Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-03 19:26:11    
Ujumbe wa biashara wa mkoa wa Guangdong wa China kuanzisha shughuli barani Afrika

cri

                    

    Guangdong mkoa ulioko kusini mwa China, ni mkoa ulioendelea zaidi nchini China, na umepata maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi katika miaka kadhaa iliyopita. Katika Miaka ya hivi karibuni, serikali ya mkoa wa Guangdong imetunga sera ya kiuchumi ya kwenda nje, na kuhimiza wanaviwanda na wafanyabiashara wa mkoa wa Guangdong waende nchi za nje kuanzisha shughuli zao. Ili kutekelza sera hiyo, serikali ya mkoa wa Guangdong ilipeleka ujumbe wa kiuchumi na kibiashara kwenye nchi za nje. Mwaka jana, ujumbe wa wajumbe wa kampuni 35 za mkoa wa Guangdong ulitembelea nchi za Amerika ya Kusini chini ya uongozi wa katibu mkuu wa kamati ya serikali ya mkoa huo Bw. Zhang dejiang, na thamani ya mikataba iliyosainiwa kati ya ujumbe huo na nchi hizo ilifikia dola za kimarekani bilioni moja.

    Safari hii, serikali ya Guangdong imetuma ujumbe mkubwa zaidi ulioongozwa na Bw. Zhangdejiang kwenda kwenye nchi za Afrika. Ujumbe huo ulitembelea nchi tatu za Afrika, zikiwemo Afrika Kusini, Misri na Algeria. Katika ziara hiyo, ujumbe huo uliokuwa na wanaviwanda zaidi ya 80 ulifanya mikutano mbalimbali kuhusu uwekezaji vitega uchumi, biashara na miradi ya ujenzi. Wajumbe hao walibadilishana maoni na watu wa hali mbalimbali wa kiserikali, viwanda na wafanyabiashara katika nchi hizo za Afrika, na walisaini mikataba yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2 na milioni 430. Naibu mkuu wa mkoa wa Guangdong Bw. Tang Binquan alieleza kuwa, ziara hiyo ilipata mafanikio makubwa ambayo yameletwa na ushirikiano mzuri kati ya serikali na watu wa China na Afrika.

    Wanaviwanda wengi wanaona kuwa, hivi sasa sera ya kiuchumi ya kwenda nje ya mkoa wa Guangdong inatekelezwa vizuri, hali ambayo inawavutia wajumbe wengi wa idara za uchumi na biashara kushiriki.

    Ujumbe huo ulishirikisha kampuni 62 za mkoa wa Guangdong, zikiwemo kampuni 26 za kitaifa, 20 binafsi na 16 za kihisa. Katika ziara yake barani Afrika, ujumbe huo ulifanya mikutano mikubwa mitatu inayohusika, ukiwemo Mkutano wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Guangdong na Afrika Kusini uliofanyika huko Johannesburg, Mkutano wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Guangdong na Misri uliofanyika huko Cairo, na Mkutano wa maelezo kuhusu hali ya uwekezaji vitega uchumi nchini Algeria uliofanyika huko Algiers. Mikutano hiyo iliwashirikisha watu zaidi ya 1300 wa hali mbalimbali katika nchi hizo tatu, wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara na wanaviwanda. Katika mikutano hiyo, pande mbili za Guangdong, China na nchi za Afrika zilisaini mikataba yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2 milioni 430. Kati ya hiyo, mikataba ya kibiashara ina thamani ya dola za kimarekani bilioni 1 na milioni 240, zikiwemo uuzaji wa bidhaa nje za dola milioni 640 na bidhaa zilizoagizwa kutoka nchi za nje dola za kimarekani milioni 600; mikataba 11 ya uwekezaji vitega uchumi yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 110, na mikataba 16 kuhusu miradi ya ujenzi yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1 na milioni 8.

    Kampuni maarufu ya binafsi inayotengeneza viyoyozi ya Zhigao ya Guangdong ilishiriki kwenye ujumbe wa mwaka jana uliotembelea Amerika ya Kusini. Katika ziara yake hiyo barani Afrika, kampuni hiyo ilipata matokeo makubwa, si kama tu ilisaini mkataba na Misri juu ya kuiuzia nchi hiyo bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 10, bali pia itatoa dola za kimarekani milioni 28 kuanzisha viwanda vya kutengenezea viyoyozi nchini Nigeria na Botswana. Kampuni ya Zhongyu ya Guangdong ni kampuni maarufu inayotengeneza pikipiki. Katika ziara barani Afrika, kampuni hiyo imeamua kutumia dola za kimarekani milioni 11 laki 5 na elfu 85, ili kuanzisha kiwanda cha kutengeneza pikipiki kwa kushirikiana na Algeria. Mbali na hayo, kampuni maarufu ya kitaifa ya upashanaji habari ya Zhongxing itatumia dola za kimarekani milioni 30, kushirikiana na Algeria na kuanzisha shughuli nchini humo.

    Kuhusu mikataba ya ujenzi barani Afrika, mikataba iliyosainiwa katika ziara hiyo ni mingi zaidi, ikilinganishwa na ya zamani. Kampuni ya Upashanaji Habari ya Zhongxing ilipata miradi yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 220 nchini Angola, Misri na Algeria, wakati kampuni nyingine maarufu ya upashanaji habari ya Guangdong ya Huawei ilipata mradi wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 116 nchini Misri na Algeria. Mbali na hayo Kampuni ya Huazheng ya viumbe ya Guangdong ilisaini mkataba na Misri wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 480 wa kutengeneza sukari na malori makubwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-03