Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-24 22:21:18    
China yafaulu kurusha satellite ya kwanza ya uchunguzi wa hali ya hewa

cri

    Satellite ya kwanza ya uchunguzi wa hali ya hewa inayotulia kwenye anga ya juu, ilirushwa angani kwa roketi ya aina ya "Masafa Marefu" No.3 A. satellite hiyo, ambayo inajulikana kwa jina la "Fengyun" No.2 C, ilisanifiwa na kutengenezwa na China yenyewe, ilirushwa angani saa 3 na dakika 20 ya tarehe 19 mwezi Oktoba kwenye kituo cha Xichang.

    Dakika 24 hivi baada ya roketi hiyo kuwashwa moto, kituo cha upimaji na udhibiti wa Satellite cha Xian na meli ya upimaji inayojulikana kwa "Yuanwang", ambayo ilikuwa ikitekeleza jukumu la upimaji kwenye bahari ya Pasifiki, viliripoti kuwa Satellite hiyo imefanikiwa kuingia katika njia yake inayoenda sambamba na dunia. Baada ya kurekebishwa katika siku chache zilizofuata, Satellite hiyo ilitulizwa kwenye anga ya nyuzi ya 105 ya longitudo ya mashariki.

    Satellite ya "Fengyun" No.2 C yenye uzito wa tani 1.38 ni ya uchunguzi wa hali ya hewa, na satellite mbili za A na B zilizorushwa angani mwaka 1997 na 2000 zilikuwa ni za majaribio. Satellite ya "Fengyun" No.2 C iliyorushwa angani safari hii ni ya kisasa zaidi ikilinganishwa na satellite za A na B. Satellite hiyo inaweza kupiga picha za mawingu na kukusanya takwimu kuhusu hali ya hewa pamoja na mito na maziwa. Licha ya hayo satellite hiyo inaweza kufanya upimaji kuhusu tufani, mvua, ujoto wa maji ya bahari, mawingu pamoja na mionzi ya jua.

    Tangu iliporusha kwa mara ya kwanza satellite ya namna hiyo mwaka 1987, China imerusha satellite 7 za uchuguzi wa hali ya hewa. Satellite zote hizo zilisanifiwa na kutengenezwa taasisi ya utafiti wa teknolojia ya safari za anga ya juu ya Shanghai. Satellite ya "Fengyun" No.2 C iliyorushwa angani safari hiyo inaweza kufunika theluthi moja ya ardhi ya dunia kutoka anga ya Ikweta katika nyuzi 105 ya longitudo ya mashariki. Kutokana na mpango wa maendeleo ya satellite za uchunguzi wa hali ya hewa, China itarusha angani satellite nyingine kadhaa za uchunguzi wa hali ya hewa katika miaka ya karibuni ili kukidhi mahitaji ya utabiri wa hali ya hewa na upimaji wa hewa ya dunia.

    Roketi iliyotumiwa safari hiyo ya kurusha satellite ya "Fengyun" No.2 C ina nguvu ya kubeba uzito wa tani 300 zikiwa na uzito wake yenyewe wa tani 243. Roketi ya aina hiyo yenye urefu wa mita 52.52, inayojulikana kwa "Masafa Marefu" No.3 A ni chombo muhimu cha kupeleka angani satellite za China. Roketi za "Masafa Marefu" zimetumiwa mara 81, na zimefanikiwa kupeleka angani satellite kwa mara 39 mfululizo tangu mwaka 1996.

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-24