Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-22 17:47:36    
Ukataji wa karatasi

cri

   "Maua ya plum ni kiboko ya maua: yanachanua hata siku za baridi kali. Kunguru(magpie) wawili wanaimba kwenye tawi; wanatutakia furaha ya mwaka mpya." Hivyo ni vituko vilivyotokea katika tamasha ya utamaduni na sanaa iliyoonyeshwa moja kwa moja na Kituo cha TV cha Jimbo la Henan na Xie Zhong, msanii wa ukataji wa karatasi, wakati wa Sikukuu ya Yuanxiao ya mwaka 1994. Xie aliwatakia watazamaji "furaha ya kila familia" kwa kutumia kazi yake aliyoipenda ya "Kunguru na Maua ya Plum".

    Xie Zhong mwenye umri wa zaidi ya miaka 30 ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Mgodi wa Xinfeng wa Mji wa Yuzhou jimboni Henan. Alianza kushughulika na sanaa ya kukata karatasi baada ya saa za kazi tangu mwaka 1971; hadi leo amekwishatengeneza vitu zaidi ya 200 vya aina mbalimbali. Ufundi wake maalumu waukataji karatasi unaonekana kaika miundo yake barabara ya upangaji; mistari huwa ni rahisi na ya usawa. Kila mara sikukuu zinapofika au harusi zinapofungwa majirani zake wa karibu na wa mbali huja kwake kumwomba vitu vya sanaa ya kukata karatasi iwe ishara ya bahati njema. Wakati fulani wafanyakazi wa Kituo cha TV cha Henan walihojiana naye na wakaja kuonyesha kazi zake katika TV mara nyingi. Watazamaji wanaoishi mbali sehemu za Luoyang, Anyang, Zhoukou na Xinyang wakaanza kumwandikia barua kuomba kazi zake za sanaa za karatasi.

    Walimu wa mwanzo wa Xie Zhong walikuwa ni mama na nyanya yake. Sawa na wanawake wengine wengi wa Zhongyuan(sehemu za kati na mwisho za Mto Manjano) mama na nyanya ya Xie Zhong ni hodari wa kufanya kazi za mikono kama vile kutengeneza maua ya karatasi, kutarizi au kukata maua ya kupamba kwenye viatu. Xie Zhong alianza kupenda sanaa ya kukata karatasi tangu alipokuwa mtoto. Wakati alipokuwa na umri wa miaka 17 alijiunga na jeshi na alilitumikia katika sehemu fulani ya Kaskazini-Mashariki mwa China. Wakati wa Mapinduzi Makubwa ya Utamaduni, kutokana na kupenda kwake haki na huruma aliyokuwa nayo, aliwahi kumsaidia profesa mmoja mzee aliyekuweko katika hali ngumu ya maisha na ugonjwa. Kabla ya hapo, Profesa huyo alikuwa akifundisha somo la sanaa. Baada ya kupona, profesa huyo alimfundisha Xie Zhong ujuzi kuhusu ubunifu wa sanaa jadiia. Ujuzi huo ulimsaidia sana Xie Zhong katika siku zilizofuata.

    Miaka kadhaa baadaye Xie Zhong akaana kutengeneza vitu vya sanaa kwa kukatakata karatasi kila alipopata wasaa. Mkewe alimwelewa sana na akawa anamsaidia katika maisha. Kutokana na uzalendo wake kwa mahali alipozaliwa na upendo wake kwa mambo ya jadi, sasa hivi kuna vitu vingi vya sanaa alivyotengeneza Xie Zhong kwa kukata karatasi ambavyo vimejaa uhai wa sanaa jadiia na kutoa harufu nzito ya vitu vya kienyeji.

 

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-22