Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-30 18:35:29    
Kwa nini China kuharakisha ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji

cri

    Hivi haribuni, kituo cha kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji cha Gou Pitan kimefanikiwa kuzuia maji kwenye mto Wujiang, mkoani Guizhou, China, kituo hicho ni kituo muhimu kabisa cha mradi wa kusafirisha umeme hadi mashariki kutoka magharibi nchini China, ambao wingi wa hisa zake zinamilikiwa na kampuni ya umeme ya China. Hali kadhalika, kampuni hiyo imetangaza kuwa kituo hicho kitaanza kuzalisha umeme mwaka 2009 kabla ya wakati uliowekwa. Kutokana na hali hiyo, wataalamu wa nishati walisema kuwa China inapaswa kuharakisha mwendo wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji.

    Kwa nini China inaharakisha ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji?

    Kwanza, nguvu ya maji ni nishati inayoweza kutengenezwa upya, pia ni chaguo ya kwanza ya nchi mbalimbali duniani katika kuzalisha umeme. Uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya maji, ambao ni shughuli ya kimsingi ya nchi yenye maliasili nyingi ya nguvu ya maji, una umuhimu mkubwa kwa kuhifadhi na kutumia ardhi, kuboresha mazingira na kusukuma mbele maendeleo endelevu ya uchumi na jamii.

    Pili, uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya maji ni njia muhimu ya kudhibiti maji ya mito. Hali isiyo na uwiano ya kunyesha mvua katika nchi yetu inasababisha mafuriko ya maji na ukame kutokea mara kwa mara, na kutokuwa na miradi ya kudhibiti maji kwenye sehemu ya juu ya mito ni sababu kubwa ya kutoweza kudhibiti hali hiyo. Uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya maji ni mambo muhimu katika kutimia maliasili ya maji. Miradi ya kudhibiti maji kwenye sehemu ya juu na ya kati ya mito ambayo ni sehemu yenye maliasili nyingi ya nguvu ya maji itapunguza maafa kwenye sehemu ya chini na ya kati ya mito, na pia italeta ufanisi kwa kazi mbalimbali za kumwagilai maji mashambani, kutoa maji, kusafarisha bidhaa kwa njia ya meli na kusafirisha maji.

    Tatu, uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya maji utasaidia hifadhi ya mazingira. Nguvu ya maji ni nishati mbadala nzuri wa makaa ya mawe ambayo italeta uchafuzi katika mazingira. Aidha, kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji kinaweza kuboresha mazingira na kuzuia mmomonyoko wa ardhi.

    Nne, uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya maji utaleta faida kubwa kwa jamii, hali ambayo imethibitishwa na mifano nyingi ya nchini na ya nchi za nje. Miradi ya kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji sio tu italeta ufanisi mkubwa katika kukinga mafuriko ya maji, kumwagilai maji mashambani, kutoa maji, kusafarisha bidhaa kwa njia ya meli, kusafirisha maji, kufuga na utalii, bali pia italeta nafasi nyingi za ajira, na kusukuma mbele uchumi wa sehemu.

    Kutokana na hali ya matumizi ya nishati nchini China, kuharakisha mwendo wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji ni chaguo muhimu ya mkakati wa nishati wa China.

    Kwa upande mmoja, kiwango cha matumizi ya nguvu ya maji kiko chini. Uchunguzi mpya unaonesha kuwa jumla ya nguvu ya maji nchini China ni zaidi ya kilowati milioni 680, miongoni ya nguvu hiyo, zaidi ya kilowati milioni 400 inaweza kutumiwa kwa kuzalisha umeme., Hivi sasa China imekuwa nchi ya kwanza duniani kwa uwezo wake wa kuzalisha umeme kilowati milioni 100 kwa nguvu ya maji. Lakini kiasi cha nguvu ya maji inayotumiwa hakifikii asilimia 25 ya jumla. Kuna pengo kubwa kati ya China na nchi yenye kiwango cha juu cha kutumia nguvu ya maji kwa kuzalisha umeme, hivyo China inapswa kuongeza ufanisi ya kutumia nguvu ya maji.

    Kwa upande mwingine, China ni nchi ya kwanza duniani kwa matumizi yake ya makaa ya mawe, na ni nchi ya pili kwa matumizi ya mafuta na umeme ikiwa nyuma ya Marekani. Hivi sasa, nishati inayotumiwa nchini China karibu zote ni makaa ya mawe na mafuta. Hivyo, kuharakisha uzalishaji wa umeme kwa nguvu ya maji ni chaguo muhimu ya kuboresha mwundo wa nishati ya China, na kutimiza maendeleo endelevu.

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-30