Fedha nyingi haziwezi kuwaokoa wagonjwa wa Ukimwi, na dawa ya kutiba ugonjwa wa Ukimwi bado haujapatikana, kutokana na wazo hilo kauli nyingi za kukatisha tamaa yamekuwa zikitokea duniani, zikisema kuwa fedha zinazotumika kwa ajili ya tiba ya Ukimwi ni hasara tupu. Lakini hivyo sivyo ukweli ulivyo.
Tuchukue Brazil kama ni mfano. Mwaka 1996 nchi hiyo ilikuwa ya kwanza duniani kutoa mpango wa kusambaza dawa za Ukimwi kwa bei ya chini, na kwa ajili ya kutekeleza mpango huo serikali ya Brazil ilitumia dola za Kimarekani milioni 180. Kutokana na takwimu, tokea mwaka 1996 hadi 2002, wagonjwa wa Ukimwi zaidi ya laki moja walipata tiba bure, walioathirika walipungua kwa asilimia 80, waliolazwa hospitali pia walipungua kwa kiasi kikubwa. Mtaalamu wa Ukimwi, daktari maafuru wa Brazil aliwahi kufanya hesabu, akisema kuwa katika muda huo kutokana na wagonjwa wa Ukimwi na watu walioathirika kupungua kwa kiasi kikubwa, serikali imeokoa fedha za ruzuku za matiba dola za Kimarekani bilioni 2 licha ya kuwaingiza katika hesabu wagonjwa wengi waliokuwa hawajalazwa hospitali.
Mfano mwingine kuwa, hospitali moja ya nchi ya Cote d'Voire siku chache zilizopita ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari vya Ufaransa ikisema kuwa tokea mwaka 1995 hadi 1999 Ukimwi ulikuwa ni chanzo kikubwa cha vifo vya wafanyakazi wa Shirika la Umeme la nchi hiyo. Tokea hapo shirika hilo lilitumia dola za Kimarekani laki 2.1 kwa ajili ya kutoa tiba bure kwa wagonjwa wa shirika hilo, na katika muda wa miaka miwili tu kiasi cha wagonjwa wa Ukimwi waliokufa kilipungua kwa asilimia 60, na waathirika wapya walipungua kwa asilimia 78 ikilinganishwa na hapo kabla, na kiasi cha wagonjwa waliolazwa hospitali kimepungua kwa asilimia 81. Kutokana na hali hiyo shirika hilo liliokoa dola za Kimarekani laki 5.6.
Isitoshe, mwaka 2003 Benki ya Dunia ilitoa taarifa, ikisema kuwa nchini India fedha kwa ajili ya maisha ya mgonjwa wa Ukimwi kwa mwaka mmoja haifikii dola za Kimarekani 300, fedha hizo ni kiasi kidogo sana ikilinganishwa na wastani wa thamani za bidhaa zilizozalishwa nchini humo na mtu mmoja. Fedha zinazotumika kuzuia maambukizi ya watoto wachanga kutoka kwa mama mzazi kwa kila mmoja ni dola za Kimarekani 30, kila nchi inaweza kumudu kiasi hicho cha fedha. Lakini faida ya fedha hizo inaweza kuonekana katika sekta mbalimbali.
Hata nchi zilizoendelea haziwezi kujitenga na hali ya ugonjwa wa Ukimwi katika nchi nyingine. Mwaka 2001, taarifa ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa nchi kubwa za viwanda kama Marekani, kila mwaka inatoa fedha chini ya asilimia 1 ya bajeti yake ya miradi ya nchi za nje, kusaidia nchi zinazoendelea katika tiba ya Ukimwi. Lakini Ukimwi sio wa nchi fulani bali ni wa dunia nzima, na unahitaji fedha nyingi. Ofisa mwandamizi wa mambo ya Ukimwi nchini Marekani aliwahi kusema kuwa Afrika ni chimbuko kubwa la nishati, lakini Ukimwi umekuwa ukienea kwa kasi mno barani humo, msimamo wa kupuuza hali ya ugonjwa huo barani Afrika kutaathirisha vibaya vitega uchumi vya Marekani na faida zake kutoka bara la Afrika.
Kutokana na hali hiyo, fedha kwa ajili ya tiba ya Ukimwi inahusika moja kwa moja uchumi wa dunia nzima, na hakuna nchi hata moja inayoweza "kuwa salama". Kama mtaalamu wa uchumi wa Ufaransa alivyosema katika mkutano wa Ukimwi duniani uliofanyika mwaka jana, kwamba "tiba ya Ukimwi sio tu suala la kibinadamu, bali zaidi ni suala la faida za kiuchumi."
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-09
|