Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-25 21:41:02    
Mto Changjiang

cri

    Chanzo cha Mto Changjiang kiko kusini magharibi ya kilele cha Geladandong cha safu ya mlima wa Tanggula katika uwanda wa juu wa Qinghai na Tibet. Tawi kuu la mto huo linapita kwenye mikoa na miji na mikoa inayojiendesha 11 ikiwa ni pamoja na Qinghai, Tibet, Sichuan, Yunnan, Chongqing, Hubei, Hunan, Jiangxi, Anhui, Jiangsu na Shanghai, na kuingia kwenye bahari ya Donghai mashariki ya kisiwa cha Chongming. Urefu wa mto huo ni kilomita 6300, kilomita 800 zaidi ya Mto Manjano. Urefu huo umechukua nafasi ya tatu duniani ukiwa ni chini ya Mto Nile ulioko barani Afrika na Mto Amazon ulioko barani Amerika ya Kusini. Mto Nile unapitia nchi 9 na Mto Amazon unapitia nchi 7, lakini Mto Changjiang uko nchini China tu.

    Tawi kuu la Mto Changjiang unapitia sehemu ya kati ya China kuanzia magharibi hadi mashariki. Mamia ya matawi yake yamesambaa katika maeneno makubwa hadi kufikia mikoa wa Guizhou, Gansu, Shanxi, Henan, Guangxi, Guangdong, Zhejiang na Fujian. Eneo hilo limefikia kilomita za mraba milioni 1.8, ambalo ni asilimia 20 ya eneo la ardhi ya China. Na kiasi kikubwa cha maji ya Mto wa Huaihe pia yanaingia kwenye mto wa Changjiang kupitia Mfereji wa Dayunhe.

    Sehemu ya juu ya Mto Changjiang iko magharibi ya mji wa Yichang. Urefu wa sehemu hiyo ni kilomita 4504 na eneo la bonde la mto limefikia kilomita za mraba milioni 1. Na katika sehemu ya juu, sehemu kutoka Zhimen hadi Yibin yenye urefu wa kilomita 3464 inaitwa Mto wa Jingshajiang, na sehemu kutoka Yibin hadi Yichang yenye urefu wa kilomita 1040 inaitwa Mto wa Chuanjiang. Sehemu ya kati ya Mto Changjiang inaanzia Yichang hadi Hukou, ambayo urefu wake ni kilomita 955 na eneo la bonde ni kilomita za mraba milioni 6.8. Sehemu iliyoko mashariki ya Hukou ni sehemu ya chini. Sehemu hiyo ina urefu wa kilomita 938 na eneo la kilomita za mraba milioni 1.2.

    Mto Changjiang ni mto wenye maji mengi zaidi nchini China, kiasi cha maji kimefikia mita za ujazo bilioni 961, ambacho kimechukua asilimia 30 ya maji ya mito nchini China na ni mara 20 ya maji ya Mto Manjano. Kiwango hicho pia kinachukua nafasi ya tatu duniani ikiwa ni chini ya Mto Amazon na Mto Congo iliyoko katika sehemu ya Ikweta. Na ingawa maeneo ya bonde la Mfereji wa Panama na Mto Mississippi ni makubwa kuliko Mto Changjiang, lakini maji katika mito hiyo ni machache, ambapo maji ya Mfereji wa Panama ni asilimia 70 ya Mto Changjiang, na Mto Mississipi ni asilimia 60.

    Kufuatana na aina za maeneo ya kimaumbile ya China, bonde la mto wa Changjiang linaweza kugawanywa katika sehemu tatu, yaani sehemu ya kati ya China, sehemu ya kusini magharibi na sehemu ya Qingzang.

    Uchumi, sayansi na teknolojia kwenye bonde la mto wa Changjiang ni zenye msingi mkubwa. Uchumi wa sehemu hiyo unachukua nafasi muhimu katika uchumi wa China. Kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo si kama tu unasaidia kuharakisha maendeleo ya uchumi wa China na kuinua faida ya kiuchumi, bali pia kutatoa mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano wa sehemu tatu za Mto Changjiang, kutimiza sehemu hizo tatu kusaidiana kwa maliasili, teknolojia na uchumi wao, na kusukuma mbele maendeleo ya nguvu za uzalishaji yenye uwiano.

    Katika maendeleo ya uchumi wa zama za karibu, bonde la Mto Changjiang ni chimbuko la viwanda nchini China. Katika kipindi kuanzia kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China hadi mwishoni mwa miaka ya 70, uchumi wa sehemu ya ndani ya China ulipata maendeleo makubwa, na maendeleo ya uchumi wa sehemu ya pwani ya bonde la Mto Changjiang yalikuwa makubwa zaidi nchini China.