Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-26 20:47:29    
Mafanikio yaliyopatikana katika kazi ya kupunguza idadi ya watu maskini nchini China yaivutia dunia

cri

 

    Tarehe 17 Oktoba ilikuwa siku ya kimataifa ya kupunguza umaskini duniani. China ilitangaza kwa fahari kuwa, idadi ya watu maskini vijijini ilipungua na kufikia milioni 29 mwishoni mwa mwaka 2003 kutoka milioni 250 ya mwaka 1978, ambapo idadi ya watu maskini imepungua na kuwa asilimia 3 hivi ya idadi ya jumla ya watu wa vijiji kutoka ile ya asilimia 30.7.

    Kupunguza idadi ya watu maskini ni matumaini ya watu wengi tangu enzi na dahari. Chini ya uongozi wa chama cha kikomunisti cha China, lengo hilo linafanikiwa nchini China. Hayo ni mafanikio makubwa duniani, ambayo yamesifiwa sana na watu wengi.

    Zifuatazo ni tarakimu zinazoonesha mafanikio hayo:

    Idadi ya watu maskini vijijini ambao bado hawajatatua tatizo la lishe ilipungua na kuwa milioni 29 mwishoni mwa mwaka 2003 kutoka milioni 250 ya mwaka 1978; wastani wa pato halisi la kila mkulima wa wilaya muhimu 592 uliongezeka kwa asilimia 5.8 mwaka jana. Hili ni ongezeko la asilimia 1.5 kuliko lile la kila mkulima wa nchi nzima, na hii ni mara ya kwanza kwa pato la wakulima wa sehemu maskini kuongezeka zaidi kuliko wastani wa kiwango cha nchi nzima.

   Toka mwaka 1986 hadi 2003, hekta 179 za mashamba ziliandaliwa kimsingi, na tatizo la maji ya kunywa kwa watu milioni 74.59 lilitatuliwa.

    Hali ya uendeshaji wa shule imeboreshwa dhahiri katika sehemu zenye matatizo ya kiuchumi, idadi ya watoto wasioweza kupata nafasi ya kwenda shule imepungua na kufikia asilimia 7.8. Na asilimia 70.2 ya vijiji vimejenga zahanati, hali ya ukosefu wa madaktari na dawa vijijini imepungua kwa dhahiri. Na teknolojia nyingi zinazofaa katika uzalishaji wa mazao ya kilimo zimeenea vijijini, ambapo kiwango cha wakulima kufanya kazi kwa njia za kisayansi kimeinuka kwa dhahiri.

    Mkuu wa Benki ya dunia Bwana James Wolfensohn anaona kuwa, kama upunguzaji wa idadi ya watu maskini ni kigezo, basi China hakika ni nchi iliyotoa mchango mkubwa kabisa kwa ajili ya kazi ya kupunguza umaskini kote duniani.

    Serikali ya China inawaongoza wananchi wote kufanya kazi ya kuondoa umaskini, imepata njia inayolingana na hali halisi ya nchi ya China yaani: serikali inafanya kazi ya uongozi, watu katika jamii wanashiriki katika kazi katika hali ya kujitegemea, kuwasaidia watu maskini kuendeleza uzalishaji wa mazao, na kujipatia maendeleo kwenye nyanja mbalimbali.

    Katika dunia nzima, shughuli za kuwasaidia watu maskini za nchi nyingi huanzishwa na mashirika ya wafadhili, lakini shughuli hizo nchini China zinaongozwa na kuelekezwa na serikali katika ngazi mbalimbali.

    Katika miaka ya hivi karibuni, jumuiya zisizo za kiserikali pia zimefanya kazi kubwa katika kuondoa umaskini nchini China, ambapo zinasaidia kujenga shule za msingi kuwasaidia watoto wa familia zenye matatizo ya kiuchumi kupata nafasi za kwenda shule, kuwasaidia walemavu kujiendeleza, kuwasaidia kina mama wenye matatizo ya kiuchumi katika uzalishaji mazao, kuwasaidia watoto wa kike waliokosa nafasi za kwenda shule kupata elimu ya lazima, na vijana wa kujitolea kuwasaidia watu maskini kujiendeleza na kadhalika.

    Mkurugenzi wa Shirika la mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa Bwana Brang alina kuwa, harakati za China kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiuchumi kuondokana na umaskini zinastahiki kuigwa na nchi mbalimbali duniani. Maarifa yenye thamani kubwa ya China kuhusu maendeleo ni kubuni na kushikilia sera mwafaka ya kuwasaidia watu maskini.

    Serikali ya China na wananchi wake wamechukua hatua mbalimbali zinazofaa hali halisi ya nchini katika kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiuchumi kuondokana na umaskini kama vile kufanya semina mbalimbali za kutoa mafunzo ya kazi, kueneza teknolojia ya kisasa ya kilimo na kuwasaidia wakulima maskini kuendeleza shughuli za kilimo zenye umaalum wa kienyeji; kuwasaidia wakulima kwenda nje ya maskani yao kufanya kazi; sehemu ya mashariki na magharibi kufanya ushirikiano katika kuondoa hali ya umaskini; na kuhamisha wakulima walioishi kwenye sehemu zenye hali duni ya kijiografia.

    Kupunguza na kuondoa umaskini ili kupata maendeleo kwa pamoja, ni lengo na nia imara ya serikali ya China.

 

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-26