Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-07 15:01:45    
Mkutano wa wakuu kuhusu familia duniani wajadili maendeleo ya uwiano ya familia na jamii

cri

    "Familia ni ishara ya heri na baraka mithili ya jua la Sanya". Mkurugenzi wa Kamati ya taifa ya idadi ya watu na uzazi wa mpango Bwana Zhang Weiqing aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano wa wakuu kuhusu familia duniani mwaka 2004. Wajumbe zaidi ya 300 kutoka nchi na sehemu mbalimbali duniani tarehe 6 walikusanyika huko Sanya mkoani Hainan kwenye mandhari ya kupendeza, wakijadili maendeleo ya uwiano ya familia na jamii.

    Saa 3 asubuhi ya jana, wajumbe wa nchi mbalimbali walikaribishwa kwenye mkutano huo. Watoto chipukizi 56 waliovaa nguo tofauti za makabila 56 ya China waliwapa maua kwa heshima, mkutano huo ulifunguliwa katika hali motomoto na ya kirafiki.

    Naibu spika wa Halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China ambaye pia ni mwenyekiti wa Shirikisho kuu la kina mama la China Bibi Gu Shoulian, alihudhuria ufunguzi wa mkutano huo na kutoa hotuba. Alisema kuwa, China ni nchi inayoendelea yenye idadi kubwa ya watu zaidi na familia nyingi zaidi kuliko nchi nyingine duniani. Taifa la China lina mila nzuri ya jadi ya kuzingatia zaidi familia, kuheshimu wazee na kuwatunza watoto. Serikali ya China imeweka sera na miradi kuhusu familia kwenye mikakati ya maendeleo ya nchi, kuchukua hatua na vitendo halisi kulinda familia na kusukuma mbele maendeleo mazuri ya familia.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Kofi Annan ameutumia salamu mkutano huo akidhihirisha kuwa, familia ni shina la kimsingi kabisa lililo na maendeleo endelevu katika jamii. Familia mbalimbali zinafanya kazi muhimu sana katika mchakato wa kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa .Bwana Annan anaona kuwa, malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa yaliyosainiwa na nchi mbalimbali duniani, ni malengo makubwa kwa ajili ya kujenga siku nzuri zaidi za karne ya 21.

    Ajenda kuu ya Mkutano huo wa wakuu kuhusu familia duniani ni "Familia na malengo ya maendeleo ya milenia", mkutano huo unalenga kujumuisha mafanikio yaliyopatikana katika miaka 10 iliyopita tangu kuanzishwa kwa mwaka wa familia duniani, kubadilishana maoni kuhusu "Mpango wa utekelezaji wa mkutano wa kimataifa wa idadi ya watu na maendeleo uliofanyika Cairo" na uzoefu wa kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa, kuongeza maelewano na maoni ya pamoja kuhusu malengo ya mwaka wa familia duniani na masuala ya familia, na kujadili changamoto na sera zinazozikabili familia za siku za usoni, ili kuzihamasisha familia mbalimbali duniani zifanye juhudi kwa pamoja ili kufikia lengo la urafiki, maafikiano, usawa na maendeleo ya pamoja.

    Malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa uliothibitishwa mwaka 2000 yalithibitisha kupunguza kwa nusu idadi ya watu maskini kabisa kabla ya mwaka 2015, kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, kuimarisha afya za kina mama na watoto, kueneza elimu ya kimsingi, kusukuma mbele usawa wa kijinsia, na kuzuia hali ya mazingira isizidi kuwa mbaya. Malengo hayo yameelekeza mwelekeo kwa maendeleo ya familia duniani.

    Katika wakati wa mkutano huo, wajumbe wa nchi mbalimbali watafanya majadiliano kuhusu uhusiano kati ya familia na maendeleo endelevu, kuondoa umaskini, kutoa elimu, usawa wa kijinsia, afya ya uzazi na usalama wa mama wazazi, kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi, mazingira na utandawazi wa upashanaji habari.

    Mwenyekiti wa Shirika la familia duniani Doktor Kusazho alitoa matumaini kuwa mkutano huo utatoa mchango katika kuimarisha ujenzi wa uwezo mbalimbali wa familia, kuhamasisha familia mbalimbali kufanya juhudi kwa kujenga jamii nzuri zaidi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-07