Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-07 21:28:19    
Hali ya Ukraine bado inavutia ufuatiliaji wa kimataifa

cri

    Ili kusukuma mbele utatuzi wa mgogoro wa kisiasa uliosababishwa na uchaguzi mkuu nchini Ukraine, katibu mkuu wa shirikisho la usalama na ushirikiano la Ulaya Bwana Jan Kubis jana alasiri alifunga safari kuelekea Ukraine kufanya usuluhisho. Wakati huo huo, shughuli za upinzani za kiraia zinaendelea mitaani mwa Kiev, mji mkuu wa Ukraine, nguvu mbili za kisiasa zilizoongozwa na waziri mkuu wa sasa Bwana Viktor Yanukovych na kiongozi wa upinzani Bwana Viktor Yushchenko zinaendelea kupambana ili kupata ushindi katika duru la pili la upigaji kura unaotarajia kufanywa tarehe 26 mwezi huu.

Chini ya upinzani mkali wa vyama vya upinzani na shinikizo kubwa kutoka nchi za magharibi, mahakama kuu ya Ukraine tarehe 3 mwezi huu ilitoa hukumu ya mwisho, na kubatilisha matokeo ya upigaji kura uliofanyika tarehe 21 Novemba, na thibitisha kufanya upigaji kura tena tarehe 26 mwezi huu, hukumu hiyo imeielekeza hali ya Ukraine kumpendelea zaidi kiongozi wa upinzani.

Lakini hukumu hiyo ya mahakama kuu na kurudi nyuma kwa chama tawala haikuwafanya wapinzani kulegeza madai yake. Mgombea wa upinzani Bw. Yushchenko alisema kuwa, vyama vya upinzani vilidai kusambaratisha mara moja serikali ya Yanukovych na kamati kuu ya uchaguzi mkuu. Pia aliwataka wafuasi wake wasiache shughuli za upinzani. Wachunguzi wameeleza kuwa, nia ya Yushchenko ni kujaribu kuvunja serikali ya Yanukovych, na kumshurutisha ajiuzulu ili kuhakikishia ushindi wake katika upigaji kura wa duru jipya.

Kutokana na upinzani mkali na kuimarika kwa uguvu za uingiliaji kati kutoka nje, serikali ya Yanukovych imekumbwa na hali ya wasi wasi sana. Rais Leonid Kuchma jana alimlaani wazi Yushchenko kwa kuvunja mapatano yaliyoafikiwa kwa kufanya mazungumzo ya pande nyingi ya kimataifa, kuchochea na kuzidisha msukosuko wa hali ya nchi hiyo. Alisisitiza kuwa, waandamanaji hawawezi kuwakilisha raia wote milioni 48 wa Ukraine, pia alieleza kuwa, uingiliaji kati wa nguvu za nje umechafua zaidi hali ya kisiasa ya Ukraine.

Chama tawala cha Ukraine pia kinafanya matayarisho ya mwisho. Habari zinasema kuwa, rais Kuchma ametoa mswada wa kupunguza madaraka ya rais na kuongeza madaraka ya bunge, na kuukabidhi upitishwe kwenye mkutano maalum wa bunge utakaofanyika tarehe 7, mswada huo unakusudia kudhoofisha madaraka ya rais ili kuweka kizuizi fulani kwa vyama vya upinzani.

Kutokana na kukaribia kwa tarehe ya upigaji kura, maendeleo ya hali ya Ukraine bado ina mambo kadhaa yanayoyumbayumba.

Kwanza, bado haijulikani kama vyama vya upinzani vinaweza au la kumshurutisha Yanukovych kujiuzulu na kuunda upya kamati kuu ya uchaguzi mkuu kutokana na matakwa yao, ili kuondoa vipingamizi vya kuushinda uchaguzi mkuu. Kutokana na sheria ya Ukraine, ni rais peke yake ana haki ya kusambaratisha serikali.

Pili. Chama tawala kitachukua hatua gani kukabiliana na changamoto zilizozushwa na wapinzani. Rais Kuchma jana aliwahi kusema kuwa, Yanukovych angeacha kujiunga na uchaguzi mkuu, inamaanisha kuwa, huenda Kuchma ataacha kumunga mkono Yanukovych.

Isitoshe, msimamo wa wapiga kura pia ni sababu muhimu ya kuamua matokeo ya mapambano kati ya vikundi hivyo viwili. Japokuwa hivi sasa nguvu ya Yushchenko inatia fora, lakini waungaji mkono wa Yanukovych hawataacha jitihada zao.

Jambo lingefuatiliwa ni msimamo wa Russia. Mwishoni mwa mwezi uliopita, rais Putin wa Russia alitangulia kumpelekea Yanukovych simu ya hongera, lakini baada ya mahakama kuu ya Ukraine kutoa hukumu ya mwisho, rais Putin aliyefanya ziara nchini Uturuki alisema kuwa, Russia inapenda kushirikiana na rais mteule yeyote wa Ukraine.