Tarehe 5 Misri ilimwachia huru jasusi mashuhuri wa Israeli Azam Azam, kwa kutimiza masharti ya kubadilishana wafungwa, siku hiyo serikali ya Israeli pia iliwaachia huru wanafunzi 6 walioshikwa wa Misri. Wachamabuzi wanaona kuwa tukio la jasusi Azam linaonesha uhusiano wa Misri na Israeli. Ofisa mmoja wa Misri ambaye anataka jina lake lihifadhiwe, alidokeza kuwa hakuna sharti lolote kwa Azam kuachiliwa huru, hakukuweko "biashara yoyote" au kuhusiana na kuachiwa huru kwa wanafunzi 6 wa Misri.
Lakini wachambuzi wanaona kuwa kuachiwa huru kwa Azam kunahusika na waziri wa mambo ya nje Bw. Ahmed Aboul Gheit na waziri wa upelelezi Bw. Omar Suleiman wa Misri ambao walifanya ziara nchini Israel tarehe 1 mwezi huu. Katika ziara hiyo nchi mbili za Misri na Israel ziliafikiana kuhusu masuala mengi ya uhusiano katika pande hizo mbili, likiwemo la kumwachia huru Azam na Misri kupeleka askari 750 kwa sehemu ya Gaza. Kabla ya ziara hiyo, wabunge la unge la taifa la Misri walipitisha uamuzi wa kuandika barua kwa wizara ya mambo ya nje wakitaka Bw. Gheit kuishinikiza Israel na kujaribu kuwawezesha wananfunzi 6 wa Misri walioshikwa na upande wa Israel waweze kurudi nchini pamoja nao katika ndege moja. Licha ya hayo, barua hiyo imelaumu idara ya polisi ya Israel kuwashika wanafunzi wa Misri ni kutokana na kulipiza kisasi kwa Azam kushikwa na upande wa Misri.
Azam ana umri wa miaka 49 mwaka huu, yeye ni mpalastina mwenye uraia wa Israel na ni mwanakivwnada, kabla ya kukamatwa alifanya kazi katika kiwanda cha nguo kilichowekezwa na Israel nchini Misri. Mwaka 1997 alikamatwa na polisi wa Misri na katika mwaka huo huo alishitakiwa kwa kosa la kukusanya habari muhimu kwa ajili ya idara ya upelelezi ya Isral, na alihukumiwa kifungo cha miaka 15 pamoja na kazi za sulubu. Wanafunzi 6 wa Misri waliokamatwa na polisi ya Israeli tarehe 13 mwezi uliopita, kwa makosa kuingia Israeli kiharamu wakiwa na lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Katika miaka 8 iliyopita tangu Azam kutiwa gerezani, Israel ilichukulia tukio hilo ni jambo kubwa la uhusiano kati ya pande hizo mbili, ambalo lilizungumzwa karibu katika kila mkutano wa ngazi ya juu wa pande mbili za Misri na Israel, na maofisa wengi wa ngazi ya juu na wabunge wa Isral walikwenda gerezani kumwamgalia Azam. Mbali na hayo, rais wa zamani wa Marekani BW. Bill Clinton na rais Geoge Bush wa sasa, mwenyekiti wa zamani marehemu Yassa Arafat, mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya chama cha ukombozi wa Palastina Abas pamoja na wanasiasa muhimu wa nchi za magharibi walikuwa wasuluhishi wakijaribu kufanikisha mpango wa kumbadilisha Azam kwa sharti la kuwaachia huru wapasltina na wanamgambo wa chama cha Hizgullah cha Lebanon waliofungwa na Israel, lakini rais Mubarak wa Misri alishikilia kusema kuwa kumwachia huru Azam au la kunahusiana na haki ya sheria ya Misri, hivyo si vizuri kwa serikali kuingilia suala hilo.
Wachambuzi wanaona kuwa kuachiliwa huru kwa Azam hakuwezi kubadilishwa kwa sharti la kuwaachia huru wanafunzi 6 wa Misri, ambao bado hawajahukumiwa. Hali halisi ni kuwa uhusiano uliokuwa mbaya kabisa, hivi sasa unaanza kuboreshwa, na kwamba Misri inajitahidi kuonesha umuhimu wake katika mchakato wa amani ya mashariki ya kati baada ya enzi ya Yassa Arafat.
Baada ya Bw. Yassa Arafat kufariki dunia, jumuia ya kimataifa inatarajia sana Palastina Israel zihimize mchakato wa amani ya mashariki ya kati kwa kutumia nafasi ya jumuia ya kimataifa kulifuatilia suala la Palastina. Marekani, Israel na Umoja wa Ulaya zinaona kuwa kufariki kwa Arafat ni "nafasi nzuri" kwa uhimizaji wa mchakato wa amani ya mashariki ya kati. Hivyo, katika wakati wa kutokea mabadiliko makubwa katika hali ya mashariki ya kati, Misri inataka kurekebisha sera zake za kidiplomasia, kuondoa vikwazo katika uhusiano wa pande mbili za Misri na Israel ili kuonesha umuhimu wake zaidi katika mchakato wa amani ya mashariki ya kati.
Idhaa ya kiswahili 2004-12-06
|