Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-17 10:29:45    
Shule ya Wushu katika kijiji nchini China

cri
Shule ya mchezo wa Wushu ya Zhonghua iko kwenye kijiji kimoja kilichoko mji wa Laizhou mkoani Shandong, mashariki mwa China. Shule hiyo ilianzishwa na mchezaji maarufu wa Wushu wa China Bw. Li Mingzhi. Bw. Li Mingzhi alipokuwa mtoto alianza kufanya mazoezi ya mchezo wa Wushu, alikuwa anapewa mafunzo na wachezaji wengi hodari wa mchezo wa Wushu. Mwaka 1992 alikataa ajira ya mshahara mkubwa ya nchi ya nje na kuamua kurudi maskani yake kuanzisha shule hiyo.

    Katika miaka 12 iliyopita, shule hiyo imebadilika kuwa shule kubwa iliyojulikana kote nchini China na hata duniani kutoka shule ndogo iliyoko kwenye kijiji kimoja. Wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo wamewahi kupata medali za dhahabu 75 nchini China na 32 duniani. Mbali na hayo, shule hiyo ilipeleka zaidi ya wanafunzi elfu tatu kwenye vyuo vikuu na vikundi maalum vya mchezo wa Wushu, na kuwa moja kati ya " shule kubwa 10 za mchezo wa Wushu nchini China."

    Saa 11 asubuhi, kengele inalia kwa wakati, na mazoezi ya wanafunzi yanaanza. Shule imeweka utaratibu kwa wanafunzi kuvaa nguo na kutandika kitanda kwa dakika kumi. Halafu wakakimbia kwenda kwenye kiwanja cha michezo na kufanya mazoezi ya asubuhi.

    Saa 12 na dakika 10, wanafunzi wanamaliza mazoezi ya asubuhi yakiwemo kukimbia, kurusha mateke, kujizungusha, kurusha ngumi, kila mmoja anaonekana kuwa na nguvu kubwa. Baada ya kifungua kinywa wanakwenda madarasani na kuanza kusomo. Mkuu wa shule hiyo Bw. Li Mingzhi anasema:

    " si kama tu, shule hiyo inazingatia mchezo wa Wushu, bali pia masomo ya elimu, wanafunzi wakijifunza masomo vizuri na wataweza kufahamu vizuri ubora na maana ya mchezo wa Wushu, na katika siku za usoni watakuwa wachezaji bora wa Wushu."

    Baada ya masomo ya mchana, wanafunzi wanakwenda kula chakula cha mchana na kupumzika. Saa 10 alasiri mazoezi ya mchezo wa Wushu yanaanza rasmi. wanafunzi wanaanza kufanya mazoezi chini ya mafundisho ya walimu kwa kutumia vyombo mbalimbali kama vile jambia, fimbo, na viboko.

    Wanafunzi hawa wanaosoma katika shule hiyo wengi walijiunga na shule hizo kutokana na kuupenda mchezo wa Wushu. Na miongoni mwa wanafunzi hao, wengi wanakuwa wamefanya mazoezi ya Wushu kabla ya kujiunga na shule hiyo. Kuwawezesha watoto hao wanaopenda mchezo wa Wushu kuishi pamoja kwa amani si jambo rahisi.

Zhi Yuntao ni bingwa wa mchezo wa Wushu wa China mwaka huu na Tan Songtao ni bingwa wa mkoa wa Shandong wa mwaka huu, sasa wanafunzi hawa wawili ni marafiki mwazuri, lakini mwanzoni walipoingia shule walikuwa wakipambana. Mwalimu wao Bw. Liu Jian anasema:

    " nakumbuka kuwa, watoto hawa wawili walipoingia shuleni walikuwa wakigombana kutokana na kutoelewana vizuri kwenye mazoezi. Kutokana na msaada wa mwalimu, walibadilikna a kuwa marafiki wazuri. Na katika mazoezi ya miaka miwili walisaidiana na wakapata mafanikio mazuri."

    Zhi Yuntao na Tan Songtao walisema kuwa, mwanzoni waliposoma katika shule hiyo hawakuweza kuelewa halisi maana ya mchezo wa Wushu, walifikiri kuwa, mchezo wa Wushu uliweza kutatua masuala mbalimbali na kupata heshima mbele ya watu wengine. Lakini walimu walituambia kuwa, mchezo wa Wushu unaweza kujenga mwili na kujilinda, lakini ukitaka kutatua matatizo kwa ngumi utakwenda kinyume na maana halisi ya mchezo wa Wushu.

    Dai Shuang ni mwanafunzi wa kike wa shule hiyo, alisema kuwa, katika shule ya mchezo wa Wushu ya Zhonghua si kama tu anaweza kujifunza masomo mbalimbali, bali pia anaweza kufanya mazoezi ya mchezo wa Wushu na kujenga mwili. Alisema kuwa, shule hiyo ilimsaidia kujenga imani yake, sasa lengo lake ni kujiunga na Chuo Kikuu cha Polisi cha China na kuwa polisi baada ya kuhitimu masomo.

    Shule ya mchezo wa Wushu ya Zhonghua inaendelea kwa kasi kubwa. Hivi sasa Mkuu wa Shule hiyo Bw. Li Mingzhi anapanga kuanzisha shule nyingine nchi za nje, anasema:

    " kabla ya mwaka 2008, tutaijenga shule ya mchezo wa Wushu ya Zhonghua kuwa shule ya kimataifa, kuwawezesha wageni wengi zaidi kutambua utamaduni wa jadi wa Wushu wa China na kuupenda mchezo wa Wushu."

    Hivi sasa, shule hiyo imeanzisha matawi huko California, Marekani na Pairs, Ufaransa, ambapo shughuli za kuanzisha tawi mjini Seoul zimeanza. Mbali na hayo wanafunzi kutoka Marekani, Canada, Italia, Uholanzi, Ujerumani, Israel, Korea ya Kusini, na Japan wamefika kwenye kujifunza mchezo wa Wushu.

Idhaa ya kiswahili CRI 2004-11-17