|
Wakati mkutano wa 7 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya unafanyika huko The Hague, Uholanzi, China na Umoja wa Ulaya jana zilisaini "Taarifa ya pamoja kuhusu kuzuia kuenea kwa silaha na kudhibiti zana za kijeshi", na kuthibitisha kuwa China na Umoja wa Ulaya, ni wenzi wakubwa wa kimkakati kwa upande mwingine katika nyanja hiyo.
Taarifa hiyo ya pamoja ni waraka wa kwanza uliosainiwa na China na nchi nyingine kuhusu kuzuia kuenea kwa silaha na kudhibiti silaha, ambayo imeonesha hali ilivyo ya ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya katika nyanja hiyo,. Pia waraka huo umethibitisha wazi lengo halisi la ushirikiano huo kati ya pande hizo mbili katika nyanja hiyo. Mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera ya kidiplomasia na usalama Bwana Javier Solana alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema:
Baada ya kutiwa saini kwa taarifa hiyo ya pamoja, Umoja wa Ulaya na China zitaanzisha ushirikiano katika nyanja husika mbalimbali, hasa kuimarisha udhibiti wa raslimali ambazo huenda zitatumika katika kutengeneza silaha kali.
Taarifa hiyo ya pamoja inasema kuwa, China na Umoja wa Ulaya zikiwa nguvu kubwa katika nyanja ya usalama wa kimataifa, zinabeba jukumu kubwa katika kulinda amani, usalama na utulivu wa kimataifa na kikanda, na pande hizo mbili zitaendelea kufanya juhudi kwa kusukuma mbele kazi ya kuzuia kuenea kwa silaha duniani. Taarifa hiyo hakika ina umuhimu mkubwa kwa ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya hata na nchi nyingine katika nyanja hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya udhibiti wa zana za kijeshi katika Wizara ya mambo ya nje ya China Bwana Liu Jieyi alipohojiwa alisema kuwa, kuzuia kuongezeka kwa usambazaji wa silaha ni suala muhimu katika dunia ya hivi sasa, suala hilo linahusiana na amani na utulivu wa dunia. China na Umoja wa Ulaya zina maslahi makubwa ya pamoja katika nyanja hiyo. Alisema:
Katika taarifa hiyo China na Umoja wa Ulaya, kila upande unauchukulia upande mwingine kuwa ni mwenzi mkubwa wa ushirikiano katika kudhibiti silaha na kuzuia kuenea kwa silaha, hii imeonesha kuwa pande hizo mbili zinazingatia sana suala hilo na zinataka kuimarisha ushirikiano katika nyanja hiyo.
Katika miaka kadhaa iliyopita, ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya katika nyanja ya kuzuia kuenea kwa silaha na kudhibiti zana za kijeshi unaimarika na kuongezeka siku hadi siku. Sababu moja kubwa inatokana na maslahi makubwa ya pamoja ya pande hizo mbili katika nyanja hiyo. Kusainiwa kwa taarifa hiyo kumeleta nafasi nzuri sana kwa kuimarisha zaidi maingiliano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika nyanja hizo.
Bwana Liu Jieyi anaona kuwa, taarifa hiyo ina umuhimu kwa China na Umoja wa Ulaya, pia itafanya athari zenye juhudi kwa jumuiya ya kimataifa. Akisema:
China na Umoja wa Ulaya kuimarisha ushirikiano katika kuzuia kuenea kwa silaha na kudhibiti zana za kijeshi, kwanza kunatokana na maslahi ya pamoja, na maslahi hayo pia yanalingana na maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa, hivyo kuimarisha ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya katika nyanja hizo pia kutaleta faida na maslahi kwa nchi mbalimbali duniani.
Bwana Liu ameainisha pia kuwa, kutiwa saini kwa taarifa hiyo ya pamoja pia kuna umuhimu katika kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi, kwani China na Umoja wa Ulaya zimesaini makubaliano mengi muhimu kuhusu udhibiti wa zana za kijeshi kati ya pande nyingi, kama vile mkataba wa kupiga marufuku silaha za kemikali, mkataba wa kupiga marufuku silaha za kiviumbe na mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia. Pia China na Umoja wa Ulaya zimefanya ushirikiano na kufanya kazi nyingi katika kutekeleza mikataba hiyo na kulinda heshima na maamuzi ya mikataba hiyo, hii vilevile inalingana na maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.
Idhaa ya Kiswahili2004-12-09
|