Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-08 17:50:02    
Teknolojia ya kuotesha mbegu za mpunga chotara ya China yachukua nafasi ya mbele duniani

cri

Bw. Yuan Longping Baba wa mpunga chotara

Mpunga ni zao muhimu la chakula nchini China na katika nchi za Asia pia. Umoja wa mataifa umetaja mwaka 2004 kuwa ni "mwaka wa mpunga duniani".

Ofisa wa kamati ya maandalizi alisema kuwa lengo la maonesho ya safari hii ni kuhimiza maendeleo ya teknolojia ya kuotesha mbegu za mpunga chotara duniani, maendeleo ya kilimo cha zao la mpunga pamoja na upashanaji habari na ushirikiano wa teknolojia husika. Utafiti na matumizi ya teknolojia ya mpunga chotara ya China yamekuwa yakichukua nafasi ya mbele duniani, na China imetoa mchango mkubwa katika kutoa dhamana ya chakula. Mchele ni chakula kikuu kwa watu kiasi cha bilioni 3 wa duniani kwa hivi sasa.

Mkutano wa safari hii utawaalika viongozi wa sekta ya mpunga wa chotara, wataalamu wa taasisi za utafiti wa sayansi, wasimamizi wa uenezaji wa teknolojia ya kilimo, wafanya biashara wa sekta ya mbegu pamoja na wawakilishi wa baadhi ya mashirika ya nchi za nje.

Chakula ni kitu muhimu cha kwanza kwa binadamu, na mpunga ni chakula muhimu zaidi kuliko vyakula vya aina nyingine. Serikali ya China inazingatia sana suala la usalama wa chakula, siku zote inajitahidi kuwaunga mkono wanasayansi wa China kuotesha mbegu za mpunga chotara zenye mavuno makubwa, na imepata mafanikio makubwa yanayosifiwa na duniani.

Katika kipindi cha maonesho, zitaoneshwa mbegu nyingi mpya za mpunga chotara zikiwa ni pamoja na mbegu mpya aina 105 zilizooteshwa kwa unga wa maua ya aina tatu za mpunga dume, na mbegu mpya aina 46 zilizooteshwa kwa unga wa maua ya aina mbili za mpunga dume, mbegu aina 13 za majaribio ya kulinganisha uchanganyaji mpya wa mpunga chotara wa Marekani, mbegu aina 46 za majaribio ya kikanda na ya uzalishaji wa mpunga mpya na bora za mkoa wa Hainan, pamoja na mbegu aina 9 za uzalishaji wa majaribio ya mpunga mpya duniani.

Katika maonesho hayo, mtafiti wa taasisi ya sayansi ya China Bw. Yuan Longping anayesifiwa kuwa ni "Baba wa mpunga chotara" atatoa mhadhara wa utafiti wa kitaaluma. Na mtaalamu wa kuotesha mbegu za mpunga kwenye anga ya juu Bw. Xie Huaan pia atatoa hotuba kuhusu maendeleo mapya ya kuotesha mbegu kwenye anga ya juu.

Shirika la utoaji msaada wa chakula duniani hivi karibuni lilitangaza kumtunuku Profesa Yuan Longping tuzo ya chakula duniani mwaka 2004. Tuzo ya aina hiyo ilianzishwa mwaka 1986 ikikusudia kuwazawadia watu wenye mafanikio katika kutoa chakula bora na kingi kwa binadamu.

Ofisa wa kamati ya maandalizi alisema kuwa "maonesho ya mbegu mpya za mpunga chotara" yatakayofanyika kila mwaka katika siku za baadaye yataonesha mambo mengi zaidi mwaka hadi mwaka, na kuwa maonesho ya kimataifa ya mbegu mpya za mpunga chotara, na kuwa uwanja wa kimataifa wa kuonesha teknolojia ya mpunga chotara, kupeana maarifa ya uzoefu na kuendeleza biashara.

Mashirika ya hali ya juu yanayoshiriki katika maonesho ya safari hii ni pamoja na kituo cha uvumbuzi wa utafiti cha Hainan cha mpunga chotara na mimea ya ubadilishaji wa gene katika mpango No. 863 wa taifa, kituo cha taifa cha utafiti wa teknolojia ya mradi wa mpunga chotara, kituo cha taifa cha huduma ya kueneza teknolojia ya kilimo na taasisi ya China ya utafiti wa mpunga.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-08