Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-09 16:29:41    
Qinghai yapata mafanikio katika kukuza uchumi kwa kutumia hali yake bora ya rasilimali

cri

    Kampuni ya Guoluo inayoshughulikia utafiti na usindikaji wa mazao ya mifugo iliyoko mkoani Qinghai, sehemu ya kaskazini magharibi ya China, ilianzishwa mwaka huu. Hivi sasa, kampuni hiyo iliyoanzishwa miezi kadhaa iliyopita, imefanikiwa kuuza bidhaa zake za maziwa ya unga na nyama kavu ya ng'ombe wa kitibet katika sehemu za kati na magharibi za China, pamoja na sehemu nyingine zilizoendelea ikiwemo miji ya Beijing na Shanghai. Alipozungumzia sababu ya kampuni hiyo kupata maendeleo ya kasi, mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bw. Han Gaori alimwambia mwandishi wetu wa habari kwa furaha,

    "Sababu moja muhimu ni kutegemea hali bora ya rasilimali maalum za mifugo zisizo na uchafuzi wowote, na kutoweka aina yoyote ya dawa wakati tunapozisindika. Hii ni moja ya umaalum wa bidhaa zetu."

    Bw. Han alisema kuwa Guoluo iko kwenye sehemu ambayo iko kwenye mita zaidi ya 4,200 kutoka usawa wa bahari katika sehemu ya kusini ya mkoa wa Qinghai. Katika sehemu hiyo hakuna watu wengi wala viwanda vikubwa. Ubora huo pekee wa mazingira ya kimaumbile unafanya mazao ya mifugo yawe safi, na yasiwe na vitu vya uchafuzi na kupendwa na watu wengi. Bw. Han anatarajia kufanya ushirikiano na sehemu iliyoendelea ya sehemu ya mashariki ya China pamoja na kampuni zenye mitaji na mfumo bora wa biashara, na amenuia kuongeza pato la kampuni yao hadi kufikia Yuan za Renminbi milioni 100 kutoka Yuan zaidi ya milioni 20 za hivi sasa.

    Habari zinasema kuwa mbinu hiyo imeanza kutumiwa na kampuni nyingi za mkoa wa Qinghai. Msaidizi mkuu wa mkoa wa Qinghai Bw. Ma Jiantang alimwambia mwandishi wetu wa habari,

    "Hali bora ya wanyama na mimea ya uwanda wa juu ni moja ya hali bora ya mkoa wa Qinghai. Katika miaka ya karibuni, sekta ya kilimo na mifugo ya uwanda wa juu isiyo na vitu vya uchafuzi imeendelezwa kwa haraka. Hivi sasa uzalishaji wa bidhaa za aina hiyo umeendelezwa katika viwanda vya kisasa."

    Mkoa wa Qinghai ni mkoa mkubwa nchini China, mkoa huo una eneo la kilomita za mraba zaidi ya laki 7 na elfu 20, na kilomita za mraba laki 3 na elfu 30 ni mbuga yenye majani yanayoweza kuwa malisho ya mifugo. Mkoa wa Qinghai una rasilimali nyingi za kimaumbile zikiwa ni pamoja na ng'ombe maalumu wa Tibet wajulikanao kwa jina la yak, mbuzi, na dawa ya miti-shamba ijulikanayo kwa jina la rhubarb na aweto.

    Rasilimali nyingi za wanyama na mimea ya mkoa wa Qinghai, si kama tu zimezivutia kampuni nyingi kuwekeza huko, pamoja na kutekeleza sera za kustawisha sehemu ya magharibi, hivi sasa wafanyabiashara wengi kutoka nchi za nje pia wanavutiwa na rasilimali za huko. Bw. Mario Angelucci kutoka Ujerumani hivi sasa anajiandaa kwenda huko kujenga kiwanda cha mbao kwa kuvutiwa na rasilimali za miti za mkoa wa Qinghai. Alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema,

    "Nimefika hapa Qinghai hivi karibuni, sijatembelea sehemu nyingi, hivyo ni vigumu kutathimini mazingira ya uwekezaji yalivyo. Lakini mambo niliyoyaona katika kipindi hicho yamenifanya nivutiwe sana na sehemu hiyo."

    Mbali na rasilimali za wanyama na mimea, rasilimali nyingi za madini za mkoa wa Qinghai pia zimewavutia wawekezaji wengi. Habari zinasema kuwa zaidi ya aina 60 za madini zimegunduliwa katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na asbestos, kainite, crystal, lead, zinc, mafuta ya asili ya petroli na chuma.

    Kampuni ya chuma cha pua maalumu ya Xining ni kampuni moja kubwa ya serikali, hivi sasa kampuni hiyo imekuwa na uwezo wa kuzalisha tani zaidi ya milioni moja za vifaa vya chuma cha pua. Mhasibu mkuu wa kampuni hiyo Bw. Wang Dajun alisema kuwa mkoa wa Qinghai una mali asili nyingi ya madini, inayoiwezesha kampuni ya chuma cha pua cha Xining kujiendeleza kwa kutumia rasilimali hizo. Aliongeza kusema kuwa bidhaa za kampuni yao zinauzwa vizuri sana, hivi sasa mfumo wa mauzo wa kampuni hiyo umefikia karibu kila sehemu nchini na kuwa na pato la Yuan za Renminbi zaidi la bilioni 1.7 kwa mwaka. Maendeleo ya kampuni ya chuma cha pua cha Xining yamehimiza maendeleo ya viwanda vingine vinavyohusika vya huko, na inafanya kazi muhimu katika kuhimiza maendeleo ya uchumi ya mkoa huo mzima.

    Miaka 10 iliyopita Bw. Chen Yongqi kutoka Hong Kong alikwenda Qinghai kuwekeza kwa kujenga kiwanda cha aluminium. Alisema kuwa wakati ule kusafiri kwenda huko kutoka Hong Kong ilimchukua siku mbili. Ingawa wakati ule, ujenzi wa miundo mbinu wa huko haukuwa wa kuvutia, lakini aliamua kwenda huko kuwekeza. Alisema, "Mkoa wa Qinghai una mali asili nyingi ya madini, tena tunaweza kuzalisha malighafi za aluminum kwa kutumia rasilimali za huko pamoja na nguvu kazi kwa gharama ndogo."

    Katika miaka ya karibuni, kutokana na kuhamasishwa na sera za kustawisha sehemu ya magharibi ya China, ujenzi wa miundo-mbinu ya mkoa wa Qinghai zikiwemo barabara, njia za reli, usafiri wa ndege na mawasiliano zimepata maendeleo makubwa. Hivi sasa inamchukua Bw Chen saa chache tu kusafiri kutoka Hong Kong hadi Qinghai. Kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji mkoani Qinghai kunazidisha imani yake kuwekeza katika mkoa huo. Hivi karibuni, Bw. Chen aliwekeza tena Yuan zaidi ya bilioni 1.1 kwa kujenga kituo cha kuzalisha umeme kwa nguvu za maji.

    Hata hivyo, mkoa wa Qinghai hautumii rasilimali zake bila kikomo, pamoja na serikali kuu ya China kutoa wazo la kuzingatia maendeleo endelevu. Mkoa wa Qinghai unazingatia sana kuwa na maendeleo endelevu ya uchumi, unatoa kipaumbele kwa hifadhi ya rasilimali, kutumia rasilimali bila ubadhilifu na kuhifadhi mazingira ya asili.

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-09