Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-01 16:43:43    
Mji wa Weihai mkoani Shangdong, China

cri

  

    Weihai ni mji ulioko pwani ya mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. Mji huo uko kwenye ncha ya mashariki kabisa ya peninsula moja. Mji wa Weihai unazungukwa na bahari kubwa kwa pande zake tatu, mwambao wake una urefu wa kilomita karibu 1000. Mji huo wa pwani una hewa safi na mazingira mazuri, zaidi ya asilimia ya sehemu ya mjini imepandwa miti na majani. Wakati wa majira ya joto hakuna joto kali, na siku za baridi ya huko pia sio kali sana. Kila mwaka mji huo unawavutia watalii wengi. Mwaka 2003, mji huo ulipewa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya sehemu mwafaka kwa makazi.

    Mjini Weihai majengo mengi si makubwa, lakini yamejengwa vizuri na yamejisitiri vizuri ndani ya miti. Mji huo unaegemea bahari, ukitembea mtaani unaweza kuona bahari mbele yako. Ingawa mji uko karibu sana na bahari, lakini pwani ya bahari ni safi sana, maji ya bahari pia ni masafi hata unaweza kuona hali ya ndani yake. Kandokando ya bahari kuna bustani yenye umbo refu, na miti ya aina mbalimbali imepandwa huko. Watalii wakifika huko huvutiwa sana na sura inayopendeza ya mji huo. Wakazi walioishi kwa miaka mingi mjini humo, wakitaja maskani yao hutumia maneno mengi ya kusifu mji huo. Mkazi wa Weihai msichana Yingna alisema:

    Mji wa Weihai una anga buluu zaidi, watu wengi wakifika mji huo, picha ya kwanza wanayopata kuhusu mji huo huwa ni kwamba, anga ya Weihai ni ya buluu zaidi kuliko miji mingine. Naona hii ni sifa nzuri zaidi kwa Weihai. Na Wakazi wa Weihai wanaona majivuno zaidi kuhusu bahari ya Weihai. Mji huo umepambwa kwa miti mingi, naona fahari kubwa kuishi kwenye mji huo.

    Ukienda nje ya mji, utaona mandhari ya kupendeza zaidi. Kwenye sehemu ya bahari ya Weihai, vimetapakaa visiwa vikubwa na vidogo karibu mia moja na ghuba yenye mvuto zaidi ya 30, ambapo milima ya kijani, bahari ya buluu na anga ya buluu vinaonekana na kuwa kivutio kikubwa kwa watalii. Kisiwa cha Liugong kilichoko karibu zaidi na mji wa Weihai ni sehemu yenye vivutio vya utalii vya ngazi ya kitaifa, husifiwa na watu kuwa ni "bahari ya peponi". Asilimia 85 ya eneo la kisiwa hicho imefunikwa na misitu, ndani ya misitu kuna wanyama na mimea mingi yenye thamani ya aina mbalimbali. Hata hali ya utamaduni ya kisiwa cha Liugong ni tofauti na sehemu nyingine. Kuna kumbukumbu ya utamaduni wa kale ya miaka elfu moja iliyopita, pia kuna mabaki ya shule ya jeshi la kwanza la majini la China, jukwaa la kale la mizinga na gati la chuma.

    Sehemu ya Shengshuiguan iliyoko umbali wa kilomita 40 kutoka kwenye kisiwa cha Liugong ni sehemu yenye vivutio vya miti minene, na jinsi inavyoonekana ni kama bahari ya miti. Ukipanda gari la kwenye waya linalopita kwenye anga ya sehemu hiyo, utaona mawimbi ya miti na kusikia milio ya miti, hayo yote yanaweza kugusa hisia zako na kujisikia kama uko nje ya dunia. Ndani ya misitu ya huko, kuna miti mingi iliyokuwepo kwa miaka mingi. Miongoni mwa miti hiyo, mti mmoja wa ginkgo umekuwepo kwa miaka zaidi ya elfu moja. Mwongozaji wa utalii alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, mti huo ni wa ajabu sana, kwani miti miwili ya kiume na kike ilikua kwa pamoja, hivyo mti huo unaitwa kuwa mti wa mke na mume. Matunda ya miti hiyo yote ni ya mapacha, yaani peke mbili ziko kwenye ganda moja, hii ni nadra kuonekana katika sehemu nyingine duniani, mti huo ni kama hazina kubwa ya sehemu hiyo.

Idhaa ya kiswahili 2004-11-01