Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-08 19:36:56    
Mfumo wa kutumia kwa pamoja zana za utafiti wa kisayansi

cri
    Mfumo mkubwa wa kutumia kwa pamoja zana za utafiti wa kisayansi umeundwa katika mji wa Chongqing ulioko sehemu ya magharibi ya China. Hivi sasa mfumo huo utaingia katika kipindi cha kazi kwa majaribio. Tarehe 2 mwezi Desemba, serikali ya mji wa Chongqing ilitoa mwaliko kwa sekta mbalimbali za jamii kuwa wachunguzi wa sayansi wakati wowote wanaweza kutoa ombi la kutumia zana zake nyingi za utafiti wa kisayansi zenye thamani ya Yuan milioni 460 kwa kupitia tovuti ya www.csts.net.cn. ambazo nafasi zilitumiwa kwa 25% tu. Hivi sasa ufanisi wake umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

    Zamani zana kubwa kubwa za utafiti wa kisayansi hazikutumiwa ipasavyo wala hazikusimamiwa vizuri hapo. Tokea mwaka huu mji wa Chongqing umegharamia Yuan milioni 2 kuimarisha mfumo huo. Naibu mkurugenzi wa kamati ya sayansi ya mji wa Chongqing Bw. Pi Qiaoqing alisema kuwa kuanzisha mfumo wa kutumia kwa pamoja zana za kisasa za utafiti wa kisayansi ni kupanga upya matumizi ya zana za utafiti wa kiwango cha juu.

    Kamati ya sayansi ya mji wa Chongqing ilieleza kuwa mfumo wa kutumia kwa pamoja zana za utafiti wa kisayansi ni wa kwanza kwa ukubwa na ukamilifu wa utaratibu katika sehemu ya magharibi ya China. kwanza, tovuti yake inawapa watu habari kuhusu wingi wa zana hizo, namna ya kuwasiliana nao, kiasi cha malipo yanayohusika, kazi za zana hizo, ziko wapi na namna ya kuzitumia kwenye mtandao. Habari hizo zinaeleza kwa kirefu kuhusu zana kubwa 658 za utafiti wa kisayansi za mji wa Chongqing. Kamati ya sayansi ya mji wa Chongqing ikishirikiana na idara za fedha, elimu na bei za vitu, imebuni kanuni za usimamizi na utekelezaji za matumizi ya pamoja na zana za utafiti wa kisayansi. Hivi sasa katika hali ya kupata ruzuku kutoka serikali ya mji wa Chongqing, mfumo huo unapunguza malipo ya matumizi kwa kiasi cha kutoka 10% hadi 30%.

    Kuhusu mfumo wa kutumia kwa pamoja zana kubwa za utafiti wa kisayansi, naibu kiongozi wa taasisi ya usanifu wa kisayansi wa mawasiliano, Bw. Fang Boping alisema kuwa kutoka kwa upande wa watu wanaotumia zana hizo za utafiti wa kisayansi, idara husika zinaweza kuokoa fedha zilizonuia kununua zana kubwa za utafiti, hivyo gharama ya utafiti na majaribio imepungua, tena wanasayansi wanaotumia zana hizo, wanaweza kuwa na majadiliano na kubadilishana uzoefu wao.

    Kwa upande wa serikali ya Chongqing ambayo inatoa matumizi ya zana hizo, inaweza kupata malipo, ambayo yanaweza kutumika katika kuzitunza na kurudisha polepole gharama ya kuzinunua zana hizo.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-08