Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-20 15:27:10    
Mchango mkubwa wa sayansi katika mafanikio kwa China kupata medali za dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya Athens mwaka 2004

cri
    Mashindano ya Olimpiki ya Athens ya mwaka 2004 yalifungwa, Katika mashindano hayo, ujumbe wa michezo wa China ulipata medali 32 za dhahabu, na kuchukua nafasi ya pili kwa wingi wa idadi ya medali za dhahabu. Hayo ni matokeo mazuri kwa China katika mashindano ya Olimpiki tangu mwaka 1984. kutokana na hali hiyo, wachezaji na makocha wote wanaona kuwa, jitihada kubwa na mbinu za kisayansi ni sababu muhimu ya mafanikio.

    Liu xiang

    Katika medali 32 ulizopata ujumbe wa michezo wa China, medali ya dhahabu ya mchezaji Liu Xiang katika mchezo wa kuruka viunzi mita 110 kwa wanaume ni muhimu sana. Matokeo ya Liu Xiang ni dakika 12.91, ni sawasawa na rekodi ya dunia. Jina lake lilijulikana dunia nzima. Tangu mwaka 2002, Taasisi ya sayansi ya michezo ya Idara Kuu ya michezo ya China ilianza kutoa huduma maalumu za kisayansi kwa mazoezi ya Liu Xiang. Bw. Li Ting aliyeshughulikia huduma hiyo alijulisha kwamba, ili kupata habari husika kwa wakati, zaidi ya wanasayansi kumi wa taasisi ya sayansi ya michezo waliambatana na mchezaji Liu Xiang kushiriki mashindano mbalimbali, walirekodi takwimu mbalimbali katika mashindano na mazoezi ya kawaida, halafu walizitafiti takwimu hizo kwa Kompyuta na kutoa matokeo kwa Liu Xiang na kocha wake. Anasema:

    " kwa mfano kupiga picha haraka wakati Liu Xiang aliporuka kwenye viunzi, kurekodi takwimu kwa makini ni muhimu sana kwa kocha na mchezaji kupanga mpango wa mazoezi wa siku za baadaye."

    Bw. Li Ting alidokeza kuwa, "software" ya utafiti wa picha ya wanasayansi ilinunuliwa kutoka nchi za nje kwa bei kubwa. Mbali na software hizo, Idara Kuu ya michezo ya China ilitenga fedha maalumu kwa kundi la utafiti ili kutoa takwimu nyingi zaidi za kisayansi kwa Liu Xiang na wachezaji wengine. Kutokana na msaada mkubwa wa serikali na ushirikiano mkubwa wa watafiti, mchezaji Liu Xiang akapata medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya Athens.

    Kwenye mashindano ya Olimpiki ya Athens, wachezaji wa China Meng Guanliang na Yang Wenjun walipata medali ya dhahabu katika mchezo wa kupiga makasia mita 500 kwa wanaume wawili wawili? hii ni medali ya kwanza ya dhahabu katika michezo ya maji kwa China. Mchezaji Meng Guanliang alipotoa maoni yake baada ya kupata medali ya dhahabu alisema kuwa, mbali na kufanya mazoezi kwa nguvu kubwa, sayansi na teknolojia ni sababu muhimu ya kupata ushindi. Anasema:

    " kwenye mazoezi yetu, wanasayansi walirekodi takwimu zetu za kibaiolojia na kemikali kwa makini sana, hii inaonesha umuhimu wa sayansi na teknolojia katika michezo."

    Meng Guanliang na Yang Wenjun

    Bw. Meng Guanliang alisema kuwa, kila baada ya masomo ya mazoezi, wanasayansi waliwachukua vipimo vya damu ili kufanya upimaji wa takwimu ya kibaiolojia na kemikali kutambua hali ya mwili ya wachezaji.

    Kupiga makasia mita 500 kwa wanaume wawili wawili ni mchezo unaohitajika nguvu kubwa, kwenye mchezo huo, kufanya uhusiano mzuri kati ya mashua, maji na wachezaji ni muhimu sana kwa kupata matokeo mazuri. Ili kuhakikisha mazoezi ya mchezo huo yanafanyika kwa njia ya kisayansi na kujipatia mafanikio, Idara Kuu ya michezo ya China ilituma madaktari watano kufuatana na wachezaji wa mchezo huo kwa miaka mitatu. Madaktari hawa watano walitumia elimu ya sayansi ya nguvu, elimu ya baiolojia, elimu ya saikolojia katika mazoezi ya kawaida na kuandaa mfumo wa upimaji wa GPS. Matokeo yalionyesha kuwa, mafanikio yalipatikana katika mazoezi ya kisayansi. Naibu mkuu wa kundi la mchezo wa kupiga makasia la China Bw. Yuan Shoulong anasema:

    " baada ya kutumika kwa mfumo wa upimaji wa GPS, rekodi ya wachezaji iliongezeka kwa kasi kubwa."

    Li Ting na Sun Tiantian

    Bw. Meng Guanliang na Bw. Yang Wenjun walijulikana kama " farasi weusi" katika mashindano ya Olimpiki ya Athens, lakini "farasi weusi" halisi ni wachezaji wa tennis Li Ting na Sun Tiantian. Michezo ya Tennis ya China ilikuwa nyuma duniani, na matokeo ya wachezaji wa tennis wa China yalikuwa si mazuri sana. Kituo cha michezo ya tennis cha China kiliwaalika maprofesa wa chuo kikuu cha michezo ili kufanya utafiti kuhusu takwimu za wachezaji na kuboresha mazoezi. Bi Li Ting alisema kuwa, kama kusingekuwa na mbinu za kisayansi, yeye na Sun Tiantian wasingeweza kupata medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya Athens. Anasema:

    " naona kuwa, "farasi weusi" ni sifa kubwa kwetu, ushindi wetu wa dakika za mwisho uliwashangaa watu wengi."

    Sasa, ili kujiandaa na mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2008, idara husika za China zimeanza kuchukua hatua mbalimbali. Zinatumia njia za kisayansi kuwaandaa wachezaji. Kwa mfano ili kuinua matokeo ya michezo ya kuogelea, kituo cha michezo ya kuogelea cha China kimetenga fedha zipatazo ya Yuan milioni 20 ili kuanzisha vyombo vya kupiga picha chini ya maji na mfumo wa upimaji.

    Ofisa wa Idara Kuu ya michezo ya China alidokeza kuwa, ili kuiwezesha michezo ya China kupiga hatua mbele, tangu mwaka huu, China imeanza kuongeza fedha kugharamia mambo ya kisayansi katika michezo ili kuhakikisha China kupata matokeo mazuri zaidi katika mashindano ya Olimpiki ya Beijing mwaka 2008.

Idhaa ya kiswahili 2004-10-20