Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-02 21:38:10    
Serikali ya mpito ya Somalia yaundwa

cri

    Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia Bw. Ali mohamed ghedi jana huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya alitangaza orodha ya mawazi wa serikali ya mpito ya Somalia. Baada ya Bw. ghedi kutangaza orodha hiyo, mawaziri 27 waliapisha mara moja. Kuundwa kwa serikali ya mpito ya Somalia kunamaanisha kuwa Somalia imepiga hatua muhimu katika kumaliza hali ya kutokuwa na serikali kwa muda wa miaka 13.

    Habari zinasema kuwa, serikali ya mpito ya Somalia inaundwa na mawaziri 31, manaibu mawaziri 31 na mawaziri 5 wa taifa. Hivi sasa mawaziri wanne wakiwemo mawaziri wa usalama, wa uhamiaji, wa elimu na wa mambo ya ndani bado hawajateuliwa. Kama hali ya usalama ya Mogadishu, mji mkuu wa Somalia itakuwa nzuri, basi serikali ya mpito ya Somalia itarudi Mogadishu kufanya kazi huko hivi karibuni.

    Somalia ilikuwa katika hali ya kutokuwa na serikali kuanzia mwaka 1991. Kuanzia mwezi Oktoba, mwaka 2002, kutokana na usuluhisi wa Jumuiya ya maendeleo kati ya serikali za Afrika Mashariki (IGAD), serikali ya Somalia ilifanya mazungumzo na pande mbalimbali za kisiasa nchini Kenya na kujadiliana kuhusu suala la mchakato wa amani ya Somalia. Kuanzia mwaka huu, mchakato wa amani ya Somalia umepata maendeleo makubwa. Mwezi Februari, pande zote za Somalia ziliafikiana kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba ya mpito. Mwezi Agosti, bunge la mpito la Somalia lilianzishwa rasmi mjini Nairobi, na wabunge 275 waliapishwa. Mwezi Oktoba, bunge la mpito lilimchagua Bw. Abdulahi Yusuf kuwa rais wa muda. Mnamo tarehe 3, mwezi Novemba, Bw. Yusuf alimteua Bw. Ghedi kuwa waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia.

    Serikali mpya ya mpito ya Somalia ni matokeo ya usawazishaji kati ya makabila makubwa ya Somalia na makundi ya kijeshi. Kwanza, bunge la mpito la Somalia lililoundwa mwezi Agusti mwaka huu ni matokeo ya usawazishaji wa pande mbalimbali za Somalia, na hivyo serikali mpya inayoundwa katika msingi huo ndiyo matokeo ya usawazishaji. Katika viti 275 vya bunge, makabila manne makubwa kabisa ya Somalia yamegawana viti 61 kwa mbalimbali, na viti 31 vinavyobaki vinachukuliwa na Umoja wa makabila madogo. Rais wa muda wa Somalia Bw. Yusuf anatoka kabila la Wadarod, ambalo ni moja la makabila manne makubwa kabisa, na waziri mkuu Bw. Ghedi anatoka kabila la Wahawiye, kabila lingine kubwa kabisa.

    Pili, mawaziri wengi ni viongozi wa makundi ya kijeshi. Kati yao, waziri wa biashara na waziri wa ujenzi wa umma walikuwa viongozi wawili wa Mogadishu, na waziri anayeshughulikia mambo ya ukarabati anatoka Kismayu, kituo muhimu cha kusini mwa Somalia.

    Wachambuzi wanasema kuwa, baada ya kuundwa kwa serikali ya mpito, mchakato wa amani ya Somalia bado unakabiliana na changamoto. Kwanza, namna ya kunyang'anya silaha kutoka kwa pande mbalimbali ni suala moja kwa serikali mpya ya Somalia. Baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka mwaka 1991, pande mbalimbali zilitokea nchini Somalia. Hivi sasa pande hizi bado zina silaha nyingi, na migogoro kati ya pande hizo bado inatokea mara kwa mara. Hali hii ni tishio kubwa kwa Somalia kutimiza amani katika siku za usoni. Hivi sasa, rais wa muda wa Somalia Bw. Yusuf ameomba Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kupeleka jeshi la kulinda amani nchini Somalia ili kuisaidia serikali mpya kumaliza kazi ya kuondoa silaha za pande zote na kuunda jeshi jipya la taifa.

    Pili, hali ya Somalia ya kutokuwa na serikali ilikuwepo kwa miaka 13. Baada ya serikali mpya kuundwa, kama serikali hiyo itaweza kuendeshwa bila matatizo, au pande zote za Somalia zitatekeleza kwa uhalisi makubaliano na kukubali kuongozwa na serikali kuu bado haijulikani.

    Aidha, kutokana na kuwepo kwa kukubwa na vita kwa miaka mingi, uchumi wa Somalia hivi sasa umekuwa katika hali ya kusimama, na watu wengi wanaishi katika hali ya umaskini sana. Hayo yote yataathiri vibaya mchakato wa amani ya Somalia.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-02