Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-24 21:20:11    
Maendeleo makubwa yapatikana katika elimu ya mkoa unaojiendesha wa Tibet

cri
Mwaka 1951, Tibet ilipokombolewa kwa amani, watibet waliokuwa na elimu walikuwa ni wachache sana. Katika miaka mingi iliyopita, kutokana na misaada ya serikali kuu ya China, hali ya elimu ya Tibet inabadilika na kuwa nzuri siku hadi siku. Hivi sasa sehemu nyingi za mkoa unaojiendesha wenyewe wa Tibet zilianza kutekeleza sera ya elimu ya lazima ya miaka 9..

    Mliosikia ni sauti ya wanafunzi wa shule ya msingi ya wilaya ya Lulang ya sehemu ya Linzhi mkoani Tibet. Lulang ni wilaya ndogo yenye watu zaidi ya 1000 tu. Wanafunzi 163 wa shule ya msingi ya Lulang wote wanatoka kwenye familia za watibet wa huko. Zamani, shule hiyo ilikuwa na madarasa machache, vifaa rahisi vya kufundisha na mazingira ya shule yalikuwa ya hali duni. Mwaka 2003, serikali ya mkoa unaojiendesha wa Tibet ilitoa fedha zipatazo Yuan milioni moja ili kukamilisha ujenzi wa miundo mbinu ya shule hiyo. Mbali na hayo, shule hiyo ilianzisha darasa lenye vifaa vya mtandao wa internet. Katika darasa hilo wanafunzi wanaweza kutembelea mtandao wa internet, na kuangalia televisheni ya satilaiti. Wanafunzi walimwambia mwandishi wa habari kuwa, wanafurahia kusoma katika shule hiyo.

    Hivi sasa katika mkoa wa Tibet, maendeleo makubwa yamepatikana katika kuboresha mazingira ya elimu. Kwa kuwa viongozi wa serikali ya mkoa unaojiendesha wa Tibet wanazingatia sana hali ya elimu ya Tibet, na watu wa sehemu nyingine za China pia wanatoa misaada mikubwa kwa Tibet. 

    Kiongozi wa wilaya ya Jiangzi ya sehemu ya Rikaze mkoani Tibet Bw. Li Dongchang alitoka Shanghai, mji mkubwa wa China. Alifika Tibet miaka kadhaa iliyopita, ili kuunga mkono maendeleo ya Tibet na kushughulikia elimu mkoani Tibet. Baada ya kufika Tibet alikuwa anazingatia sana kazi ya elimu ya msingi. Hivi sasa, kutokana na jitihada za Bw. Liu, kampuni kadhaa za China zimetoa michango ya Yuan milioni 1.8 ili kuboresha ujenzi wa miundo mbinu ya elimu ya Tibet. Anasema:

    " Tunaona kuwa elimu ni msingi kwa ustawishaji wa Tibet, ingawa mazingira ya uchumi wa Tibet si mazuri lakini tunapaswa kuwawezesha watoto kwenda shule. makada wote wa sehemu nyingine walipofika Tibet walizingatia sana elimu."

    Misaada mikubwa kutoka serikali ya Tibet na kampuni mbalimbali za China si kama tu unaboresha hali ilivyo ya elimu ya Tibet bali pia umebadilisha maoni ya watibet kuhusu elimu. Wafugaji na wakulima wa Tibet walitambua mabadiliko makubwa katika maisha yao kutokana na maendeleo ya elimu, wanaona kuwa elimu inaletea faida kubwa kwa maisha, hivyo wanafurahia kuwapeleka watoto kusoma shuleni.

    Suolang Deji ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya sehemu ya Rikaze mkoani Tibet. Alimwambia mwandishi wa habari kuwa, wazazi wake ni wafugaji, hawawezi kusoma. Lakini wazazi wake walimuunga motto wao kwenda shule. Alisema kuwa anapenda sana kusoma vitabu. Kutokana na sera ya wizara ya elimu ya China, vitabu vyote vya shule za msingi na sekondari vinatolewa bure na serikali. Katika masomo ya shule, Suolang Deji anapenda masomo ya lugha ya kichina na kingereza. Hivi sasa anaweza kuzungumza na wageni kwa kingereza rahisi. Anasema:

    " Hivi sasa mazingira ya shule ni mazuri, tuna kompyuta, tunasoma lugha ya kingereza, kichina na kila kitu, baadaye tutakwenda chuo kikuu."

    Hivi sasa kazi ya elimu ya mkoa unaojiendesha wa Tibet inaendelea kwa kasi, idadi ya watu waliopata elimu inaongezeka sana. Katika shule zaidi ya 1000 katika sehemu hiyo, 87% ya watoto wanaokwenda shuleni .

    Ofisa wa idara ya elimu na michezo ya Lasa Bw. Jiayong Sangding ni mfanyakazi wa elimu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30. Alipozungumzia maendeleo ya elimu ya Tibet alifurahi sana anasema:

    " kazi ya elimu ya Tibet imebadilika kuwa nzuri katika miaka ya hivi karibuni. Kabla ya kufanya mageuzi kulikuwa hakuna elimu yenye maana ya kisasa. Mwaka 1952 serikali ya China ilianzisha shule ya kwanza ya msingi mjini Lasa, hadi mwezi October mwaka huu, elimu ya lazima ya miaka 9 inatekelezwa kimsingi mjini humo."

   

    Bw. Jiayong Sangning alisema kuwa, katika miaka 10 iliyopita, serikali ya China ilitoa fedha za Yuan milioni 400 ili kujenga shule mpya au kukarabati shule mkoani Tibet. Mbali na hayo, mikoa mingi pia imetoa misaada kwa elimu ya Tibet. Hadi sasa misaada kutoka mikoa mingine ya China kwa ajili ya kujenga shule mpya na kuboresha vifaa vya elimu vya Tibet imefikia Yuan milioni 200.

    Habari zinasema kuwa, hadi kufikia mwaka 2010, lengo la elimu ya lazima ya miaka 9 na kuondoa hali ya watu kutojua kusoma na kuandika mkoani Tibet litatimizwa kimsingi.

Idhaa ya kiswahili 2004-11-14