Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-07 20:53:09    
Sera mpya za utulivu za mambo ya fedha zitatangazwa mwakani

cri

   Sera za mambo ya fedha zilizotekelezwa karibu miaka 7 iliyopita zitabadilishwa kwa sera mpya za utulivu. Mkutano wa idara ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China uliofanyika tarehe 1 ulisema, "kutokana na mabadiliko ya hali ya uchumi wa taifa na matakwa ya kuimarisha mafanikio yaliyopatikana katika kurekebisha maendeleo ya uchumi wa taifa kwa udhibiti wa mpango wa serikali kuu, sera mpya za utulivu kuhusu mambo ya fedha zitatekelezwa kuanzia mwaka kesho.

    Sera za mambo ya fedha ni kimoja cha vyombo vinavyotumiwa na serikali kudhibiti uendeshaji wa uchumi wa taifa. Wakati uchumi uko katika hali ya kurudi chini, serikali inajitahidi kuhimiza ongezeko la uchumi kwa kuongeza matumizi ya fedha; lakini baada ya uchumi kuzinduliwa, matumizi ya fedha ya serikali yanatakiwa kupunguzwa. Hivi sasa sera za mambo ya fedha za China zinazoelekezwa kwenye utulivu, zinatokana na kufuatana na mabadiliko hayo.

   Ingawa sera zinazotumika hivi sasa zitaachwa mara moja, lakini zimetoa mchango mkubwa. Toka mwaka 1998 China ilipoanza kutekeleza sera za kuhimiza maendeleo makubwa ya kiuchumi, China ilitoa vyeti vyenye thamani vya dhamana ya serikali vya muda mrefu vyenye thamani ya Yuan za Renminbi bilioni 910, ambavyo vilihamasisha mahitaji ya nchi na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa taifa.

    Umaalumu wa sera ya kuhamasisha ongezeko kubwa la uchumi ni kuhimiza maendeleo ya uchumi wa taifa kwa kutoa vyeti vingi vyenye thamani vya dhamana ya serikali na kuwa na pengo kubwa katika mambo ya fedha ya taifa. Lakini hatua hiyo ni rahisi kusababisha mgogoro wa mambo ya fedha endapo pengo hilo halitazibwa kwa muda mrefu. Toka mwaka 2002, pengo la mambo ya fedha ya China lilikuwa zaidi ya Yuan bilioni 300, kiasi ambacho ni cha juu kabisa tangu China mpya kuasisiwa. Kwa miaka mitatu mfululizo uwiano wa pengo la mambo ya uchumi ulifikia asilimia 3, ambao umekaribia kiwango cha tahadhari kinachothibitishwa na nchi nyingi duniani.

    Sera za kuhamasisha ongezeko kubwa la uchumi zinatumika katika hali maalumu, kwa kuangalia kipindi kirefu na wastani mambo ya fedha ya nchi yanatakiwa kufuata kanuni za kulingana kati ya mapato na matumizi na kupunguza pengo la mambo ya fedha hatua kwa hatua. Hata hivyo kuna mashirika na wataalamu wengi wanajadiliana sana kuhusu namna ya kuacha kwa taratibu utekelezaji wa sera za kuhamasisha ongezeko kubwa la uchumi.

    Ukweli ni kwamba katika miaka miwili ya karibuni, serikali ilipobuni bajeti ya matumizi ya fedha, ilianza kuchukua baadhi ya hatua za kudhibiti ongezeko kubwa la uchumi. Toka mwaka 2003 China ilianza kupunguza vyeti vyenye thamani vya dhamana ya serikali, ambavyo ilikuwa ni pungufu Yuan bilioni 10 kuliko mwaka 2002, na vilikuwa pungufu Yuan bilioni 30 katika mwaka 2004.

    Kubadilisha sera za kuhimiza ongezeko kubwa la uchumi kuwa za utulivu kunatokana na hali halisi ilivyo. Katika miaka ya karibuni uwekezaji nchini uliongezeka kwa haraka sana, hususan kutoka mwaka 2003 uwekezaji wa sekta ya mali zisizohamishika ulikuwa na ongezeko kubwa kwa mfululizo, ambapo pato la China liliongezeka pia kwa mfululizo. Imekadiriwa kuwa pato la China kwa mwaka litakuwa ni zaidi ya Yuan bilioni 500. Mabadiliko hayo yameweka mazingira mwafaka ya kuacha utekelezaji wa sera za kuhamasisha ongezeko kubwa la uchumi.

     Kuanza kutekeleza sera za mambo ya fedha za utulivu kunamaanisha China kupiga hatua moja muhimu katika kurekebisha uchumi wa taifa. Sera za mambo ya fedha za utulivu zinamaanisha kuwa siyo sera za kupanua wala kupunguza peke yake, bali ni kutumia sera za aina mbili kuendana na hali halisi na kudumisha uwiano kwa jumla. Kitu kinachofuatiliwa zaidi na watu ni kuwa katika mwaka kesho sera za mambo ya fedha za kuhamasisha ongezeko kubwa la uchumi na sera za sarafu za utulivu zitatumika kwa pamoja kwa mara ya kwanza nchini China. Hatua hiyo itahimiza maendeleo ya uchumi yenye utulivu.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-07