Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-22 21:41:18    
Mandhari nzuri ya sehemu ya Taohuayuan

cri

    Nchini China kuna hadithi moja iliyoeleza kuwa, siku moja mvuvi mmoja alipotea njia na kuingia kwenye bonde moja lililofunikwa na maua mengi ya mpichi. Mvuvi huyo akaingia kwenye bonde hilo na kuona kuwa watu wa huko wanaishi maisha ya utulivu na baraka, na hata hawajui mabadiliko yoyote yaliyotokea nje ya bonde hilo. Baadaye mvuvi huyo akawaambia watu wengine hali aliyoiona sehemu hiyo. Watu wengi waliochoshwa na maisha yao ya mijini wakawa na kiu ya kwenda huko. Sehemu hiyo ya bonde la maua ya mpichi ndiyo Tiaohuayuan ya mji wa Changde mkoani Hunan, kusini mwa China.

    Sehemu ya Tiaohuayuan iko kusini ya mji wa Changde. Sehemu hiyo yenye eneo la hekta zaidi ya 130 ilipandwa miti zaidi ya laki moja ya mpichi, kila ifikapo majira ya kuchanua kwa maua ya mpichi, sehemu hiyo kweli inapendeza kweli.

    Siku moja ya majira ya kupukutika tulifika Changde, tukapanda mlima kwa kufuata misitu. Njiani tuliona pango moja dogo la kawaida. Tukaingia kwenye pango hilo, tukatoka nje tukafika kwenye kijiji cha Qinren. Mwongozaji wa utalii Zhou Liying alituambia kuwa, hakuna njia nyingine inayoweza kutufikisha kwenye kijiji cha Qinren, bali tunapaswa kupita kwenye pango dogo la mlima. Kweli tuliona kijiji hicho kiko katika sehemu ya kujitenga na nje.

    Watu wanapaswa kupita kwenye pango hilo la mlima, halafu wanaweza kuona nyumba na mashamba na mabwawa ya kufugia samaki. Kijiji cha Qinren kina familia 9 tu, jina la ukoo la wakulima wengi linaitwa Qin. Vitu vingi vya matumizi ya wakulima wa huko vinatengenezwa nao wenyewe, vingine vilinunuliwa kutoka chini ya mlima. Majengo ya kijiji hicho mengi yalijengwa kwa miti na mianzi.

    Tulipoingia kwenye kijiji hicho kidogo cha kale, kweli tulijisikia hali tofauti na ile tuliyoiona katika vijiji vingine. Nyumba mojamoja zilizojengwa kwa miti na mianzi ziko katikati ya kila tuta kuna mashamba na mabwawa. Nyuma ya nyumba imepandwa miti ya mpichi, na watoto wanacheza mbele ya nyumba. Kijiji hicho kinazungukwa na milima kwa pande tatu, upande mmoja unaegemea ziwa moja. Inasemekana kuwa, mababu wa wakulima wa kijiji cha Qinren walikuwa wakimbizi wa enzi ya Qin ya kale zaidi ya miaka 2000 iliyopita, na walikwenda huko kukwepa vurugu za vita, wakaanza kuishi huko na kuzaliana na kujitenga na nje ya sehemu hiyo.

    Ingawa hivi sasa wageni wanafika huko kila siku kutokana na usitawi wa shughuli za utalii, lakini kijiji hicho kingali bado kinaonekana tulivu sana, na wakulima wa huko bado ni wachangamfu, wakarimu na wapole sana. Tulimwona mwanamke mmoja mbele ya nyumba moja ya mbao, tukasalimiana na kuongea naye. Punde si punde mwanamke huyo aliingia ndani ya nyumba yake na kutuletea chai yenye harufu nzuri. Mwenyeji mmoja alituambia kuwa, tulikaribishwa kwa heshima kubwa na wenyeji wa huko, kwani chai ya Lei ni chai ya Lei ya Qinren inayojulikana sana, chai hiyo huwakirimu wageni kwa heshima kubwa.

    Chai hiyo ilitengenezwa kwa tangawizi, mchele, chai pamoja na simsim na korosho zilizosagwa, halafu kutiwa maji na kuchemshwa, chai hiyo inaweza kusaidia watu kuondoa joto mwilini na kuzuia mafua. Wakati wa mapumziko, wakulima wa huko hukaribisha jamaa na marafiki nyumbani wakinywa chai na kula vyakula vingine hata kuanzia asubuhi hadi jioni. Hii imeonesha maisha ya utulivu na ya kujiburudisha ya wakulima wa kijiji hicho.

    Wasikilizaji wapendwa, wiki ijayo tutaendelea kuwasimulia kuhusu vivutio vya sehemu ya Taohuayuan ya mji wa Changde, mkoani Hunan.

Idhaa ya Kiswahili2004-11-22