Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-01 21:08:41    
Mikutano ya wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki yafungwa

cri

    Mikutano ya siku mbili ya wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki ilifungwa jana huko Vientiane, mji mkuu wa Laos. Mikutano hiyo imepiga tena hatua kubwa kwa kusukuma mbele maendeleo ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki katika nyanja za siasa, uchumi, na utandawazi wa utamaduni, na kusukuma mbele zaidi ushirikiano kati ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki na nchi za Asia ya mashariki.

   Kwenye mkutano wa 10 wa wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki uliofanyika tarehe 29 Novemba, viongozi waliohudhuria mkutano huo walisaini "Mpango wa utekelezaji wa Vientiane" na "Makubaliano ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki kuhusu nyanja zinazopewa kipaumbele katika mchakato wa utandawazi", nyaraka hizo muhimu zinalenga kusukuma mbele maendeleo ya utandawazi wa kikanda wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki na kupunguza pengo ndani ya umoja huo, ambazo zimekuwa mipango ya utekelezaji ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki ya mwaka 2004 hadi 2010.

    Vyombo vya habari vinaona kuwa, "Mpango wa utekelezaji wa Vientiane" umetoa sera ya uelekezaji mpya kwa Umoja wa Asia ya kusini mashariki katika kukabiliana na changamoto za ugaidi unaoonekana dhahiri katika sehemu hiyo, bei zinazoongezeka za mafuta na maambukizi ya magonjwa. Na "Makubaliano ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki kuhusu nyanja zinazopewa kipaumbele katika mchakato wa utandawazi" yanahakikisha kazi za kutekeleza kihalisi na kuharakisha ujenzi wa sehemu ya biashara huru ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki, pamoja na kujitahidi kujenga soko peke yake la mzunguko huria wa bidhaa, huduma, wataalamu na mitaji na kuharakisha ujenzi wa vituo vya bidhaa ifikapo mwaka 2020.

    Umoja wa Asia ya kusini mashariki unazitaka nchi mbalimbali za umoja huo, nchi zinazofanya mazungumzo moja kwa moja nao na jumuiya ya kimataifa zijitahidi kutoa misaada kwa nchi 4 za Cambodia, Laos, Myanmar na Vietnam ambazo maendeleo ya uchumi wao bado yako nyuma. Nchi hizo nne pia zilifanya mkutano maalum kujadili maendeleo ya nchi hizo ya siku zijazo katika mchakato wa utandawazi, kufanya usawazishaji na ushirikiano wa kusaidiana kwenye msingi wa usawa, kunufaishana na kutoingiliana kati ya mambo ya ndani. Hizo ni hatua za Umoja wa Asia ya kusini mashariki zinazolenga kupunguza pengo la maendeleo ya uchumi ndani ya nchi wanachama.

    Mikutano ya wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki pia ina umuhimu mkubwa katika kuimarisha ushirikiano kati ya umoja huo na nchi za Asia ya mashariki. Tarehe 29 Novemba Umoja wa Asia ya kusini mashariki uliitambua rasmi China kuwa ni nchi yenye mfumo kamili wa uchumi wa soko huria, na kusaini nyaraka muhimu mbalimbali kuhusu ushirikiano wa uchumi na biashara na utaratibu wa kuondoa migogoro. Nyaraka hizo zimeondoa vikwazo kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa sehemu ya biashara huru kati ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki na China. Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki na Korea ya kusini uliofanyika tarehe 30 Novemba pia umeamua kuanzisha mazungumzo kuhusu sehemu ya biashara huru kati ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki na Korea ya kusini. Aidha Umoja wa Asia ya kusini mashariki na Japan pia zitafanya mazungumzo kuhusu kuanzisha uhusiano wa kiuchumi kwenye nyanja zote, na kuamua kukamilisha mazungumzo hayo ndani ya miaka miwili.

   Kwenye mkutano wa wakuu wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki pamoja na China, Japan na Korea ya kusini, wakuu waliohudhuria mkutano huo pia wamekubaliana kufanya mkutano wa wakuu wa Asia ya mashariki wakati utakapofanyika mkutano wa wakuu wa Umoja wa Asia ya mashariki huko Kuala Lumpur, Malaysia mwaka 2005, ili kujadili ushirikiano wa kiuchumi kati ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki na nchi za Asia ya mashariki katika nyanja zote.

    Aidha, wakati wa mikutano hiyo, nchi nyingi zikiwemo Russia, India, Australia na New Zealand zilieleza nia yao ya kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Asia ya kusini mashariki.

    Na nchi mbalimbali pia zilibadilishana maoni kuhusu masuala makubwa duniani kama vile ugaidi, suala la nyuklia la peninsula ya Korea, suala la Iraq, na mchakato wa amani ya mashariki ya kati.

    Wachambuzi wanaona kuwa ushirikiano na maendeleo kati ya nchi za Asia ya mashariki pia utapiga hatua mpya kutokana na maendeleo mapya ya utandawazi wa uchumi wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-02