Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-01 16:29:25    
Kitu Iran inachopata na wasiwasi wake kutokana na azimio jipya

cri

    Baada ya Iran kuelewana na Umoja wa Ulaya, Shirika la Nishati ya Atomiki duniani IAEA juzi lilipitisha azimio jipya kuhusu suala la nyuklia la Iran. Iran si kama tu inaondoa kwa muda wasiwasi wake wa kuliwasilisha suala lake la nyuklia kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, bali pia inaweza kuzihimiza nchi tatu Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kuongeza vitu vinavyoinufaisha Iran katika azimio hilo jipya. Lakini kupitishwa kwa azimio hilo hakumaanishi kuwa suala la nyuklia la Iran limemalizika.

    Kusema kweli, Iran imepata mafanikio katika mazungumzo kati yake na Umoja wa Ulaya. Kwanza, IAEA imepitisha azimio kuamua kuwa haitawasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama. Uamuzi huo umeifanya Marekani ishindwe katika suala hilo. Pili, katika azimio lililofikiwa na nchi tatu mwishoni, limesema kuwa Iran inasimamisha shughuli za uranium nzito "kwa hiari", pia limesema kwamba kitendo hiki cha Iran "sio wajibu wake wa sheria". Hii inaifanya Iran kujitoa kutoka hali isiyoweza kuisaidia.

    Baada ya mswada wa azimio la mwisho ulioandikwa na nchi tatu Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kumalizika, mjumbe wa Iran katika IAEA alisema kuwa azimio hilo ni "azimio lenye maana nzuri kabisa" baada ya suala la nyuklia la Iran kufuatiliwa. Lakini haimaanishi kuwa Iran itakubali azimio hilo kwa hiari, na azimio hilo halilifanya suala la nyuklia la Iran kumalizika wala halizifanyi Marekani na nchi nyingine zibadili misimamo yao.

    Msemaji wa serikali ya Iran alisema kuwa, azimio jipya halikidhi matakwa yote ya Iran, na baadhi ya maneno bado yanaonesha kuwa nchi nyingine haziiamini Iran. Katibu wa kamati kuu ya usalama ya nchi ya Iran jana alisema kuwa, kusimamisha shuguli za uranium nzito ni kitendo cha muda. Alisisitiza kuwa Iran haitaacha shughuli za uranium nzito.

    Maneno hayo yanaonesha kuwa, Iran inakubali azimio hilo kwa shingo upande na bado ina wasiwasi kuhusu utekelezaji wa azimio hilo.

    Kwanza, azimio hilo linazitaka Iran na Umoja wa Ulaya kutekeleza maafikiano yaliyofikiwa kati yao, lakini kwa kiasi fulani, azimio hilo linailenga Iran tu. Ingawa Iran inasisitiza kuwa haitaacha haki yake ya kutumia kiamani nishati ya nyuklia, lakini kufuatana na maafikiano kati yake na Umoja wa Ulaya, Iran imesimamisha shughuli zote za uranium nzito tarehe 22, mwezi uliopita. Lakini Iran sasa haijui kama ahadi zilizotolewa na Umoja wa Ulaya zinaweza kutekelezwa au la.

    Pili, azimio hilo jipya la IAEA haliwezi kuifanya Marekani kubadilisha msimano wake kuhusu suala la nyuklia la Iran. Baada ya IAEA kupitisha azimio hilo, msemaji wa Ikulu ya Marekani Bw. McClelan alisema kuwa, katika mwaka mmoja na nusu uliopita, Iran imevunja ahadi zake mara kwa mara, hivyo wanachama wa Umoja wa Ulaya na IAEA na jumuiya ya kimataifa lazima wakae macho. Alisisitiza kuwa, Iran inapaswa kutimiza ahadi zake, na Marekani itaendelea kuchunguza hali ya Iran ya kutimiza ahadi. Kutokana na maneno ya Bw. McClelan, Marekani bado haijaondoa shaka kwa mpango wa nyuklia wa Iran.

    Tatu, ufahamu na tafsiri za pande husika kuhusu azimio jipya zinatofautiana. Iran inasisitiza kuwa haitaacha shughuli za uranium nzito, lakini mkuu wa IAEA Bw. El Baradei alisema kuwa, hakuna kikomo kwa Iran kusimamisha shughuli za uranium nzito. Jumuiya ya kimataifa inaihimiza Iran kuchukua hatua kubainisha mpango wake wa nyuklia, lakini haiwezi kukidhi ombi la Iran kumaliza suala hilo mapema.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-01