Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-02 21:06:14    
New York-Kofi Annan azitaka kampuni kuchangia zaidi kinga na tiba ya ugonjwa wa UKIMWI

cri
    Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw. Kofi Annan jana aliposhiriki kwenye harakati iliyofanywa na idara za fedha katika Wallstreet, New York kwa ajili ya kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani aliwataka viongozi wa kampuni kuchangia zaidi kuzuia kuenea kwa UKIMWI duniani.

    Bw. Kofi Annan aliainisha kuwa idara za kampuni na fedha zinaweza kulichangia fedha shirika la fedha la kupambana na UKIMWI la umoja wa mataifa au kushirikiana na miundo husika ya umoja wa mataifa kuwa wenzi katika harakati za kukinga na kutibu UKIMWI duniani.