Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-02 19:35:28    
Barua za wasikilizaji 1102

cri
    Msikilizaji wetu Gulam Haji Karim wa sanduku la posta 97 Zanzibar Tanzania ametuletea barua akisema kuwa, anatoa pongezi kwa maadhimisho ya miaka 55 ya China mpya. Anasema katika muda huo wa miaka 55 Jamhuri ya watu wa China imekwenda mbio sana. Katika kujenga China mpya ya kisasa kwa kutumia sayansi na teknolojia, China mpya inashindana na nchi zilizoendelea katika miaka mia moja. Ikiwa mtu aliyetembelea China miongo miwili iliyopita akirudi leo China, ataiona China mpya. Kwa mfano akiwa katika miji mikubwa miwili Beijing na Shanghai, atajiona kama yuko Ulaya magharibi, kama vile Paris au New York.

    Anasema Jamhuri ya watu wa China katika muda mfupi uliopita imejijenga ndani na nje. Leo Jamhuri ya watu wa China ina uhusiano wa kibalozi na zaidi ya nchi 160 duniani, na pia China inatoa misaada bila masharti ya kisiasa kwa nchi nyingine za Asia na Afrika. Pia China imekuwa na uhusiano maalum na nchi za Afrika, kama kipindi kimoja cha Radio China kimataifa kwa lugha ya kiswahili, kipindi hicho kinajulikana kama Daraja la urafiki kati ya China na Afrika. Mwisho anasema anaitakia China maendeleo zaidi katika miaka ijayo iwe ya amani, raha na furaha.

    Msikilizaji wetu mwingine maarufu Mbarouk Msabah ametuletea barua kutoka sanduku la posta 20301, Manama Bahrain akisema kuwa, kuanzia tarehe 18 hadi tarehe 25 Oktoba mwaka huu amekuwa huko mjini Manama katika kisiwa cha Ghuba ya Uajemi cha Bahrain kikazi. Anasema anaishukuru sana Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa kutokana na kuambatanisha matangazo yake pamoja na makala mbalimbali kwenye tovuti ya idhaa ya kiswahili, kwani imekuwa rahisi sana kwake kutembelea tovuti yetu hiyo na kufaidika na matangazo yetu kila siku huko mjini Manama.

    Anasema anapenda kutuahidi kuwa ataendelea kusikiliza matangazo yetu popote pale alipo na kutuma maoni yake kuhusu vipindi vyetu mbalimbali pamoja na makala ambazo zitakuwepo kwenye tovuti yetu yenye kuvutia.

    Tunamshukuru sana Bwana Mbarouk Msabah kwa moyo wake na umakini wa kufuatilia sana vipindi vyetu. Tumetiwa moyo na maoni yako nasi tunaahidi kuendelea kuchapa kazi zaidi ili kufurahisha zaidi wasikilizaji wetu.

    Pia anaishukuru Radio China kimataifa kwa kuwa dirisha lililowazi kuonesha hasa jinsi China ilivyo, na jinsi wachina wanavyozikumbuka nchi nyingine zinazoendelea kama za Afrika, ikiwemo Tanzania. Mwisho kabisa Bwana Ngogo ameandika shairi lisemalo: Sera za China zidumu:-

    Ras Manko nina hamu, pokea zangu salamu

    China nimeifahamu, maisha yake matatu

    Imefika yangu zamu, nifanyiwapo karamu

    Wachina kwa majukumu, sera zao zinadumu

    Ni marafiki wa damu, tunao kila awamu

    Watufunza kujikimu, kwa kazi ni muhimu

    Wao ni wataalamu, malengo yetu yatimu

    Wachina kwa majukumu, sera zao zinadumu

    Beti nne sio adimu, mwisho umenilazimu

    Nitawapaka marhamu, na kwa akili timamu

    China kwa ukarimu, uzidi shika hatamu

    Wachina kwa majukumu, sera zao zinadumu.