Ripoti iliyowasilishwa kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan na kikundi cha maofisa waandamizi cha suala la mageuzi ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa, dunia ya hivi sasa imebadilika sana ikilinganishwa na ile wakati Umoja wa Mataifa ulipoanzishwa, matishio makubwa yanayohatarisha amani na usalama wa kimataifa yamekuwa na aina nyingi zaidi, kwa hivyo inapaswa kuwepo kwa dhana mpya ya usalama kwa pamoja.
Ripoti hiyo "dunia yenye usalama zaidi: wajibu wetu wa pamoja" ina sehemu nne, yaani mahitaji ya kukabiliana na matishio kwa pamoja, matishio ya aina 6 yanayoikabili dunia ya hivi sasa, pamoja na uzuiaji wake, usalama wa pamoja na utumiaji wa nguvu na mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo inasema kuwa, lengo muhimu ya kuanzisha Umoja wa Mataifa ili kuwa ni kuzuia balaa kama vile vita vya pili duniani lisitokee tena, lakini hivi sasa matishio yanayoikumba amani na usalama wa kimataifa siyo tu vita miongoni mwa nchi mbalimbali, bali pia aina 5 kubwa za matishio, yaaani umaskini, magonjwa ya kuambukizwa, uharibifu wa mazingira, migogoro ya ndani ya nchi, silaha kali, ugaidi na uhalifu wa makundi ya kimataifa.
Ripoti hiyo inasisitiza kuwa, kutokana na utandawazi wa kiuchumi duniani, matishio hayo hayazuiliwi tena na mipaka ya nchi, nchi moja haina uwezo wa kuzuia matishio hayo kwa juhudi za peke yake. Ili kufanikisha kukabiliana na matishio hayo yenye utatanishi, inapaswa kutegemea utaratibu wenye nguvu na haki wa usalama wa pamoja.
Ripoti hiyo inaona kuwa, kutokana na "katiba ya Umoja wa Mataifa" na utaratibu unaokubalika duniani kuhusu sheria ya kimataifa, kwa tishio la dharura ambayo hakuna utatuzi mingine mzuri, nchi inaweza kutekeleza haki ya kujilinda, na kuchukua hatua kabla ya kushambuliwa. Lakini ikitaka kuchukua "kitendo cha kijeshi cha kujilinda" dhidi ya tishio lisilo la dharura, inapaswa kuliwasilisha suala hilo kwenye Barara la Usalama la Umoja wa Mtaifa. Ama sivyo, kitendo chochote cha kijeshi cha upande mmoja huenda kikavunja utaratibu wa kimataifa wa hivi sasa. Ripoti hiyo inakanusha kurekebisha au kutafsiri upya kifungu cha 51 cha "katiba ya Umoja wa Mtaifa" kinachohusika na haki ya kujilinda.
Ripoti hiyo pia inasema kuwa, kutokana na kifungu cha 7 cha "katiba ya Umoja wa Mataifa", Baraza la Usalama lina uwezo wa kutatua matishio yote ya usalama yanayotatuliwa na nchi mbalimbali, zikiwemo hatari za magaidi, silaha kali na nchi zisizoaminika. Kwa hivyo, hakuna haja ya kuanzisha taasisi mpya itakayochukua nafasi ya Baraza la Usalama, bali inapaswa kuongeza nguvu yake ya kikazi.
Ripoti hiyo inaunga mkono Baraza la Usalama ipewe haki ya kuingilia wa kibinadamu wakati mauaji ya kikabila, uondoaji kabisa wa ukabila na matukio makubwa yanayoikiuka sheria ya kibinadamu ya kimataifa yatakapotokea katika nchi fulani, na ambapo serikali ya nchi hiyo haina uwezo au mataka ya kuchukua hatua kuyazuia matishio hayo. Ripoti hiyo pia inatoa vigezo vitano kuhusu Baraza la Usalama kutumia nguvu ya kijeshi, yaani kiwango cha matishio hayo, lengo la matumizi ya nguvu ya kijeshi, kama matumizi ya nguvu ni njia ya mwisho au la, nguvu ya kijeshi inalingana na matishio yaliyopo au la, na kama matumizi ya nguvu utasababisha matokeo mabaya zaidi au la.
Mwezi Aprili mwaka jana Marekani ilianzisha vita vya Iraq bila ya idhini ya Baraza la Usalama, na kuhatarisha sana hadhi ya Umoja wa Mataifa. Tukio hilo lilimfanya Bw. Annan ateue kikundi cha maofisa waandamizi cha suala la mageuzi ya Umoja wa Mataifa mwezi Novemba mwaka jana, ili kutoa mapendekezo kuhusu masuala yanayoikumba dunia ya hivi sasa ya matishio ya pamoja, njia za kuyakabiliana kwa pamoja na mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Bw. Annan ataiwasilisha ripoti hiyo kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa tarehe 2 mwezi Desemba.
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-01
|