Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-02 20:29:22    
Nani anaweza kuchukua nafasi ya Alan Greenspan ?

cri

    Pamoja na kuharakishwa kwa uundaji wa kundi la maofisa wanaoshughulikia mambo ya uchumi katika awamu ya pili ya rais Bush wa Marekani, maofisa wa idara mbalimbali za kiuchumi za serikali ya Marekani wameanza kufahamika siku hadi siku, na cheo kimoja muhimu kinachofuatiliwa na watu ni kiti cha mwenyekiti wa kamati ya akiba ya fedha ya serikali kuu ya Marekani. Kutokana na kuwa mwenyekiti wa sasa Bw. Alan Greenspan amekuwa na wazo la kujiuzulu, hivyo ingawa kipindi cha kazi zake bado kina miezi 14, lakini uteuzi wa mtu atakayechukua nafasi yake sasa hivi unazungumziwa sana. Watu wa sekta mbalimbali nchini Marekani na hata duniani wanafuatilia kama mwenyekiti mpya wa kamati ya akiba ya fedha ya serikali kuu ya Marekani ataweza kufanya kazi kama alivyokuwa Bw. Greenspan.

    Bw. Greenspan aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya akiba ya fedha mwaka 1987, na ameshika wadhifa huo kwa vipindi vinne mfululizo, katika vipindi vya madaraka yake vya miaka 18 alianzisha "Enzi ya Greenspan" ya uchumi wa Marekani. Siku zote Bw. Greenspan alifuatilia mfumuko wa bei ya bidhaa nchini Marekani, kila mara uchumi wa taifa unapokuwa na ongezeko kubwa la kupita kiasi, yeye alikuwa anatoa onyo na kupunguza maendeleo ya uchumi, na kwa upande mwingine kila mara uchumi ulipoanza kuzorota, alikuwa anawapa imani wawekezaji. Hivyo amesifiwa na watu kuwa ni mwenyekiti wa kamati ya akiba ya fedha aliyeshika madaraka hayo kwa miaka mingi zaidi na kuweza kuzuia ipasavyo mfumuko wa bei za bidhaa na kudumisha ongezeko la uchumi wa Marekani.

    Ili kudhibiti mfumuko wa bei ya bidhaa mwaka 1988, kamati ya akiba ya fedha ya Marekani ilishikilia kuongeza faida ya mikopo iliyotolewa na kubana matumizi. Toka mwaka 1990 hadi mwaka 1991 wakati uchumi wa Marekani ulipokuwa na dalili ya kuzorota, Bw. Greenspan kwa upande mmoja alipunguza utoaji wa mikopo na kuinua faida ya akiba ya mitaji ya benki, kwa upande mwingine aliingiza mitaji mingi masokoni ili kufufua uchumi na kuimarisha imani ya sekta ya mambo ya fedha. Katika kipindi hicho, alijitahidi kupunguza shinikizo lililoletwa na ongezeko la uchumi kwa njia ya kuongeza faida na kutoa kipaumbele kwa kutuliza bei ya bidhaa, hatimaye uchumi wa Marekani ukaanza kukua katika hali nzuri. Baada ya hapo Bw. Greenspan alikuwa hodari sana katika kukabiliana na migogoro mingi ya dharura ukiwemo mgogoro wa mambo ya fedha uliotokea nchini Mexico, kupanda kwa mfululizo kwa thamani ya vyeti vya hisa nchini Marekani na mgogoro wa mambo ya fedha uliotokea barani Asia.

    Baada ya kutokea tukio la "tarehe 11 Septemba" ingawa kwa ujumla uchumi wa Marekani unaendelea kukua, lakini matukio mengi yaliyotokea nchini Marekani yakiwemo "Kuvunjika kwa povu jipya la uchumi", "Tukio la tarehe 11 Septemba", kashfa ya kampuni ya Enron", mapambano dhidi ya ugaidi na vita vya Iraq yamekuwa pigo kwa uchumi wa Marekani, vilevile yameathiri uchumi wa dunia nzima kwa ujumla. Kutokana na kukabiliwa na hali ya namna hiyo, Bw. Greenspan anapunguza hatua kwa hatua faida ya akiba ya fedha za wakazi zilizowekwa katika benki, ambayo imefikia kiwango cha chini kabisa katika miaka 46 iliyopita. Hatua hizo zimechangamsha sana uchumi wa Marekani, ufanisi wa uzalishaji mali unakuzwa upya na hali nzuri imeonekana katika soko la hisa. Baada ya kupitia kipindi cha kuzorota kwa uchumi, ambacho kinachukuliwa na watu kuwa ni kipindi kibaya kabisa wa uvuguvugu kabisa katika historia ya Marekani. Mwezi Juni mwaka huu Bw. Greenspan aliona kuwa uchumi wa Marekani umepata nguvu mpya, hivyo kamati ya akiba ya fedha ya Marekani iliacha utekelezaji wa sera za kutoa faida ndogo kwa akiba ya fedha za wakazi zilizowekwa katika benki, kinyume chake ikatumia sera za kuongeza faida kwa fedha zilizowekwa katika benki, na kuweka kiasi cha faida katika kiwango cha kutochangamsha maendeleo ya uchumi wala kuyazuia.

    Kutokana na hali hiyo, baadhi ya watu wanamsifu Bw. Greenspan kuwa ni mtu anayeweza kuathiri hali ya uchumi wa Marekani akimfuatia rais wa Marekani. Hivyo, uteuzi wa mwenyekiti mpya wa kamati hiyo ni suala kubwa linalofuatiliwa nchini Marekani hata duniani.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-02