Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-09 19:34:51    
Mazungumzo ya amani ya Ireland ya kaskazini yakwama, lakini bado kuna matumaini

cri

    Duru jipya la juhudi za serikali ya Uingereza, serikali ya Ireland na vyama vikubwa vya madhehebu yanayopingana jana zimetangaza kushindwa kwa duru jipya la mazungumzo yaliyofanywa kwa kuondoa hali ya mkutano ya mazungumzo ya amani ya Ireland ya Kaskazini jana. Lakini viongozi wa nchi hizo mbili bado wanaona kuwa mazungumzo yamepata maendeleo makubwa na kuamini kuwa pande hizo mbili hatimaye zitaweza kufikia makubaliano mwishowe.

    Serikali ya Uingereza na serikali ya Ireland zilizoandaa mazungumzo hayo zilitarajia pande hizo mbili kufikia makubaliano, lakini kiongozi wa chama kikuu cha madhehebu ya Protestanti chama cha Demokrasia na Umoja (DUP) cha nchi hiyo Bw. Ian Paisley, ambaye ni pande moja kubwa ya mazungumzo hayo, siku hiyo baada ya kukutana na mkuu wa jumuiya ya kimataifa ya usimamizi isiyopendelea upande wowote ambayo inashughulikia kusimamia hatua ya kunyang'anya silaha kutoka kwa makundi ya wanamgambo ya nchi hiyo Januali John De Chastelain, alitangaza kuwa, kutokana na kundi kubwa la wanamgambo wa madhehebu ya liitwalo "Jeshi la Jamhuri ya Ireland" (IRA) kukataa kupigwa picha katika hatua ya kunyang'anya silaha, chama cha DUP hakikuweza kusaini makubaliano na kundi kubwa la madhehebu ya Katoliki yaani Sinn Fein.

    Ingawa duru hilo la mazungumzo limeshindwa, lakini waziri mkuu wa Uingereza Bw. Tony Blair na waziri mkuu wa Ireland Bw. Bertie Ahern bado wanaona kuwa mazungumzo hayo yamepata maendeleo makubwa. Kwanza, jeshi la IRA limekubali kwa mara ya kwanza kutangaza kuacha vitendo vya kimabavu, na kuacha silaha zote kabla ya mwishoni mwa mwaka huu. Hatua hiyo itatatua kikamilifu suala la kunyang'nya silaha kutoka kwa IRA, ambalo limesumbua mchakato wa amani ya Ireland ya Kaskazini tangu kusaini mkataba wa amani wa nchi hiyo mwaka 1998.

    Pili, chama cha DUP chenye msimamo thabiti kimekubali kwa mara ya kwanza kushirikiana na chama cha upinzani Sinn Fein katika serikali ya muungano. Chama cha DUP kilikuwa kinapinga kithabiti mkataba wa amani ya nchi hiyo na ushirikiano na chama cha Sinn Fein, na hata kilikataa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na chama cha Sinn Fein. Chama cha DUP kubadilisha msimamo wake kuna umuhimu wa kihistoria.

    Aidha, chama cha Sinn Fein kwa mara ya kwanza kimefikia makubaliano na serikali ya Uingereza kuhusu kushiriki kwenye usimamizi wa polisi wa nchi hiyo na utekelezaji wa sheria. Hatua hicho imesukuma mbele ushirikiano kati ya vyama vya madhehebu yanayopingana.

    Ili kuimarisha maendeleo yaliyopatikana katika mazungumzo hayo, Bw. Blair na Bw. Ahern siku hiyo walikwenda huko Belfast, mji mkuu wa Ireland ya Kaskazini, na kutangaza mapendekezo mapya yaliyotelewa na serikali za nchi hizo mbili kwa pande za mazungumzo tarehe 17 mwezi Novemba. Kwa upande mmoja, zinataka kuthibitisha kwa maandishi maudhui ya maafikiano yaliyopatikana katika mazungumzo; kwa upande mwengine, zinataka umma kuwa na maoni kuhusu masuala yaliyotokea katika mazungumzo ili kusimamia na kusukuma mbele mazungumzo hayo katika siku za baadaye.

    Wachambuzi wanaona kuwa, ingawa duru hilo la mazunguzmo limeshindwa, lakini maendeleo yaliyopatikana yataweza kuthibitishwa kuwa ni ya kihistoria, na bado kuna matumaini kwa pande hizo mbili kufikia makubaliano. Hivi sasa, serikali ya Uingereza na serikali ya Ireland zinapaswa kufanya uamuzi: kuendelea kusaidia kutatua matatizo yaliyopo au kufuata njia nyingine. Ya kwanza, serikali za nchi hizo zinapaswa kufanya uchambuzi kutafuta njia ya kukwepa vikwazo vilivyopo hivi sasa, au kuzifanya pande hizo mbili kuafikiana kuhusu suala la kupiga picha katika hatua ya kunyang'anya silaha kupitia mbinu za kiteknolojia ili kulinda maafikiano yaliyopatikana. Kama hazitapata njia ya kukwepa vikwazo, zitafikiria kutumia njia nyingine, zikiwa ni pamoja na kupunguza jeshi la Uingreza nchini humo, kutatua suala la watuhumiwa wa kigaidi wa IRA waliotoroka na kuwaachia huru wafungwa wa IRA, ili kubadilisha ushirikiano wa pande hizo mbili katika bunge la nchi hiyo na serikali ya muungano kwa masharti fulani.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-09