Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-10 15:37:58    
Jumuiya ya OPEC yapunguza uzalishaji na kudumisha bei au la?

cri

    Mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Jumuiya ya OPEC leo utafanyika huko Cairo, mji mkuu wa Misri ili kuthibitisha uzalishaji wa mafuta ghafi wa nchi wanachama za OPEC katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2005. Hali ambayo OPEC itaendelea na uzalishaji wa hivi sasa au kupunguza uzalishaji ili kudumisha bei italeta athari kubwa kwa soko la mafuta ghafi la kimataifa, hivyo mkutano huo unafuatiliwa sana.

    Kutokana na hotuba zilizotolewa na mawaziri wa nchi wanachama kwa vyombo vya habari kabla ya mkutano huo, sauti ya kupunguza uzalishaji na kudumisha bei ni kubwa. Waziri wa mafuta wa Libya Bw. Fathi Hamed Ben Shatwan alisema kuwa, kwanza nchi wanachama wa OPEC isipokuwa Iraq, lazima zitekeleze uzalishaji wa mafuta ghafi kwa mapipa milioni 27 kila siku. Kama bei ya mafuta itaendelea kuanguka, basi inapaswa kupunguza uzalishaji wa kila siku. Maneno hayo ya Bw. Shatwan yanamaanisha kuwa, kuanzia mwaka kesho, nchi wanachama wa OPEC zitapunguza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa milioni 1 hadi milioni 1.5 wa kila siku. Waziri wa nishati wa Kuwait Bw. Ahmed Fahdal-Sabah pia alimuunga mkono. Alipendekeza kuwa, kuanzia miezi mitatu ya pili ya mwaka kesho, jumuiya hiyo itapunguza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa 500,000 kwa siku. Waziri wa nishati, viwanda, umeme na maji wa Qatar Bw. Abdullah Bin Hamad al-Attiyah alieleza wasiwasi wake kwamba katika miezi mitatu ya pili ya mwaka kesho mahitaji ya mafuta yataweza kupungua na hivyo kusababisha bei ya mafuta kuendelea kuanguka. Alisema kuwa, kama mkutano huo utaafikiana kuhusu kupunguza uzalishaji wa kila siku, Qatar itaunga mkono. Waziri wa nishati na madini wa Venezuela Bw. Rafael Ramirez alisema kuwa, Jumuiya ya OPEC lazima itoe uamuzi wa kudumisha bei. Iran pia imeeleza kuunga mkono kupunguza uzalishaji ili kudumisha bei ya mafuta.

    Vilevile baadhi ya nchi wanachama za OPEC hazikubali kutoa uamuzi wa kupunguza uzalishaji mara moja kutokana na kutuliza bei ya mafuta. Mwenyekiti wa OPEC, ambaye pia ni waziri wa nishati wa Indonesia Bw. Purnomo Yusgiantoro jana huko Cairo aliwaambia waandishi wa habari kwamba, kwa kuwa hivi sasa mafuta ya ghafi yanahitajika sana, hivyo bei ya mafuta bado inaendelea kuwa juu na Jumuiya ya OPEC inaziruhusu nchi wanachama kuzalisha mafuta yanayozidi mgao. Saudi Arabia, Algeria na Nigeria zinaridhiwa na hali ya uzalishaji wa mafuta wa OPEC ya hivi sasa na hazina wasiwasi kuhusu bei ya mafuta kuanguka hivi karibuni. Zimependekeza OPEC kufanya mkutano mwezi March, mwaka kesho ili kutathmini hali na kutoa uamuzi husika.

    Bei ya mafuta ya soko la kimataifa kuanzia mwezi Mei mwaka huu imeanza kupanda, na mwezi Oktoba mwaka huu bei ya mafuta ilivunja rekodi ya dola 55 za kimarekani na kuweka rekodi ya juu kabisa ambayo ni dola 55.67 za kimarekani. Baada ya mwezi Novemba, bei ya mafuta ilianza kuanguka. Sababu muhimu ni kuwa akiba ya mafuta ya Marekani, ambayo ni nchi kubwa kabisa inayotumia mafuta, imekithiri. Wachambuzi wa soko wanakadiria kuwa, kwa sababu uchumi wa dunia unaweza kuendelea pole mwakani, na mahitaji ya mafuta ya kila siku duniani yatapungua, hivyo ni vigumu kwa bei ya mafuta mwakani kupanda. Aidha, ingawa mapato ya nchi wanachama za OPEC yanaongezeka kutokana na bei ya mafuta kupanda, lakini kushuka thamani kwa dola za kimarekani kumeleta hasara kwa nchi zinazoalisha wa mafuta ambazo zinatumia dola za kimarekani kuwa njia ya kuuza mafuta. Hivyo, mkutano wa Cairo unaweza kutoa uamuzi wa kupunguza uzalishaji ili kudumisha bei ya mafuta baada ya kutathmini hali ya mahitaji na utoaji wa mafuta katika miezi mitatu ya kwanza ya mwakani. Suala la hivi sasa ni lini OPEC itaanza kupunguza uzalishaji na itapunguza kwa kiasi gani.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-10