Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-01 21:21:16    
China kuchukua hatua ili kupunguza madhara yanayotokana na matukio ya ghafla kwa watoto

cri
Katika miaka ya hivi karibuni, matukio ya ghafla kwa watoto hutokea mara kwa mara. Hali hiyo inafuatiliwa na watu wa hali mbali mbali za jamii.

Kutokana na maendeleo makubwa ya uchumi na jamii, kiwango cha matibabu na maisha ya wachina kinainuka kwa kiasi kikubwa. Zamani, magonjwa yaliyotishia afya za watoto, kama vile magonjwa ya maambukizi, hali isiyo ya uwiano ya chakula bora yamedhibitiwa kwa mafanikio, lakini madhara ya ghafla kwa watoto yamekuwa ni sababu muhimu inayotishia afya za watoto siku hadi siku. Naibu mkurugenzi wa Idara ya udhibiti wa magonjwa katika wizara ya afya ya China Bibi Feng Yueju anajulisha:

" Hivi sasa nchini China, matukio ya ghafla kwa watoto yanatokea mara kwa mara. Hali hiyo inafuatiliwa na watu wengi wa jamii nchini China. Matukio ya ghafla si kama tu yanaathiri afya za watoto na vijana, bali pia yanaleta hasara na huzuni kubwa kabisa kwa familia."

Takwimu zinaonesha kuwa, matukio ya ghafla yamekuwa chanzo kikubwa cha vifo vya watoto. Zamani, wachina wengi waliona kuwa, matukio ya ghafla ni hali isiyoweza kujulikana kabla ya wakati, hivyo haiwezi kudhibiti. Lakini hivi sasa, watu wanatambua kuwa, kutokana na msaada wa miradi ya usalama, maendeleo ya tiba, matukio ya ghafla yanaweza kuzuiliwa na kudhibitiwa. Hivyo wataalamu wameanza kufanya utafiti na uchuguzi kuhusu madhara yanayotokana na matukio ya ghafla .

Muda si mrefu uliopita, chini ya uungozi mkono wa UNICEF, idara husika za Beijing, mji mkuu wa China zilimaliza uchunguzi kuhusu madhara yanayotokana na matukio ya ghafla . Habari zinasema kuwa, katika mwaka mmoja uliopita, vyanzo vikubwa kwa vifo vya watoto ni ajali za magari na kufa kwa maji, na sababu muhimu zisizosababisha kifo ni kuumia au kuumwa na wanyama.

Kutokana na matokeo ya uchunguzi, Beijing itachukua hatua mbalimbali ili kupunguza madhara yanayoletwa na matukio ya ghafla kwa watoto. Naibu mkuu wa Kamati ya wanawake na watoto ya Beijing Bibi Rong Hua anasema:

" Beiijing imeanza kuchukua hatua za kuzuia kutokea kwa matukio ya ghafla kutokana na matokeo ya uchunguzi. Idara husika 12 zimeanzisha vikundi vya miradi ya kuzuia matukio ya ghafla kwa watoto ."

Katika miaka ya hivi karibuni, Beijing ilifanya shughuli mbalimbali za kueneza elimu za afya na usalama ili kuongeza mwamko kwa watoto, wazazi, walimu na wananchi kuhusu swala la matukio ya ghafla. Bibi Rong Hua alisema kuwa, madhara yanayotokana na matukio ya ghafla kwa watoto yanatokana na sababu mbalimbali, zinazohusiana na watoto, familia, sehemu ya kuishi, shule, mahitaji ya watoto na utengenezaji wa vifaa vya watoto. Kuhusu hali hiyo, Beijing itaanzisha mfumo wa ushirikiano wa idara mbalimbali, kufanya mpango wa utekelezaji wa sera ya kukinga matukio ya ghafla kwa watoto na kutoa uhakikisho wa kisheria kwa watoto.

Bibi Feng Yueju alimwambia mwandishi wa habari kuwa, serikali ya China imeweka kinga ya matukio ya ghafla dhidi ya watoto kuwa lengo na kazi ya muda mrefu. Anasema:

" kazi ya kinga ya matujio ya ghafla kwa watoto imewekwa kwenye , tulifanya utafiti na kazi mbalimbali. Tuna imani kuwa chini ya jitihada ya pamoja, mafanikio makubwa yatapatikana katika kinga ya matukio ya ghafla kwa watoto nchini China."

Ingawa China imefanya kazi kubwa katika kukinga matukio ya ghafla kwa watoto, na mafanikio yamepatikana katika kazi hiyo, lakini kwa kuwa kazi na utafiti husika ulichelewa kuanza, hivyo China inahitaji kujifunza kutoka uzoefu wa nchi za nje. Hivi sasa, China imeimarisha ushirikiano na maingiliano na jumuiya mbalimbali za kinga ya matukio ya ghafla za nchi za nje. Kati ya maingiliano hayo, mafanikio yamepatikana katika ushirikiano wa serikali ya China na UNICEF."

Katika miaka ya hivi karibuni, China na jumuiya mbalimbali za kimataifa zimeanzisha uchunguzi wa matukio ya ghafla kwa watoto ili kupata takwimu za idadi ya watoto walioathirika kutokana na matukio ya ghafla. Mwakilishi wa UNICEF aliyeko Beijing Bw. Christian Voumard anasema:

" uzoefu wa nchi za nje unaonesha kuwa, matukio mengi ya ghafla yanaweza kuzuiliwa. Katika miaka 50 iliyopita, vifo vya watoto kutokana na matukio ya ghafla vilipungua katika nchi za viwanda. Upungufu huo haukutokana na maendeleo ya uchumi , bali sababu muhimu ilikuwa ahadi na jitihada kubwa za pande mbalimbali. UNICEF inapenda kuiunga mkono serikali ya China kufanya utafiti na shughuli za matukio ya ghafla kwa watoto."

Idhaa ya kiswahili 2004-12-01