Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-29 21:52:37    
Shughuli za udhibiti wa tumbaku nchini China

cri
Mwezi Mei mwaka 2003, Mkutano wa 56 wa afya wa kimataifa ulipitisha kwa kauli moja "azimio la udhibiti wa tumbaku", hili ni azimio la kwanza lenye uwezo wa kisheria kuhusu mambo ya afya ya binadamu duniani, azimio hilo linatazamiwa kutekelezwa kuanzia mwaka huu. Utengenezaji na ununuaji wa tumbaku ni mkubwa sana nchini China. Lakini China ilichukua hatua gain kuhusu udhibiti wa tumbaku? Leo tunawaletea maelezo kuhusu jambo hilo.

Uvutaji wa sigara ni kitendo kinachoharibu afya, kinasababisha ugonjwa wa saratani ya mapafu, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine makubwa. Sasa idadi ya watu waliovuta sigara duniani imefikia bilioni 1.1, na kila mwaka watu wanaokufa kutokana na kuvuta sigara wanafikia milioni 3.5.

Utengenezaji na ununuaji wa tumbaku nchini China unachukua zaidi ya 33% duniani, na wavutasigara wa China wenye umri wa miaka zaidi ya 15 wanafikia milioni 350, na kila mwaka watu milioni 1 wanakufa kutokana na uvutaji wa sigara. Mwaka 2000, gharama za matibabu kutokana na tumbaku ilifikia Yuan bilioni 49 nchini China.

Profesa wa Chuo Kikuu cha matibabu cha Xiehe cha China Bw. Yang Gonghuan ni mtaalam wa udhibiti wa tumbaku. Alisema kuwa, kama hazitachukuliwa hatua za kudhibiti tumbaku haraka, katika miaka 30 ijayo, wavuta sigara wa China watafikia milioni 430, na hali hiyo italeta matatizo mengi makubwa. Anasema:

" Kama China ikianza kuchukua hatua za kudhibiti tumbaku, magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na uvutaji wa sigara yatapungua na idadi ya vifo itapungua sana; wakati huo huo, gharama za matibabu pia itapungua sana, na idadi ya watu masikini kutokana na matibabu itakwenda chini, hivyo, udhibiti wa tumbaku una umuhimu mkubwa kwa uchumi na afya."

China siku zote inatia maanai kazi ya udhibiti wa tumbaku. Ilitunga sheria zaidi ya 20 kuhusu udhibiti wa tumbaku. Kwa mfano, vituo vya televisheni vilipigwa marufuku kutoa matangazo kuhusu sigara, na watu wanapigwa marufuku kuvuta sigara katika sehemu za umma.

Mbali na hayo, China ilianzisha shughuli nyingi kuhusu udhibiti wa tumbaku. Kwa mfano, ilianzisha miji isiyokuwa na matangazo ya tumbaku, hospitali na shule zinazopiga marufuku ya kuvuta sigara n.k; tarehe 31 mwezi Mei ni siku ya kutovuta tumbaku duniani, katika siku hiyo, shughuli mbalimbali za kupiga marufuku tumbaku zilifanyika nchini China, idara mbalimbali za serikali na jamii zilieneza elimu ya madhara ya tumbaku katika sehemu nyingi nchini China.

Katika miaka ya hivi karibuni, wavutasigara vijana na wanawake wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku, serikali ya China ilitilia maanani sana hali hiyo, hivyo shughuli za kutoa elimu kuhusu madhara ya sigara zilianza kufanyika dhidi ya watu hawa. Sasa shughuli hizo zinafanyika Beijing, Shanghai, Ningxia, Shandong, Guangdong na sehemu nyingine nchini China.

Mbali na hayo, shule za sekondari na shule za msingi za China zinafanya kampeni za "Kutovuta sigara na kuwa watu wasiovuta sigara". Wanafunzi wanatoa ahadi ya kutovuta sigara. Hadi sasa, kuna wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanashiriki katika kampeni hiyo. Mwanafunzi wa kike wa Beijing Wangxin alimwambia mwandishi wa habari kuwa:

" zamani niliona kuwa, kuvuta sigara ni kitendo kizuri. Lakini sana naelewa kuwa, kuvuta sigara ni jambo la hatari, linadhuru vibaya afya, sisi vijana hatupaswi kuvuta sigara."

Ingawa China ilifanya jitihada kubwa katika udhibiti wa sigara, lakini kazi hiyo bado ni ngumu. Sababu muhimu ni kwamba, kuvuta sigara imekuwa tabia ya watu wengi, na wavutasigara hawajui madhara ya sigara kwa afya zao. Mbali na hayo, utengenezaji wa tumbaku unaleta faida kubwa ya kiuchumi, kwa mfano, mapato ya tumbaku ya mkoa wa Yunan yalichukua 70% katika mapato yote ya mkoa huo.

Ili kuimarisha zaidi kazi ya udhibiti wa tumbaku, mwaka uliopita China ilisaini mkataba wa udhibiti wa tumbaku, ofisi wa Kamati ya afya na kuvutasigara ya Beijing Bw. Cao Ronggui alisema kuwa, mkataba huo ulitoa fursa mpya kwa China kufanya kazi ya udhibiti wa tumbaku. Anasema:

"Wizara ya afya ya China imetoa taarifa na kufanya mikutano mbalimbali ili kuwawezesha maofisa wa idara husika za udhibiti wa tumbaku kutambua umuhimu wa mkataba huo, kuimarisha zaidi udhibiti wa tumbaku na kuwekea msingi mzuri kwa China kutekeleza mkataba huo."

Kuhusu jitihada zilizotolewa na China katika udhibiti wa tumbaku, mwakilishi wa Shirika la afya ya duniani Bw. Hank Bakedam anasema:

" vipengele kadhaa vilivyowekwa kwenye Mkataba wa udhibiti wa tumbaku zilitekelezwa nchini China, bila shaka vipengele vingine zitatekelezwa. Shirika la afya ya duniani iliisifu sana China kuhusu kazi yake. Tunaona kuwa, China itajitahidi kutekeleza vipengele vyote za mkataba huo."

Idhaa ya kiswahili 2004-10-29