Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-10 18:11:19    
Taasisi ya Sayansi ya China kuongeza nguvu ya ushindani kwa kufanyiwa mabadiliko

cri
Tarehe 1 mwezi November mwaka huu ilikuwa ni siku ya kuadhimisha miaka 55 ya kuzaliwa kwa Taasisi ya sayansi ya China. Tangu taasisi hiyo ilipoanzishwa, siku zote imekuwa ni Taasisi kubwa kabisa ya kufanya utafiti wa sayansi ya maumbile nchini China. Matokeo mengi ya utafiti wa sayansi ya kimsingi ya hali ya juu yalitokana na taasisi hiyo.

Lakini katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, kutokana na ukosefu wa fedha za utafiti, hali duni ya zana na kushindwa kujiendesha vizuri, wataalamu wengi waliondoka kutoka kwenye Taasisi ya sayansi ya China, na kufanya kiwango cha matokeo ya utafiti wa sayansi kuwa nyuma duniani siku hadi siku.

Ili kubadilisha hali hiyo na kukidhi mahitaji makubwa ya maendeleo ya uchumi wa China, tangu mwaka 1998, chini ya misaada ya serikali ya China, mradi mkubwa ulioitwa " Uvumbuzi wa Ujuzi" ulianza kutekelezwa. Katibu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi ya China Bw. Li Zhigang alijulisha,

" madhumuni ya mradi huo ni kulinganisha matokeo ya utafiti wa sayansi na teknolojia na mahitaji ya ujenzi wa taifa, na kurekebisha mfumo wa mashirika mbalimbali na kufanya mageuzi ya utaratibu wa uendeshaji."

Baada ya kutekelezwa kwa mradi huo, Taasisi ya Sayansi ya China ilithibitisha malengo makubwa ya maendeleo kutokana na mahitaji ya kimkakati ya taifa na mwelekeo wa maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani. Malengo hayo ya maendeleo yanahusu sayansi na kwenye nyanja za upashanaji habari, maisha, mazingira ya maliasili, nishati, pamoja na bahari.

Wakati huo huo, Taasisi hiyo ilifanyia marekebisho makubwa katika mpango wa utafiti wa sayansi na mfumo wa mashirika tangu ilipoanzishwa. Mbali na hayo, taasisi ilianzisha vituo vikubwa vipya vya utafiti na kuweka mkazo katika utafiti wa mazingira ya dunia pamoja na utafiti wa Gene. Baada ya kufanya mageuzi, matawi ya taasisi ya China yalipungua kutoka 120 ya zamani na kufikia 80.

Kiongozi wa Idara ya utafiti wa fizikia katika Taasisi ya Sayansi ya China Bw. Sun Mu alisema:

" kupitia mradi wa uvumbuzi wa ujuzi, Taasisi ya Sayansi ya China ilianza kutumia mfumo mpya wa uendeshaji. kuwavuta wanasayansi wengi vijana kurudi China; kuchukua hatua mbalimbali ili kuhamasisha juhudi za kila mtu; na kutumia viwango vya kimataifa katika ukaguzi wa matokeo ya sayansi na teknolojia.

Shuguang 4000A

    kutekelezwa kwa Mradi wa uvumbuzi wa ujuzi, matokeo mengi zaidi ya sayansi na teknolojia yalipatikana katika Taasisi ya Sayansi ya China. Mwaka 2003, makala za taaluma zlizochapishwa kwenye magazeti ya sayansi ya kimataifa kuhusu China zilikuwa ni mara 2 kuliko miaka 6 iliyopita.                                                                            Katika miaka ya hivi karibuni, Idara ya utafiti wa Kompyuta ilitoa mchango mkubwa katika utafiti wa sayansi. Kompyuta yenye uwezo mkubwa iitwayo "Shuguang 4000A" iliyotengenezwa na  idara hiyo inaweza kufanya hesabau kwa kasi kubwa, kasi yake ilifikia nukta laki 11 kwa sekunde moja. Sasa Kompyuta hiyo inachukua nafasi ya 10 katika Kompyuta zenye uwezo mkubwa duniani. Mkuu wa idara hiyo Bw. Li Guojie anasema:

" mwaka 1995, tulitengeneza Kompyuta yenye uwezo mkubwa ya "Shuguang 1000", lakini wakati ule nafasi yetu ilikuwa ya 600. Sasa kasi ya hesabau ya kompyuta ya Shuguang 4000A imeongezeka mara 6700 kuliko ile ya zamani. Sasa Kompyuta za Shuguang 4000A zenye uwezo mkubwa zimeuzwa zaidi ya 1000 duniani."

Shuguan 1000

Ili kuunga mkono mageuzi ya Taasisi ya Sayansi ya China, serikali ya China ilitenga fedha nyingi zaidi katika utafiti wa sayansi. Mazingira ya utafiti wa taasisi hiyo na mapato ya wanasayansi yaliongezeka sana. Mwanasayansi wa idara ya utafiti wa fizikia Bw. Wang Jiantao alimwamabia mwandishi wa habari anasema:

" baada ya tekelezwa kwa mradi huo, mabadiliko makubwa yalipatikana katika mazingira ya

  uafiti wetu. Mwaka 1998, fedha tulizokuwa nazo kwa ajili ya utafiti zilikuwa kidogo. Lakini katika miaka mitatu iliyopita, fedha zilizotumika katika vifaa vya utafiti wa sayansi zilifikia Yuan milioni 150, hii ina maana makubwa kwa kazi yetu."

Kutokana na nguvu ya Taasisi ya Sayansi ya China inavyoongezeka siku hadi siku, wanasayansi wengi vijana waliofanya kazi au kusoma nchi za nje wanarudi China. Tuna imani kuwa, maendeleo ya China yatakuwa makubwa zaidi kutokana na msaada mkubwa wa matokeo ya sayansi na teknolojia ya China.

Idhaa ya kiswahili CRI 2004-11-10