Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-29 21:08:54    
China yaanzisha mafunzo ya kuzuia ugonjwa wa UKIMWI katika mpango wa mafunzo ya shule

cri
    Wizara ya elimu ya China hivi karibuni ilizitaka idara mbalimbali za elimu zianzishe masomo ya kuzuia ugonjwa wa UKIMWI katika mafunzo ya shule za sekondari na vyuo vikuu.

    Naibu waziri wa elimu Bi. Chen Xiaoya leo amesema katika harakati za kuzuia ugonjwa wa UKIMWI kuwa maudhui ya kuzuia ugonjwa wa UKIMWI ni pamoja na kupata ujuzi wa kawaida kuhusu ugonjwa huo, hatua za kuzuia ugonjwa huo, hasara zinazoletwa na UKIMWI kwa jamii na uchumi, matumizi ya dawa za kulevya na UKIMWI, ujuzi kuhusu kuchangia damu bila malipo na sera husika za kuzuia na kudhibiti UKIMWI.