Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-08 17:59:15    
Ngisi wa kukaanga

cri

Mahitaji

Gramu 250 za ngisi waliolowekwa, gramu 500 za mafuta yaliyopikwa, vitunguu maji, tangawizi, vitungu saumu, chumvi, M.S.G., mvinyo wa kupikia, wanga wa maji na vipande vichache vya matango.

Njia

1. Osha ngisi waliokwishalowekwa, ondoa ngozi, wapasue vipande viwiliviwili kutoka kichwani hadi mkiani. Watandaze kifudifudi kwenye ubao wa kukatia mboga na uwakate katika umbo la fungu la ngano(acha upana wa mm.3 baina ya mikato, kina cha mkato kiwe 3/4 ya maki ya nyama, halafu kata mikato ya mshadhari), na mwisho wakate vipande vyenye urefu wa sm.4 na upana wa sm.2.

2. Pitisha vipande hivyo vya ngisi ndani ya maji yanayochemka na uvitoe kwa mkupuo mmoja ili viviringike.

3. Pasha moto mafuta mpaka yawe na joto la asilimia 80 hivi, tumbukiza vipande vya ngisi ndani ya mafuta na kuvitoa nje mara moja, la sivyo nyama itakuwa ngumu.

4. Tia mafuta kidogo ndani ya sufuria, kisha yapashe moto, mimina mchuzi wenye mchanganyiko wa vitunguu maji, tangawizi, vitunguu saumu, chumvi, M.S.G., mvinyo wa kupikia, wanga wa maji na matango, baada ya mchuzi kuchemka, tia vipande vya ngisi, iepue na iandae tayari kwa kuliwa.