Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-01 16:12:21    
Vipande vya nyama ya kuku vilivyokaangwa pamoja na karanga na pilipili

cri

Mahitaji

    Nyama ya kidari cha kuku gramu 300, karanga iliyokaangwa gramu 15, kitunguu saumu gramu 5, unga wa tangawizi gramu 15, vipande vya vitunguu maji gramu 10, pilipili hoho gramu 5, pilipili gramu 1, sukari gramu 1, mchuzi wa soya gramu 15, chumvi gramu 1, mvinyo wa kupikia gramu 8, maji ya wanga gramu 20, supu ya kuku gramu 25, mafuta yaliyokwisha chemshwa gramu 100.

Njia

1.kausha mafuta yaliyoko kwenye nyama na uondoe manyoya yaliyobaki kwenye nyama ya kuku, ondoa ngozi, kisha ipigepige kwa mgongo wa kisu iwe laini, ikate kuwa vipande vya mraba kwa ukubwa wa sm 2 kila kimoja, na kuviweka kwenye bakuli. Tia chumvi, mchuzi wa soya na maji ya wanga, korogakoroga ili vitu hivyo vichanganyike sawasawa, na kuikata pilipili hoho yenye urefu wa cm 2. tia sukari, siki, mvinyo ya kupikia, mchuzi wa soya, supu ya kuku, wanga wa maji kwenye bakuli moja na kuzikoroga.

2.Pasha moto, gramu 100 za mafuta yaliyokwisha chemshwa hadi yawe na joto la nyuzi 60 hivi, tia pilipili hoho na pilipili mpaka ziwe rangi ya nyekundu-kahawia, tia vipande vya nyama ya kuku, pinduapindua mpaka vigawanyike, kisha tia kitunguu saumu, tangawizi na vitunguu maji na kumimina viungo vilivyochanganyika, kuvitisika na kupinduapindua, halafu tia karanga. Mpaka hapo, kitoweo hiki kina kuwa tayari kupakuliwa.