Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-10 19:54:08    
Dunia kubadilika kuwa joto ni balaa kwa ncha ya kaskazini ya dunia

cri
    Utafiti uliofanywa na wanasayansi karibu 300 kwa miaka minne mfululizo kuhusu hali ya kubadilika kuwa joto kwa ardhi ya sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia, unaonesha kuwa hewa inayotolewa na shughuli za binadamu inayofanya hewa ya dunia kubadilika kuwa joto imeleta mabadiliko makubwa kwa hewa ya sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia na kufanya barafu ya huko kuyeyuka haraka.

    Habari zilizotolewa na gazeti la New York Times hivi karibuni zinasema kuwa utafiti uliofanywa na nchi nane zenye ardhi katika sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia unaonesha kuwa mabadiliko hayo huenda yataathiri wakazi, wanyama pori na shughuli za kiuchumi za sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia.

    Ingawa hali ya kubadilika kuwa joto kwa hewa ya sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia imeendelea kwa miongo kadhaa, na utafiti husika umewahi kufanyika, lakini utafiti uliofanywa safari hii ni wa kwanza wa kutathimini kwa pande mbalimbali chanzo na matokeo ya mwelekeo huo, ambayo yanachangia hoja inayokubaliwa na wanasayansi kuwa chanzo cha kubadilika kuwa joto kwa dunia ni kuongezeka kwa hewa inayofanya dunia kubadilika kuwa joto ikiwemo hewa ya carbon dioxide, na hewa ya sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia imebadilika kwa haraka zaidi kuliko sehemu nyingine za dunia, ambayo imechangiwa na kuyeyuka kwa barafu na theluji. Pia kutoweza kuakisi mwangaza wa jua kwa sehemu hiyo, kunaifanya ardhi na maji ya huko kuchukua joto jingi zaidi la nishati ya jua. Licha ya hayo hali hiyo pia inatokana na kutoweza kuchanganyika kwa hewa baridi ya anga ya juu na hewa iliyoko karibu na ardhi na bahari za sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia. Kuvua samaki kupita kiasi, kuongezeka kwa idadi ya watu na kupungua kwa hewa ya kwenye ukanda wa ozone pia kumeathiri hali ya mazingira ya asili ya sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia.

    Wanasayansi wanaona kuwa kupunguza utoaji wa hewa inayoweza kufanya dunia kubadilika kuwa joto, kunawawezesha wakazi na wanyama pori wa sehemu ya ncha ya kaskazini ya dunia kuzoea mabadiliko hayo.

Idhaa ya kiswahili CRI 2004-11-10