Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-01 20:46:44    
China yafanya shughuli za uhamasishaji katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa UKIMWI duniani

cri

    Desemba mosi ni siku ya ugonjwa wa UKIMWI duniani. Kauli mbiu mwaka huu ni "Kuwafuatilia kina mama na kupambana na ugonjwa wa Ukimwi". Aina mbalimbali za shughuli za uhamasishaji zimefanyika katika sehemu mbalimbali nchini China, ili kuwahamasisha wananchi, hasa wanawake kufanya juhudi za pamoja kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa UKIMIWI.

    Katika miaka ya karibuni, idadi ya wanawake wanaoambukizwa UKIMWI imekuwa ikiongezeka kwa kasi. Karibu nusu ya watu wazima walioambukizwa ugonjwa huo kote duniani ni wanawake, uwiano wa kijinsia kati ya wanaume kwa wanawake wagonjwa wa Ukimwi nchini China umeongezeka na kufikia 1.4 kwa 1 mwaka 2003 kutoka 8 kwa 1 ya zamani.