini mashariki pia ni mali kubwa ya viwanda hivyo, ambao wanafanya kazi muhimu kwa maendeleo ya viwanda. Sera za kustawisha sehemu ya kaskazini mashariki zimefanya wafanyakazi hao kuwa na imani kubwa kwa maendeleo ya viwanda.

    Bw. Zheng Jianqiao ni kiongozi wa karakana moja ya Kampuni ya Nyuzi za kikemikali za Fushun, alisema kuwa hivi sasa anaona kiwanda chao kimekuwa na ufanisi mzuri na nguvu kubwa ya ushindani. Alisema, "Wafanyakazi wa viwanda vya serikali wanaona wametulia zaidi kuliko wafanyakazi wa viwanda visivyo vya serikali, viwanda vya serikali vinavutia watu zaidi, na wafanyakazi wanaona viwanda hivyo ni kama familia zao. Endapo utaratibu wa dhamana ya jamii na utaratibu wa aina nyingine unaenda sambamba na maendeleo ya viwanda, wafanyakazi wa viwanda vya serikali wananufaika zaidi. Ikilinganishwa na viwanda binafsi, viwanda vya serikali vina nguvu kubwa ya ushindani, kwani viwanda hivyo vina wataalamu wengi zaidi.

    Hivi sasa wasimamizi na wafanyakazi wengi wa viwanda vya mkoa wa Liaoning wana maoni yanayofanana na ya Bw. Zheng na kuwa na matarajio makubwa kwa maendeleo ya viwanda vya serikali. Kutokana na kuhamasishwa na sera za serikali ya China, mkakati mmoja unaosaidia maendeleo ya viwanda vya serikali umetekelezwa ili kuanzisha mazingira bora kwa maendeleo ya viwanda vya serikali. Hivi sasa viwanda vya serikali vya Liaoning vimejaa hamasa na ustawi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-19