Tarehe 1 mwezi Desemba bunge la Israel lilizuia mswada wa bajeti uliotolewa na serikali ya Bw. Sharon. Kutokana na sababu hiyo, baadaye Bw. Sharon aliwaondoa madarakani mawaziri 4 wa serikali ya shirikisho la chama tawala-chama cha mageuzi kilichopiga kura ya hapana, na kuuacha shirikisho la chama tawala kukabiliwa na hatari ya kuangushwa.
Matokeo ya bunge la Israel kuhusu mswada huo wa bajeti ni kuwa na kura 69 za hapana na 43 za ndiyo. Mshirika mmoja wa shirikisho la chama tawala cha Bw. Sharon-chama cha mageuzi, kilipiga kura ya hapana, ili kumpinga kutumia Shirk milioni 290, yaani dola za Marekani milioni 65 kwa Umoja wa Biblia wa Uyahudi wenye mrengo wa kulia, kwa kupata uungaji mkono wake kwa mswada huo. Baada ya upigaji kura, Bw. Sharon alitangaza mara moja kuwaondoa madarakani mawaziri 4 ambao ni wanachama wa chama cha mageuzi. Lakini, uamuzi huo utaanza kutekelezwa baada ya saa 48, kwa hivyo Bw. Sharon na chama cha mageuzi bado wana fursa na muda wa kuboresha uhusiano wao. Ikiwa vyama hivyo viwili haviwezi kufikia makubaliano mwishoni, Bw. Sharon atapaswa kufanya juhudi zote kadiri awezavyo, ili kuunda upya baraza la mawaziri, na kuvishawishi vyama vyingine kushiriki kwenye baraza hilo. Sababu ni kuwa, bunge la Israel litapiga kura ya kutokuwa na imani na serikali ya Sharon, ikiwa chama cha mageuzi kitaondolewa kutoka kwenye serikali ya mseto na Sharon hafanikiwi kuunda upya baraza la serikali, serikali ya Sharon yenye viti 40 kati ya 120 bungeni, haitashinda kwenye kura ya kutokuwa na imani na kitalazimika kuangushwa, ijapokuwa vyama vidogo vitaiunga mkono.
Habari zinasema kuwa, kabla ya kupigwa kura, Bw. Sharon alielewa vizuri kuwa mswada huo wa bajeti huenda hautapitishwa, lakini aliamua kujaribu na kuufanya upigwe kura. Vyombo vya habari vinaona kuwa, lengo lake ni kwa ajili ya kuishawishi kamati kuu ya uchaguzi ya chama cha Likud ikubali kuunda serikali ya mseto pamoja na chama cha Labor kwa kutumia mgogoro huo wa kiserikali. Ili kufanikiwa kutekeleza mpango wake wa upande mmoja, Bw. Sharon aliwahi kujaribu mara nyingi kukishawishi chama cha Labor kinachouunga mkono mpango huo, kujiunga na serikali lakini kutokana na kizuizi kutoka kwa kamati kuu ya chama cha Likud, mpango huo bado haujafanikiwa. Ikiwa serikali inakabiliana na hatari ya kuangushwa, chama cha Likud kitakuwa na machaguo mawili tu, yaani kuvishawishi chama cha Labor na vyama vidogo vyenye mrengo wa kulia ili kuunda serikali ya mseto, au kutangaza kufanya uchaguzi mkuu kabla ya wakati uliopangwa.
Lakini kufanya uchaguzi mkuu kabla ya wakati uliopangwa kutakiathiri sana chama cha Likud. Kutokana na hali ya uchaguzi iliyopo ya hivi sasa, uwezekano wa kupata nafasi 40 kilichonazo hivi sasa ni mdogo kabisa, baadhi ya wabunge wa chama hicho wataondolewa kutoka bungeni. Kwa hivyo, watu wengi ndani ya chama hicho wanapinga sana kufanya uchaguzi mkuu. Habari zinasema kuwa, tarehe 30 mwezi Novemba maofisa wa ngazi za juu wa chama cha Labor na chama cha Likud walianza kujadiliana kuhusu uwezekano wa kuunda serikali ya mseto, na kamati kuu ya chama cha Likud itafanya mkutano maalumu wiki ijayo na kufanya majadiliano na chama cha Labor kuhusu mazungumzo ya kuunda baraza la mawaziri.
Lakini uamuzi wa Bw. Sharon kuhusu kukishawishi chama cha Labor kushiriki katika baraza la serikali pia unakabiliana na hatari kubwa. Ingawa wanachama wengi wa chama cha Likud wanapinga kufanya uchaguzi mkuu, lakini vilevile watu wengi kabisa wanapinga chama cha Labor kushiriki katika baraza la mawaziri, miongoni mwao wengi wanapinga pia mpango wa upande mmoja. Ikiwa chama cha Labor kitashiriki katika baraza la serikali, mpango huo utapewa nguvu kubwa ya utekelezaji, lakini ikiwa uchaguzi mkuu unafanyika kabla ya wakati uliopangwa, mpango huo utacheleweshwa kutekelezwa, na hata kuuharibu kabisa. Hayo ndiyo matokeo ambayo baadhi ya wanachama wenye mrengo wa kulia kabisa wa chama cha Likud wanataka kuyaona.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Israel vilieleza vikali kuwa, mfumo wa siasa ya vyama wa Israel umejitumsukiza katika hali ya vurugukubwa, maslahi ya taifa ya Israel pamoja na mustakabali wake umekuwa tena muhanga wa mapambano ya vyama mbalimbali, hayo ni msikitiko mkubwa kwa Israel.
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-02
|