Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-17 20:08:07    
Kuacha kuvuta sigara kunanufaisha meno

cri

    Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na taasisi ya madaktari wa meno nchini Japan inasema kuwa, kuvuta sigara kunaongeza ugonjwa wa fizi na kuathiri matokeo ya matibabu ya meno. Takwimu zilizotolewa na wizara ya afya ya Japan zinaonesha kuwa katika mwaka 2002, kiasi cha 24% ya watu wa Japan walikuwa wanavuta sigara, na 43% kati yao walikuwa ni wanaume. Ingawa mwezi Mei mwaka jana, ilitolewa nyongeza ya sheria ya kulinda watu wasiovuta sigara kuathiriwa na moshi wa sigara, lakini profesa mmoja wa kitivo cha meno cha chuo kikuu cha Tokyo alisema kuwa sera zilizotungwa bado siyo kamili katika kulinda afya ya meno na matibabu yake.

 

    Taarifa hiyo inasema kuwa kuvuta sigara ni rahisi kusababisha ugonjwa wa fizi na saratani. Ingawa sigara zinazouzwa nchini Japan ni za kutafunwa, zinaweza kulinda watu wasiovuta sigara kuathiriwa na moshi wa sigara, lakini wale wanaotumia sigara za aina hiyo ni rahisi kuugua saratani ya mdomoni na kuleta madhara makubwa kwa sehemu ya juu ya mdomo na sehemu ya uso. Aidha, kuvuta sigara kunaweza kufanya ugonjwa wa fizi kurudia tena, na kuacha kuvuta sigara kunaweza kupunguza kiwango cha hatari ya kuugua ugonjwa wa fizi hadi kiwango cha watu wasiovuta sigara.

    Taarifa iliyotolewa hivi karibuni kuhusu utafiti mpya uliofanywa juu ya sigara, inasema kuwa kuvuta sigara kunaweza kusababisha saratani za mdomo wa chupa ya uzazi kwa wanawake, figo, mawengu, utumbo wa chakula na damu.

    Taarifa hiyo inasema kuwa miaka ya maisha ya wanaume wanaovuta sigara ni pungufu kwa miaka 13.2 ikilinganishwa na wanaume wasiovuta sigara, hali miaka ya maisha ya wanawake wanaovuta sigara ni pungufu ya miaka 14.5 ikilinganishwa na wanawake wasiovuta sigara.

    Idara ya afya ya Singapore hapo zamani ilikadiria kuwa kila siku kwa wastani watu 7 wanakufa kutokana na ugonjwa unaosababishwa na uvutaji wa sigara nchini humo, lakini hivi sasa idara hiyo imesema kuwa kutokana na utafiti mpya uliofanywa, idadi hiyo itaongezeka zaidi kuliko ilivyokadiriwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-17