Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-30 14:33:32    
Upepo wa Suala la Nyuklia la Iran Umetulia Tena

cri
    Mtendaji mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Bw. Mohamed Elbaradei mbele ya vyombo vya habari alitangaza kuwa vifaa vyote vya kushughulikia uranium vimefungwa na viko chini ya usimamizi wa shirika hilo, na wakati wote lina haki ya kutafanya ukaguzi bila taarifa ili kuhakikisha kama kweli imesimamisha, na endapo ukaguzi ukizuiliwa mtendaji huyo atatoa ripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Tokea mwezi Juni mwaka jana, shirika hilo liliwahi kupitisha maazimio mengi kuhusu suala la nyuklia la Iran, na kati ya maazimio hayo, azimio la tarehe 18 Septemba lilitaka Iran isimamishe shughuli zote za uranium kabla ya tarehe 25 Novemba. Nchi za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zimeahidi kutoa nishati ya nyuklia kwa ajili ya matumizi ya kawaida na kusaidia kujenga kinu cha nyuklia, kustawisha ushirikiano na Iran katika miradi mingi na kuiunga mkono ijiunge na WTO ilimradi Iran ikubali kusimamisha shughuli za uranium. Kuhusu mambo hayo pande mbili kati ya Iran na nchi tatu ziliafikiana katika tarehe 14 mwezi huu.

    Tarehe 25 bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki ilianza kufanya mkutano kujadili suala la nyuklia la Iran. Mkutano huo wa siku mbili ungemalizika tarehe 26 kama ulivyopangwa, lakini kutokana na kuwa Iran ghafla ilitoa ombi la kuendelea na shughuli za kusafisha uranium, mkutano huo ulikuwa hauna budi kurefushwa. Iran na nchi tatu za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zikashauriana haraka faraghani, na mweshowe zilipatana. Tarehe 28 Iran iliwasilisha barua yake kwenye Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki ikitangaza kufuta ombi lake la kuendelea na shughuli za kusafisha uranium, na kutokana na msingi huo nchi tatu ziliwasilisha azimio la suala la nyuklia la Iran kwenye baraza hilo.

    Mwaka mmoja uliopita, kwa lengo la kuinua hadhi ya nchi tatu katika Umoja wa Ulaya na kuondoa kisingizio cha Marekani kufanya matata, zilijitolea kufanya usuluhisho wa suala la nyuklia la Iran. Ni sawa kwamba kweli usuluhisho umepata mafanikio kwa kiasi fulani ingawa ulikumbwa na matatizo mengi. Hata hivyo, usuluhisho huo haujaifanya Iran iache kabisa haki yake ya kutoshughulikia nishati ya nyuklia kwa matumizi ya kawaida. Iran inaona kuwa hii ni haki yake iliyopo kwennye katiba la kimataifa, na inastahiki wakati wowote kurudisha shughuli hiyo ya kusafisha uranium. Hii ndio sababu ya Iran kuwa kigeugeu katika suala la nyuklia.

    Iran inaridhika na azimio la tarehe 29 la Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki. Nchi hiyo imewahi kudokeza kuwa Azimio kuhusu kusimamisha shughuli za kusafisha uranium ni "hatua ya hiari" inayochukuliwa na Iran wala siyo "wajibu wa kisheria". Haya maneno yameandikwa kwenye azimio kwa ombi la Iran. Iran inaona kuwa kuandika hivyo kunamaanisha kwamba haki ya Iran ya kutumia nishati ya nyuklia kwa matumizi ya kawaida imetambulika. Hivi sasa Iran ina matumaini makubwa kuhusu mazungunzo na nchi tatu za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza yatakayofanyika tarehe 15 Desemba na kuanzisha "kipindi kipya cha ushirikiano na Umoja wa Ulaya".

    Wachambuzi wanaona kuwa azimio hilo la Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki ni hatua nyingine ya kuridhisha katika utatuzi wa kiamani wa suala la nyuklia la Iran, lakini safari bado ndefu. Hivi sasa Iran inaendelea kushikilia haki yake ya kujiendeleza katika teknolojia ya uranium; matokeo ya mazungumzo yake na nchi tatu kwa sasa bado ni kitendawili. Zaidi ya hayo, haijulikani kama Marekani itachukua hatua fulani ya kuzidisha utatanishi wa suala la nyuklia la Iran.

Idhaa ya kiswahili 2004-11-30