Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-10-29 22:19:32    
Dawa za mitishamba za China katika kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi barani Afrika.

cri

     Wakati kampuni za dawa za nchi za magharibi zinapofikiria kupunguza bei za dawa ya Ukimwi au la barani Afrika, Madaktari wa China wametoa misaada bure katika kupambana na Ukimwi barani Afrika kwa miaka 17.

    Katika hospitali kubwa ya Muhimbili nchini Tanzania, mtaalamu wa Ukimwi Bw. Huang Shijing anatoa matibabukwa msichana anayeitwa Zena mwenye umri wa miaka 12 tu. Msichana huyo aliambulizwa virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama yake. Hivi sasa, ugonjwa huo unaingia katika kipindi cha mwisho. Sasa (tetter)inaenea kwenye mikono yake, na umbo la kucha zake limebadilika vibaya sana.

    Daktari Huang Shijing alituambia, "CD 4 yake ni 26 tu, idadi hiyo ni ya chini sana. Kwa wastani, wagonjwa wa Ukimwi wenye CD 4 chini ya 50, ni vigumu kuishi zaidi ya nusu mwaka."

    CD 4 ni aina moja ya chembechembe za binadamu, kazi yake ni kumlinda binadamu kutoshambuliwa na virusi mbalimbali, lakini pia ni adui mkubwa wa virusi vya Ukimwi. Pia virusi vya Ukimwi vinaishi na kuzaliana kwenye chembechembe za CD 4. Kadri virusi vya Ukimwi vinavyoongezeka mwilini ndivyo chembechembe za CD 4 zinavyozidi kupungua. Mtu mwenye afya njema kiasi cha chembechembe 600 hadi 1200 za CD 4 kwa kila mililita, lakini idadi hiyo hupunguka hadi chini ya 200 kwa kila mililita kwenye damu ya wagonjwa wa Ukimwi. Kama idadi hiyo itakapopunguka hadi 20 kwa mililita, mgonjwa wa Ukimwi hawezi kupambana na virusi vyovyote. Hii inamaanisha wanakabiliwa na kifo.

    Mwaka mmoja uliopita, msichana Zena mwenye CD 4 26 tu alianza kutibiwa katika idara ya mitishamba kwenye hospitali ya Muhimbili. Lakini idadi hiyo inadumishwa mpaka sasa. Hali hii inatia moyo sana kwa daktari Huang na madaktari wengine wa China.

    Daktari Huang alisema kwa imani kubwa: "Ataweza kuishi kwa miaka mingi kama ataendelea kutibiwa. Kiasi cha CD 4 kwabaadhi ya wagonjwa wetu kimeongezeka hadi 400 kutoka 20 baada ya kutibiwa kwa mwaka mmoja na kurejea katika idadi ya kawadia."

    Imani kubwa ya Daktari Huang ni kutokana na uzoefu mkubwa wa kikundi cha wataalamu wa mitishamba ya China baada ya jitihada za miaka 17. Mwaka 1987, aliyekuwa rais wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi alikuja China kutokana na tatizo la wagonjwa wa Ukimwi wanaoongezeka nchini Tanzania. Alikuwa na matumaini ya kupata njia ya kutatua tatizo hilo kwa tiba ya kijadi ya China. Wakati huo, serikali ya China ilipeleka wataalamu wa mitishamba ya China nchini Tanzania. Kuanzia hapo, China na Tanzania zilianzisha ushirikiano katika kutibu Ukimwi kwa mitishamba ya China. Mpaka sasa, ushirikiano huo umekuwepo kwa kipindi cha 6.

    Jitihada za miaka 17 zimeleta mafanikio mbalimbali katika historia ya tiba. Mwaka 1991, makala kuhusu wagonjwa 158 wa Ukimwi wa Dar es Salaam kutibiwa kwa mitishamba ya China ilitangazwa hapa Beijing. Makala hiyo ilielezea mafanikio ya wataalamu wa China katika kuwasaidia wagonjwa 6 wawe na hali ya kawaida. Jambo hilo linastaajabisha sana katika enelo la tiba ulimwenguni. Mpaka sasa, idadi ya CD 4 za wagonjwa zaidi ya 30 wanaoendelea na matibabu inakaribu kufikia idadi ya kawaida.Hali hiyo inawaletea matarajio makubwa.

    Msichana mwingine Fafuma anaishi kwa matumaini makubwa kutokana na tiba ya kichina. Alithibitishwa kuwa mgonjwa wa Ukimwi mwaka 1995, na kuanza kutibiwa wataalamu wa China.

    Fafuma alisema akiwa na tabasamu kuwa, "Mitishamba ya China inanisaidia sana. Sasa siuogopi ugonjwa huo hata kidogo, badala yake naishi kama nilivyokuwapo zamani, hata ninajiona nina afya njema."

    Fafuma alisema kuwa, alikuwa anajitahidi kushiriki kwenye mkutano wa kimataifa wa kinga na tiba ya Ukimwi. Atatoa hotuba kwenye mkutano huo na kuwasilishana uzoefu wao wa tiba na wagonjwa wengine wa Ukimwi.

    Fafuma na Zena ni wawili tu miongoni mwa wagonjwa milioni 30 wa Ukimwi na watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi barani Afrika. Lakini wanabahatika kutibiwa na kupata matibabu ya mitishamba ya kichina bure. Hii inawapatia matumaini makubwa.

    Wataalamu wa China wamewatibu maelfu ya wagonjwa wa Ukimwi nchini Tanzania kwa miaka 17 iliyopita. Idadi hiyo bado ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wa Ukimwi barani Afrika. Lakini wanafanya juhudi bila ya kusita, ambapo mafanikio watakayopata yataleta mabadiliko makubwa kwa maisha ya wagonjwa hao wa ukimwi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-10-29