Ofisa mwandamizi wa ujumbe maalumu ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya demokrasia ya Kongo Bw. M'hand Ladjouzi tarehe 1 alithibitisha kuwa kuwa, jeshi la serikali ya Rwanda limevuka mpaka na kuingia sehemu ya Goma mashariki ya Jamhuri ya demokrasia ya Kongo. Hii ni mara ya kwanza kwa ujumbe maalumu ya Umoja wa Matifa kuthibitisha jeshi la serikali ya Rwanda kuingia Jamhuri ya demokrasia ya Kongo, na kitendo hiki cha jeshi la Rwanda kimesababisha hali ya mpaka wa Jamhuri ya demokrasia ya Kongo na Rwanda kuwa ya wasiwasi tena.
Mgogoro huo wa mpaka kati ya Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo na Rwanda ulianza wiki iliyopita. Wakati huo, rais Paul Kagame wa Rwanda aliashiria mara kwa mara kuwa, kutokana na Jamhuri ya demokrasia ya Kongo kutoweza kulizuia jeshi la upinzani la Rwanda huko kwenye ardhi yake, Rwanda itapeleka jeshi lake nchini Jamhuri ya demokrasia ya Kongo na kulizingira na kuliangamiza jeshi la upinzani la Rwanda. Tarehe 30, mwezi Novemba ofisa wa kijeshi mkoani Kivu alisema kuwa, jeshi la Rwanda tarehe 28 lilikishambulia kijiji kwenye sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya demokrasia ya Kongo, na kuwaua raia 19. Msemaji wa rais wa Jamhuri ya demokrasia ya Kongo Bw.Kudura Kasongo siku hiyo alisema kuwa, Jamhuri ya demokrasia ya Kongo itaongeza askari elfu 10 huko karibu na mpaka yake, ili kujikinga na mashambulizi ya jeshi la upinzani la Rwanda na vitendo vya kuvuka mpaka vya jeshi la Rwanda.
Kutokana na hali hiyo katika mpaka ya Jamhuri ya demokrasia ya Kongo na Rwanda, ofisa wa habari wa ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya demokrasia ya Kongo Bi. Partricia Tome tarehe 1 mwezi huu alisema kuwa, vitendo vya serikali ya Rwanda vinakwenda kinyume na maendeleo ya hali ya siku za karibuni kwenye sehemu ya maziwa makuu ya katikati ya Afrika. Alizitaka Rwanda na Jamhuri ya demokrasia ya Kongo zifuate uamuzi wa azimio la Dar es Salamu lililosainiwa katika mkutano wa viongozi wa sehemu ya maziwa makuu siku 10 zilizopita, na kuhakikisha amani na utulivu kwenye sehemu hiyo. Habari zinasema kuwa, sehemu moja ya kiini cha azimio la Dar es Salamu ni kuibadilisha sehemu ya maziwa makuu kuwa na amani na usalama ya kudumu.
Kati ya mwezi Mei na mwezi June mwaka huu, hali ya mpaka wa Jamhuri ya demokrasia ya Kongo na Rwanda imewahi kuwa ya wasiwasi, na mgogoro huo ulisababishwa na jeshi la upinzani la Rwanda lililosalia nchiini Jamhuri ya demokrasia ya Kongo kuwashambulia mara kwa mara raia ya Rwanda kwenye mpaka. Wakati huo, rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria ambaye alikuwa atashika madaraka ya mwenyekiti wa zumu wa Umoja wa Afrika aliwaalika viongozi wa nchi hizi mbili waende Abuja kutatua mgogoro, na mwishowe walisuluhisha hali ya wasiwasi. Lakini baada ya nusu mwaka, mgogoro umetokea tena kwenye mpaka wa nchi hizi mbili.
Tokea mwaka huu, hatua za kulirejesha jeshi la kigeni lililosalia nchini Jamhuri ya demokrasia ya Kongo zilifanyika haraka iwezekanavyo. Mwezi Agosti, chini ya usuluhishi wa Marekani, Rwanda, Jamhuri ya demokrasia ya Kongo na Uganda zilisaini makubaliano ya kuheshimiana mamlaka ya ardhi, na kutatua kikamilifu suala la jeshi la upinzani la kundi la wahutu la Rwanda kwenye sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya demokrasia ya Kongo. Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, jeshi la serikali ya Jamhuri ya demokrasia ya Kongo na jeshi la ulinzi wa amani la Umoja wa Mataifa yalianza vitendo vya ushirikiano mkoani Kivu kwenye mpaka wa mashariki ya Jamhuri ya demokrasia ya Kongo na kulishawishi jeshi la upinzani la Rwanda kurudi nchini kwao. Serikali ya mpito ya Jamhuri ya demokrasia ya Kongo ilitunga mpango wa kurejesha jeshi la kigeni kwa hatua mbili, yaani kurejesha kwa hiari na kwa nguvu za silaha. Lakini mpango huo unatekelezwa pole pole.
Wachambuzi wanaona kuwa, mgogoro wa mpaka wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Rwanda umesababishwa na manung'uniko ya muda mrefu na hali ya kutoaminiana, nchi hizo mbili zikitaka kuondoa mgogoro huo, zinapaswa kufanya mazungumzo na mashauriano. Kitendo chochote kinachotaka kutatua suala hilo kwa nguvu za silaha kitaharibu hali ya usalama ya sehemu hiyo.
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-02
|