Tarehe 4 mwezi huu, picha za askari na makamanda wa Marekani nchini Iraq kuwadhalilisha mateka wa kivita wa Iraq zilifichuliwa, na kusababisha mshangao mkubwa duniani. Vyombo vya habari vya Marekani tarehe 6 vilitoa taarifa ikisema kuwa, ofisa mmoja wa ngazi ya juu wa wizara ya sheria ya Marekani alithibitisha kwenye barua yake aliyoikabidhi kwa maofisa wa jeshi la Marekani wanaoshughulikia kuchunguza kesi za uhalifu kuwa, wafanyakazi wa shirika la upelelezi la Marekani FBI waliwahi kuona kwa macho yao wenyewe katika kituo cha Guantanamo jinsi askari wa Marekani walivyowatesa na kuwadhalilisha wafungwa. Imefahamika kuwa, maofisa wa shirika la FBI waliwasilisha ripoti kuhusu hali hiyo kwa kikundi cha uwakili cha wizara ya ulinzi ya Marekani Januari mwaka 2003, na pande hizo mbili pia ziliwahi kufanya mashauriano kuhusu jambo hilo. Lakini ukweli umethibitisha kuwa, wizara ya ulinzi ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kuhusu jambo hilo. Muungano wa uhuru wa raia wa Marekani ACLU jana ulitangaza kumbukumbu ya serikali ya Marekani ikisema kuwa, askari wa kikosi maalum cha Marekani nchini Iraq waliowadhalilisha wafungwa walipotambua kuwa vitendo vyao vimegunduliwa na wafanyakazi wa FBI waliwatishia wasitoe taarifa kuhusu hali halisi kwa nje. Muungano ACLU ulieleza kuwa, nyaraka hizo zimefichua hali halisi ya serikali ya Marekani kuunga mkono matukio ya kuwadhalilisha wafungwa, na kujaribu kuficha ukweli wa mambo.
Lakini ni kwa nini serikali ya Bush inapuuza ukweli huo wa mambo, na kutowashughulikia wahusika?
Kwanza, vitendo vya kuwadhalilisha wafungwa viliungwa mkono na serikali kimyakimya. Gazeti la Washington Post lilichapisha makala zikisema kuwa, kutokana na waraka uliofichuliwa wa wizara ya ulinzi, serikali ya Marekani kwa kweli iliunga mkono kuchukua hatua za kikatili za kuwatesa na kuwadhalilisha wafungwa. Mwezi Aprili mwaka jana, wizara ya ulinzi ya Marekani iliidhinisha mbinu 20 za kuwatesa wafungwa, zikiwa ni pamoja na kuwavua nguo zote wafungwa na kuwanyima usingizi ili kukusanya habari kutoka kwao kwa kuwatesa. Mbinu hizo ziliidhinishwa na viongozi wa wizara ya ulinzi na kuungwa mkono na viongozi wa wizara ya sheria.
Pili, kurahisisha na kufuta matukio ya kuwadhalilisha wafungwa ni kutokana na mahitaji ya serikali ya Bush kulinda madaraka yake, na kuendelea sera yake ya upande mmoja. Ushahidi mwingi unadhihirisha kuwa, waziri wa ulinzi wa Marekani Bwana Donald Rumsfeld angewajibika kwa matukio hayo ya kuwadhalilisha wafungwa, na alikuwa analaumiwa sana kutokana na kashfa hizo, lakini hadhi yake nchini Marekani haikuathirika hata kidogo. Sababu ya rais Bush kumlinda Bwana Rumsfeld ni kwamba, Rumsfeld ni mtekelezaji thabiti wa sera zake za kuchukua vitendo kabla kushambuliwa na upande mmoja katika kipindi chake cha pili. Matukio ya kuwadhalilisha wafungwa yakishughulikiwa kwa makini, haina tofauti na kujipalia moto, kama ni hivyo basi si kama tu hadhi ya Rumsfeld haiwezi kudumishwa, bali pia yataitikisa serikali ya Bush, na kuleta athari mbaya kwa Marekani kuendelea kufuata sera kali ya upande mmoja.
Idhaa ya kiswahili 2004-12-08
|