Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-30 14:34:33    
AAPP yaendelea kukua

cri

     AAPP ni shirikisho linaloundwa na mabunge ya nchi zenye mamlaka za Asia na eneo la Pasifiki na nchi zenye mamlaka ambazo baadhi ya ardhi zake ziko barani Asia, na lilianzishwa mwezi Septemba, 1999 huko Dacca, mji mkuu wa Bangladesh. Madhumuni yake ni kuwa katika msingi wa kuheshimu na kuiunga mkono Katiba ya Umoja wa Mataifa, kukuza urafiki na ushirikiano kati ya nchi za Asia na mabunge yao, ili kuhimiza amani na utulivu wa Asia na dunia. Shirikisho hilo linatoa nafasi ya kubadilishana maoni na kukuza urafiki baina ya wabunge wa nchi wanachama ili waweze kutoa maamuzi kuhusu masuala makubwa katika msingi wa kushauriana kwa kauli moja.

    AAPP inaendelea kukua baada ya kuanzishwa, na nchi wanachama zimeongezeka kuwa 37 kutoka 26 za mwanzoni. China ni moja ya nchi wanachama ya waanzilishi wa shirikisho hilo. Katika mkutano wa Baraza la utendaji la AAPP uliofanyika mjini Manila mwezi Julai, mwaka huu ulipitisha maombi ya nchi tatu Palau, Falme za kiarabu na Libya kushiriki katika shirikisho hilo. Kufuatana na ajenda ya mkutano wa mwaka huu, ruhusa za uanachama wa nchi hizo tatu zitapitishwa mwishoni na kikao cha mkutano huo. Wakati huo, Libya itakuwa nchi mwanachama ya kwanza ya shirikisho hilo ambayo sio nchi ya Asia kabisa.

    Kabla ya mkutano wa mwaka huu, AAPP imefanya mikutano minne ya mwaka. Kutoka tarehe 16 hadi 19, Aprili, 2002, mkutano wa tatu wa AAPP ulifanyika mijini Beijing na Chongqing, China, na wajumbe zaidi ya 400 kutoka nchi zaidi ya 30 za Asia walihudhuria mkutano huo na kujadiliana kuhusu "amani na maendeleo". Mwishoni mkutano huo ulipitisha Azimio la Chongqing.

    Kwa mujibu wa sheria za AAPP, mwenyekiti wa jumuiya hiyo anachaguliwa na mkutano wa mwaka. Kipindi chake cha madaraka ni mwaka mmoja. Mwenyekiti wa hivi sasa ni spika wa baraza la chini la bunge la Philippines Bw. Jose de Venecia. Kwa kawaida, spika wa bunge la Pakistan, ambayo ni nchi mwenyeji wa mkutano wa 5 wa AAPP, Bw. Chaudhry Amir Hussain atachaguliwa kuwa mwenyekiti mpya katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 5 unaofanyika leo, na ataendesha mkutano huo.

    Katika miaka 5 baada ya kuanzishwa kwake, AAPP imefanikiwa kufanya kazi nyingi ili kuhimiza amani na maendeleo ya Asia. Kutokana na athari yake kuongezeka, AAPP sio tu baraza muhimu la mabunge na wabunge wa nchi za Asia, bali pia ni njia muhimu kwa wananchi wa nchi za Asia kuongeza maelewano na uaminifu, kubadilishana maoni na kushirikiana.

Idhaa ya kiswahili 2004-11-30