Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-01 21:24:50    
Kukimbia kwa umbali kunachangia kuendelea kwa binadamu

cri

    Katika makala moja iliyochapishwa katika gazeti la "The Nature" la toleo la tarehe 18 Novemba, wanasayansi wa Marekani wamesema kuwa kukimbia kwa umbali mkubwa ni jambo la maana kwa kumwezesha binadamu kusimama wima. Mababu-jadi wa binadamu walikuwa hodari sana katika kukimbia kwa umbali mrefu, na desturi yao ya kukimbia kwa umbali mrefu imeweka alama ya urithi katika miili ya binadamu wa hivi sasa.

    Wanasayansi wa Marekani wanasema kuwa kabla ya miaka milioni mbili iliyopita, wakati mababu-jadi wa binadamu walipoanza kutembea katika mapori ya Afrika wakiwa wima, walianza kukimbia. Hivyo kukimbia kulikuwa alama ya kujiboresha kwa binadamu. Kwanza binadamu wana magoti makubwa na magumu. Pili, miguu ya binadamu ina misuli mingi, ambayo sokwe-mtu hana, binadamu hatumii misuli wakati anapotembea, lakini anaitumia wakati anapokimbia. Binadamu ana misuli mikubwa ya matako, ambayo ni muhimu sana wakati anapokimbia, na inamsaidia binadamu kuwa na uwiano kwenye kiwiliwili chake na kuzuia mwili wake kuangukia mbele. Tatu, binadamu anapokimbia anahitaji mwili wake uburudike, hiyo ndiyo sababu binadamu ana mshipa mkubwa wa jasho na ngozi kubwa isiyo na manyoya.

    Wanasayansi wanasema kuwa binadamu si hodari kwa kukimbia kwa umbali mfupi, bali ni kwa umbali mkubwa. Kwa kuwa mazingira ya maisha kwenye mbuga barani Afrika ni kuwa wanyama wakali wanakula wanyama dhaifu, hali ambayo iliwalazimisha mababu-jadi wa binadamu wakimbie na kunyang'anyana mawindo. Huenda hii ndiyo sababu binadamu wa sasa wanaweza kumaliza mbio za Marathon, lakini wanyama wengine kama manyani au kima hawana uwezo huo.

    

    Wataalamu wanasema kuwa nadharia hiyo inaonesha kuwa uwezo huo unafanya binadamu kuwa tofauti na manyani na kima. Nadharia hiyo, ambayo bado haijakubaliwa na wanasayansi duniani.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-01